Tafuta

Vatican News
Tarehe 10-12-Mei, Vijana wakiwa katika Kongamono la Maria katika madhabahu ya Mtakatifu Gabrieli wa Mateso huko Teramo Italia Tarehe 10-12-Mei, Vijana wakiwa katika Kongamono la Maria katika madhabahu ya Mtakatifu Gabrieli wa Mateso huko Teramo Italia  

Kard.Parolin:Kongamano Vijana:kutoka Mtakatifu Gabrieli hadi Mt.Yohane Paulo II!

Wakati wa hitimisho la liturujia ya Mkesha wa Maria katika Madhabahu ya Mtakatifu Gabrieli wa Mateso, huko Teramo Italia tarehe 11 Mei 2019,Kardinali Pietro Parolin ametoa tafakari yake.Hili ni Kongamano la vijana lililoongozwa na mada:kutoka kwa Mtakatifu Gabrieli hadi Mtakatifu Yohane Paulo II:Siku ya vijana katika maisha ya Kanisa na ulimwengu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wakati wa hitimisho la liturujia ya Mkesha wa Maria katika Madhabahu ya Mtakatifu Gabrieli wa Mateso, huko Teramo Italia tarehe 11 Mei 2019, Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican alitoa tafakari yake kwa vijana hawa. Mkesha huo ulianza saa 10.00  jioni masaa ya ulaya ambao unajikita katika mantiki ya Kongamano la vijana Kimataifa  likiongozwa na mada:“kutoka kwa Mtakatifu Gabrieli hadi  Mtakatifu Yohane Paulo II:Siku ya vijana katika maisha ya Kanisa na ulimwengu;kongamano lililoanza  tarehe 10 hadi 12 Mei 2019 lenye kuwashirikisha hata vijana wengi katika pembe za dunia.

Mada ya mkesha:Hayupo hapa amefufuka

Kardinali Petro Parolin amesema, ni furaha kubwa kukutana nanyi mchana huu na kwa kutazama wingi wenu mliofika katika mkesha wa kimataifa wa Maria. Ninawasalimia kwa salam ya kindugu na maneno ambayo Baba Mtakatifu Francisko alianza nayo wakati wa mahubiri yake katika ziara yake ya hivi karibuni nchini Bulgaria na  Macedonia ya Kaskazini kwamba: Kristo amefufuka! Ni salam ya kiutamaduni ambayo wakristo wa nchi za  Mashariki wanasalimiana katika kipindi cha Pasaka na ambapo wote wanajibu: “Kweli kweli kafufuka!”na  mara moja salam hiyo inamulika moja kwa moja katika mada ya Mkesha huo iliyochaguliwa “hayupo hapa  Amefufuka:katika safari na Maria!”

Kardinali Parolini akiendelea na tafakari yake anesema zaidi ya vijana waliunganika pale, pia amependa kuwasalimia wengine ambao wanafuatilia  mkesha wa pamoja kupitia saltelite, na kuwashukuru kwamba wanaweza kufanya uzoefu hai  wa umoja wa Kanisa lote dunia na ambao  ni ishara  na chombo ambacho kama iulivyokumbusha  Mtaguso II wa Vatican ( LG n.1).  Kwa njia ya mkesha huo ni   kuwa na mwanzo wa safari ya kijiandaa na maadhimisho ya miaka 100 tangu kutangazwa kwa Mtakatifu Gabrieli wa Mateso, msimamizi wa vijana wakatoliki nchini Italia na Abruzzo

Uhusiano wa nguvu kati ya jina la Gabrieli na vijana

Kardinali  katika tafakari yake amependa kutoa umakini juu ya uhusiano wa nguvu wa jina la Gabrieli wa Mateso na vijana wa Amerino kama yeye alivyo kuwa akipenda kuwaita marafiki zake na Mama Maria, mama yake Yesu, kwamba “hata sisi  tunaalikwa katika mkesha huu kumfikiria Mtakatifu Gabrieli kurudia kutazama ndani ya moyo na akili, chini ya Msalaba pamoja na mateso ( Yh 19,25). Maria chini ya miguu ya msalaba alishuhudia kwa nguvu yake, ujasiri wake na matumaini yake kwamba Msulibwa hasingeweza kubaki kaburini! Maria hakuwa na haja ya kwenda kutazama  kaburi au kuuliza kama  alivyo fanya Tomasi, na kujibiwa kwamba  “weka kidole chako na ubavuni (Yh, 20,25)”. Yeye aliamini Yesu aliyemwona akikua, akifanya kazi, akihubiri na kutoa maisha kwa ubinadamu.

Kardinali Parolin anawataka vijana wasiwe na hofu ya kupokea changamoto za wakati wetu hasa zinazotazama utandawazi na utafiti wa kisayansi. Badala yake ni zawadi kubwa na fursa ya kuweza kuishi na kuwa sehemu ya jamii inayptakiwa  kujengwa  hata kwa njia ya mchango wao. Aidha amesema Yesu siyo nabii wa ujumbe mpya wa kidini au kijamii, bali ni kama alivyombusha Mtakatifu Yohane Paulo II katika Wosia wake wa Redemptor Hominis,” kuwa:  “ni Kiini cha dunia na cha Historia  (n. 1)”.

Mtakatifu Gabrieli alishuhudia yeye  binafsi kwamba bila Ufufuko haiwezakani kuishi kikamilifu  

Mtakatifu Gabrieli alishuhudia yeye binafsi kwamba bila Ufufuko haiwezakani kuishi kikamilifu maisha. Yeye alitafuta kila njia ya kuweza kukwepa na hatimaye alithibtisha ni kwa jinis gani haiwezekani na ndipo kukubali kwa sababu maisha yake yalikuwa makamilifu kwake yeye tu aliye hai. Kardinali Parolin anaouhakika kwamba, ni kwa njia ya maandalizi na matukio ya maadhimisho ya miaka 100 ya kutangazwa kwa Mtakatifu Gabrieli, itakuwa ni zawadi kubwa si tu kwa Kanisa laTeramo- Atri lakini hata  kwa ajili ya   Kanisa lote. Kwa uwepo wa idadi kubwa za taasisi nyingi za Kanisa na ambazo anawashukuru kwa ushiriki huo na msaada wa kuanzishwa kwa mipango hiyo, amesema  ni ishara hai ya ushuhuda wa pamoja na ambao kuna uwezekano wa kuhudumia vizazi vijavyo ili kuwa na ubunifu wa huduma ya kudumu. Anawakabidhi mikononi mwa  Mama Maria na Mtakatifu Gabrieli wa Mateso na Mtakatifu Yohane Paulo II vijana wote duniani na kuwaalika wakaribishe kwa furaha na shukrani na Baraka ya Mungu.

Kongamno la mkesha lilikuwa la kimataifa na kuuunga na wenzao

Kongamno la mkesha lilikuwa la kimataifa ambapo walikuwa wameunganika na vijana kutoka sehemu mbalimbali kama vile huko: Czestochowa Poland, katika  Kanisa la Kadhabahu ya Jasna Gora, kwa kuadhimishwa na Askofu Andrzej Przybylskj, msaidizi wa madhabahu ya Czestochowa; huko Montevideo nchini Uruguay, katika Parokia  ya  Stella Maris wa Montevieo, alikuwa anaadhimisha  Kardinali  Daniel Fernando Sturla Berhouet, sdb, Askofi Mkuu wa Montevideo;  Huko Nitra nchini Slovakia, katika Kanisa la Kutembelewa  Maria Mtakatifu,akiadhimisha Askofu Villiam Judák, wa  Nitra;  na hko Nairobi Kenya, Kutoka Ukumbi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika Mashariki CUEA, aliyekuwa anaadhimisha ni  Padre  Boniface Mungai, Msimamizi wa Kanisa dogo la CUEA; Huko  Hyderabad nchini India, kutoka  Seminari Kuu ya Kansa ya Mtakatifu Yohane, aliyekuwa anaadhimisha ni  Askofu Mkuu Thumma Bala, wa  Hyderabad. Kwa maana hiyo lilikuwa ni tukio moja kubwa la Kongamano hili la vijana kuhusu Mama Maria.

12 May 2019, 10:57