Tafuta

Vatican News
Patriaki Nasrallah Sfeir wa Kimaroniti nchini Lebanon ameaga dunia tarhe 12 Mei 2019 Patriaki Nasrallah Sfeir wa Kimaroniti nchini Lebanon ameaga dunia tarhe 12 Mei 2019   (ANSA)

Kifo cha Kard Nasrallah Boutros Sfeir,Patriaki wa Kanisa la Maroniti,Lebanon

Tarehe 12 Mei 2019 Kardinali Nasrallah Boutros Sfeir, Patriaki wa Kanisa la Maroniti tangu 1986 hadi 2011 ameaga dunia huko Beirut Lebanon akiwa na umri wa miaka 99.

Na Sr Angela Rwezaula -Vatican

Tarehe 12 Mei 2019, asubuhi, huko Beirut Kardinali Nasrallah Boutros Sfeir,Patriaki wa Kanisa la Maroniti tangu 1986 hadi 2011 amefariki dunia na ambaye tarehe 15 Mei 2019 alikuwa anatimiza miaka 99. Kufuatia na kifo chake,Kanisa la Kimaroniti limepoteza sura muhimu ya historia ya nchi  ya Lebanon kwa ujumla katika Kanisa na kijamii.

Alizaliwa tarehe 15 Mei  1920  huko Reyfoun karibu na Kesrouan nchini Lebanon. Alipewa daraja Takatifu la Upadre kunako tarehe 7 Mei  1950. Kardinali  Sfeir alikuwa ni profesa wa masomo ya filosofia na tafsiri nyingi za maandishi matakatifu  katika Taasisi ya watawa wa Mariamite wa Jounieh kabla ya kuchaguliwa kuwa askofu mwaka 1961, wa Tarso ya Kimaroniti na Kaimu Mkuu wa Upatriaki wa Antiokia na baadaye kupewa daraja la uaskofu enzi za Patriaki  wa Kardniali Paul Pierre Méouchi wa Kanisa la Kimaroniti.

Alikuwa amechaguliwa kuwa Patriaki wa 79 wa Antiokia ya Kimaroniti kunako tarehe 19 Aprili 1986 wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Lebanon na kuendelea na upatriaki huo. Baadaye alichaguliwa kuwa Rais wa Sinodi ya Kanisa la Maroniti na Rais wa Baraza la Maaskofu Lebanon. Katika shughuli hiyo pia mwaka 2006 akaongezewa kuwa Rais wa Baraza la Mapatriaki Katoliki nchi za Mashariki.

Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa Kardinali kunako tarehe 26 Novemba 1994. Alikuwa ameng’atuka shughuli za Upatriaki wa Kimaroniti na shughuli nyingine za kichungaji kunako tarehe 26 Februari 2011. Na tarehe 15 Machi 2011 alichaguliwa Patriaki wa sasa ambaye ni  Béchara Boutros Raï.

Kuafuatia na kifo chake, kwa sasa Baraza la makardinali wamebaki 221 na kati yao 120 wanaweza kuchaguliwa na 101 hawawezi kupiga kwa mujibu wa mri wao.

13 May 2019, 09:53