Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu wakati wa kukutana na wawakilishi wa Kamati ya Wayahudi kutoka Marekani tarehe 8 Machi 2019 Baba Mtakatifu wakati wa kukutana na wawakilishi wa Kamati ya Wayahudi kutoka Marekani tarehe 8 Machi 2019  (ANSA)

Kard.Koch:Unatakiwa mshikamano zaidi barani Ulaya!

Kardinali Kurt.Koch nje ya Mkutano wa 24 wa Kimataifa“Liaison Committee”akihojiana na mwandishi wa habari wa Sir anasema,Ulaya inaishi leo hii na kipeo kikubwa hasa cha wahamiaji.Tunaweza kupata suluhisho la changamoto kubwa hiyo iwapo kuna mshikamano kati ya nchi zote,maana hatuwezi kuachia baadhi ya nchi kuendesha suala la mapokezi ya wahamiaji peke yake.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tukio la uhamiaji na  ubaguzi wa rangi unaoendelea kukua hasa zaidi katika bara la Ulaya na mateso ya wakristo leo hii, ndiyo changamoto na mada zilizopo katika kitovu kwa mwaka huu kwenye Mkutano wa 24 wa Kimataifa “Liaison Committee (Ilc)”, ambapo kati ya washiriki ni pamoja na Tume ya Vatican kwa ajili ya mahusiano ya kidini na  Kamati ya Kimataifa ya Wayahudi kwa ajili ya Majadiliano ya kidini (Ijcic). Mkutano huo umeanza tarehe 14-16 Mei 2019 ambao unajikita katika mijadala mbalimbali na kubadilishana tafakari kati ya wataalam, wawakilishi wa Vyama, mashirika na waandishi wa habari, wakiongozwa na mada “ watu, mawazo na mipaka katika mwendo”. Vile vile hata mkutano kuhusu  kambi ya wakimbizi wa Siria, wa Eritrea na Afghanstan katika  shule ya lugha na utumaduni wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio huko Trastevere Roma.

Uchanguzi wa tema ya watu katika mzunguko

Kardinali Kurt Koch, Rais wa Baraza la Kipapa la kuhamasisha Umoja wa wakristo  na wa Tume  ya Kipapa kwa ajili ya mahusiano ya dini ya kiyahudi akizungumza kuhusiana na mazungumzo ya kina na ambayo yameanzishwa kwa kipindi kirefu, kando ya mkutano huo  na mwandishi wa Gazeti la Sir, amefafanua kwa kirefu lengo kuu la kuchagua tema kuhusu “watu,mawazo na mipaka katika mwendo” kwamba, mara nyingi zinachaguliwa tema kwa  pamoja katika mwanga wa changamoto za dunia yetu, na mwaka huu 2019 uchaguzi umeangukia katika tema kubwa sana ya uhamiaji, ubaguzi wa rangi na ambalo  ni tukio linalozidi kukua barani Ulaya, lakini pia hata mateso ya wakristo na uhuru wa kidini. Haya ni masuala ambayo yanakabiliana na Wayahudi na Wakatoliki. Ni muhimu sana kushirikishana njia za pamoja katika changamoto hizi ili kutafuta kwa pamoja na  kupata mapendekezo ya majibu ya kawaida, lakini kwa  pamoja! Vile vile hii ni fursa za kuimarisha kwa kina urafiki kati ya Makanisa Katoliki na Wayahudi ambayo kwa hakika ni muhimu sana, amesisitiza Kardinali Koch.

Kufunga mipaka Ulaya na kuenea kwa ubaguzi

Amefafanua juu ya suala la Ulaya kufunga mipaka yake na kwa bahati mbaya  ubaguzi wa rangi kuenea karibu kila sehemu na wakati huo huo wakristo katika dunia wanateseka na kuteswa sana. Katika ujumbe wa Kardinali Koch anao utoa kwa waamini wenye imani amesema, kwa sasa kuna tatizo kubwa katika jamii zetu. Tatizo linalotazama hasa dini na kwa sasa hata mmoja kushiriki na kuwa sehemu ya dini inaogopesha. Lakini hata hivyo amefafanua kuwa,  katika jamii kuna dalili nyingi tofauti kwa mfano  wapo wanajeshi, polisi, hata wanafunzi. Kila mmoja ana ishara yake mwenyewe na ni ya umma. Ni ishara za kidini pekee  yake zinaleta matatizo! Hii ina maana kwamba katika jamii zetu hazina maono mazuri  ya dini, kwa namna hiyo hii ni changamoto muhimu sana hasa katika jamii zetu leo hii ambazo zinazidi kuwa na dini nyingi zaidi. Ikiwa dini inapoteza nafasi yake ya umma na kuruhusiwa kwenye nyanja ya faragha, kama jamii amesisitiza, tunapoteza uwezo wa kuingilia mazungumzo na kila mmoja na kwa maana hii ni  muhimu kuzungumza juu ya nafasi ya umma ya dini.

Tukio la uhamiaji lipo mahali popote duniani na wala siyo uvamizi

Akijibu swali kwamba ikiwa wahamiaji wanaogopesha, je  ni jinsi gani ya kukabiliana na suala la uhamiaji? Kardinali Koch amethibitisha kuwa, katika mkutano huo, umefunguliwa na mada nzuri sana ya hali halisi ya wahamiaji na ambapo wameona ni kwa jinsi gani  kuna ujinga mkubwa. Wengi wanaogopa hali halisi ambayo haipo. Watu wengi wa Ulaya leo hii wana hisia kama vile ya uvamizi wa wahamiaji, lakini hii si kweli. Uhamiaji awali ya yote ni tukio lolote lile ambalo lipo duniani kote. Kwa njia hiyo ni muhimu kuwafanya watambue hali halisi kama inavyo jiwakilisha yenyewe na kuwa na imani ya hali halisi hiyo! Pia inahitaji kuchukua hali halisi ya wasiwasi wa watu kwa kiasi kikubwa na kutoa majibu mazuri kulingana na ukweli huo hasa katika kukabiliana na ukweli na hofu hizo, amesisitiza Kardinali Koch.

Je Ulaya iseme  nini kwa wayahudi na wakatoliki ?

Hatimaye Kardinali Koch akijibu swali kuhusu nini Ulaya inapaswa kusema juu ya wayahudi na wakatoliki amethibitisha kwamba Ulaya kwa sasa inaishi kipeo kikubwa hasa kwa sababu ya uhamiaji. Inakosekana mshikamano, hata kati ya watu tofauti wa nchi. Kutokana na hilo tunaweza kutatua matatizo makubwa ya changamoto ya uhamiaji iwapo tunaweza kuwa na mshikamano  wa dhati kati ya nchi tofauti. Hatuwezi kuachia baadhi ya nchi peke yake kuendesha masuala ya ukarimu na kukaribisha wahamiaji. Inahitajika kwa namna hiyo kuboreshwa kwa mazungumzo kati ya Nchi tofauti ili kuweza kutatua tatizo hilo kubwa, amehitimisha Kardinali Koch, Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya umoja wa Wakristo.

16 May 2019, 11:01