Tafuta

Vatican News
Tarehe 7 Mei 2019, Baba Mtakatifu amefika Macedonia Kaskazini na kupolewa na Rais wa nchini Tarehe 7 Mei 2019, Baba Mtakatifu amefika Macedonia Kaskazini na kupolewa na Rais wa nchini  

Hija ya Kitume:Papa amefika Macedonia Kaskazini katika ishara ya Mama Teresa!

Baba Mtakatifu anahitimisha ziara ya 29 ya kitume kwa siku tatu,akitokea Bulgaria na ametua nchini Macedonia ya Kaskazini katika mji wa Skopje.Siku hii itakuwa katika ishara ya Mama Teresa wa Calcuta.Mama ambaye alizaliwa katika mji huu wa Macedonia kunako tarehe 26 Agosti 1910.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 7 Mei 2019 Baba Mtakatifu Fracinsko amefika mji wa Skopje nchini Macedonia ya Kaskazin, ikiwa ni hatua yake ya pili ya mwisho wa ziara yake ya 29 ya kitume baada ya Bulgaria. Baba Mtakatifu ameanza safari asubuhi saa 2.33 ,saa  mahalia ikiwa ni saa 7.33  nchini Italia, baada ya kumaliza sherehe za kuagana na Waziri Mkuu wa Bulgaria Bwana Borisov.

Baada ya safari karibu ya nusu saa kwa ndege, Baba Mtakatifu ametua uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Skopje mahali ambapo amekuta rais wa Jamhuri, Gjorge Ivanov,akimsumbiri  na watoto wakiwa wamevaa nguo za utamaduni wamempatia mkate, chumvi na maji ambapo Baba Mtakatifu ameshirikishana na wote waliokuwa karibu naye. Wakati akifika  katika uwanja wa  kimataifa wa Skopje uwakilishi wa waamini katoliki walikuwapo ambao wamemsalimia Baba Mtakatifu  Francisko kwa makofi kwa vigelela hadi anamfikia waziri Mkuu.

Hii ni hatua ya kwanza  ya siku nchini Macedonia ya Kaskazini ambapo Baba Mtakatifu amepokelewa na sherehe rasmi za kumkaribisha saa 3.15 katika uwanja wa Ikulu na kutembelea kwa faragaha  Rais wa nchi Bwana, Gjorge Ivanov,saa 3.30, mkutano na waziri Mkuu Zoran Zaev. Na saa 3.45 viongozi wa nchi wa kidiplomasia katika ukumbi mkuu wa rais.  Saa 4.20 Baba Mtakatifu atatembelea Kumbu kumbu ya mama Teresa wa Kalcuta wakiwepo viongozi wa dini na mkutano na maskini 100 wanaohudumiwa na Watawa wamisionari wa Upendo wa shirika la mama Taresa wa Kalcuta.

Baba Mtakatifu ataadhimisha misa Takatifu saa 5.30  katika Uwanja wa Macedonia na baada ya chakula cha mchana saa 7.30 na alioambata nao, itafuatia mkutano wa kiekumene  na kidini saa 10.00 jioni  na vijana wa  Kituo cha kichungaji, ambapo Baba Mtakatifu atahutubia kabla ya sala ya Mama Taresa isemayo: “Unahitaji mikono yangu ee Bwana”. Saa 11.00 atakutana na mapadre na familia zao na watawa katika Kanisa Kuu. Baaada ya sherehe za kuagwa katika uwanja wa kimataifa wa Skopje, Baba Mtakatifu anatarajia kuanza safari ya kurudi Roma saa 12.30 na matarajio ya kufika  saa 2.30 usiku mjini Roma.

07 May 2019, 09:45