Hekalu la kibudha huko Wat Phra Chetuphon, Tailandia Hekalu la kibudha huko Wat Phra Chetuphon, Tailandia 

Siku kuu ya Vesakh:Kukuza hadhi ya wanawake na wasichana duniani

Watu wote wanaalikwa kuhamasisha hadhi ya kila mtu hasa wananamke na watoto.Iwe Ubuddha au Ukristo unafundisha kuwa,wanawake na wanaume wana hadhi sawa na kushika nafasi muhimu ya kukuza mwanamke.Ndiyo wito katika ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini kwa waamini wa dini ya Kibuddha wanapo sherehekea Siku kuu ya Vesakh mwaka 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa niaba ya Baraza la Kipapa la mazungumzo ya kidini, ninapenda kuwasalimia kwa heshima na sala kwa ajili ya Siku kuu ya Vesakh. Sikukuu hiyo ilete furaha na amani kwa wote, familia zenu na katika jumuiya. Ndiyo mwanzo wa ujumbe wa Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya kidini katika fursa ya Wabudha ya kuadhimisha  Siku Kuu ya Vesakh kwa mwaka 2019, Ujumbe ulioandikwa na Askofu Miguel Ángel Ayuso Guixot, M.C.C.J. Katibu Mkuu wa Baraza hilo. Katika ujumbe huo, anathibitisha kwamba unajikita kutazama Hati ya Udugu wa kibidamu kwa ajili ya Amani duniani na kuishi kwa pamoja, uliotiwa sahihi huko Abu Dhabi tarehe 4 Februari 2019 na Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Shehikh Ahmad Al-Tayyeb, Imam Mkuu wa  Al-Azhar. Ni ujumbe wenye maana sana ambao unawaalika watu wote wa kila eneo duniani kuhamasisha hadhi ya kila mwanamke na watoto, kadhalika ni mwendelezo wa mchakato wa pamoja ambao unapania kwa namna ya pekee kudumisha uhusiano wa kidini na kirafiki na waamini wa dini ya Kibudha.

Mafundisho ya Yesu na Buddha

Mafundisho ya Yesu na Budha yanahamasisha hadhi ya mwanamke. Iwe dini ya Kibuddha na Kikristo zina fundisha kuwa wanawake na wanaume wanayo hadhi sawa na wanajikita katika nafasi muhimu katika kuhamasisha wanawake. Wanawake wa kibuddha na wakristo wameweza kutoa mchango wenye maana katika tamaduni zetu za kidini na kijamii kwa ujumla wake. Pamoja na hayo hatuwezi kukataa kwa bahati mbaya kuwa  wanawake wamekuwa katika sehemu ya kubaguliwa na kutendewa vibaya. Mara nyingi ukisikiliza historia za kidini, mwanamke anawakilishwa kama mtu wa chini ya mwanamme.

Kutumia nguvu dhidi ya mwanamke na wasichana imekuwa tatizo la kidunia

Katika nyakati zetu, kutumia nguvu dhidi ya wanawake na wasichana ni tatizo la kidunia, ambalo linaikumba robo tatu ya dunia ya wanawake, na hii imezidi kuchangiwa katika hali zenye migogoro na kukuzwa katika kuhamisha watu kwa kulazimishwa. Wanawake na watoto kwa namna ya pekee pia ni waathirika hasa kwa mtazamo wa biashara ya binadamu na mitindo ya utumwa mamboleo, mifumo ya ukatili ambayo ni hasi na mara nyingi inaathiri afya yao. Ili kuweza kupingana na hali hizi hasi za ukosefu wa usawa, ni muhimu kutambua wanawake na wasichana ili wapate elimu, wawe na  malipo sawa ya mishahara, urithi na haki za mali, kujaza pengo katika uwakilishi katika nyanja za kisiasa, kwa serikali na katika kutoa maamuzi, kukabiliana na  suala la mahari ya mke na mengine. Katika kuhamasisha usawa wa hadhi na haki ya wanawake, lazima pia itufanye  kutafakari juu ya mazungumzo ya kidini na mahali ambapo wanatakiwa washiriki zaidi wanawake, kwa maana leo hii wanaume ndiyo wanachukua nafasi kubwa zaidi.

Ni dharura kulinda wanawake na kulinda haki zao msingi na uhuru

Katika ujumbe huo pia unalezea muhimu na dharura ya  kuweza kulinda wanawake na kuwatetea haki zao msingi na uhuru wao. Kama inavyoeleza Hati ya Udugu kwamba: ni muhimu na lazima kutambua hali za mwanamke katika elimu, kazi na mazoezi yake katika haki ya kisiasa. Na zaidi, lazima kufanya kazi kwa ajili ya kutoa uhuru dhidi ya shinikizo la kihistoria na kijamii inayokwenda kinyume na misingi ya imani binafsi na hadhi. Ni lazima hata kuwalinda dhidi ya unyanyaswaji kijinsia na kutendewa vibaya hasa katika biashara haramu ya binadamu na katika kutafuta faida kiuchumi kwa njia yao. Kwa sababu hii, ni lazima kufanya kila njia ya kuvunja tabia hizi na mazoea yasiyo ya kibinadamu na desturi za uovu ambazo hudharau hadhi ya wanawake na pia ili kufanya kazi ya kuweza kubadili sheria zinazozuia wanawake wasiweze kufurahia kikamilifu haki zao.

Wito kwa wale wenye mamlaka ya kuwajibika ili wakuze heshima na hadhi

Wajibu maalum katika ujumbe huo unathibitisha ni kwa wale ambao wana mamlaka na wana nafasi ya kuwajibika ili kuwatia moyo wafuasi wao waweze kusaidia kukuza hadhi na  heshima ya wanawake na wasichana na kulinda haki zao za msingi. Hivyo hivyo, ni lazima  kutoa onyo kwa ndugu kaka zetu na dada juu ya hatari zinazohusishwa na itikadi ya kijinsia, ambazo zinakataa tofauti na usawa kati ya wanaume na wanawake. Katika kukuza hadhi na heshima na usawa wa wanawake na wasichana, vilevile ni kutaka pia kuhamasisha na kulinda taasisi ya ndoa, mama na maisha ya familia. Na hatimaye wito wa mwisho katika ujumbe huo ni kuwahamasisha wabuddha kwa pamoja kuwa na jitihada za kukuza familia zote, katika jumuiya na taasisi kwa njia ya kupyaisha majukumu zaidi katika nafasi msingi ya wanawake katika ulimwengu wote na kufanya kazi yapamoja ili kupinga na  kukataa kila aina ya mtindo wa kibaguzi, usiofaa dhidi ya binadamu. Na katika roho hiyo ujumbe huo unahitimishwa kwa kuwatakiwa Siku Kuu njema ya Vesakh iliyojaa amani na furaha.

Mwezi wa Vesakh una maana gani?

Siku kuu ya Vesakh inajulikana pia kama Siku kuu ya mwanga, inayokumbusha nyakati tatu msingi wa maisha ya Buddha: kuzaliwa, kuangazwa na kifo. Kwa mujibu wa utamaduni wa dini ya Kibuddha, mwanzilishi wa dini hiyo, wanasema alizaliwa siku ya mwezi uliokuwa umejaa yaani katika mwezi wa Vesakh kunako mwaka 623 a.C. Aidha kwa mujibu wa utamaduni huo huo wanasema,katika  siku kama hiyo hiyo aliweza kuangaziwa akiwa na umri wa miaka 35, na katika siku hiyo hiyo kunako mwaka 543 a.C, akiwa na umri wa miaka 80 aliaga dunia.

Mwaka wa kifo chake Buddha kunako 543 a. C , vile vile wanasema ni mwaka ambao walianza kalenda yao ya Kibuddha. Mwezi wa Vesakh unakwenda sambamba  na kipindi cha nusu ya pili ya mwezi Aprili hadi kufikia nusu ya kwanza ya mwezi Mei. Siku kuu ya Vesakh, kwa mujibu wa utamaduni wa  Kihindi, inaadhimisha kipindi ambacho kwa miaka mia tano kabla ya Kristo, Mfalme wa Gautama Siddharta alifikia kiasi kikubwa cha kuangazwa na kuwa Buddha, yaani, aliyeamka Siddhartha kutoka katika maisha yake yote yaliyojitolea tafakari na kuenea kwa mafundisho yake ya amani, upendo na huruma, mara moja alipofikia ncha  ya  Nirvana (yaani Paradiso ya Kubuddha), na kwa maana hiyo wakati wa kuwa na huru mwenyewe kutoka kwenye mzunguko wa kufufuliwa, alijitazama nyuma yake na kuona ubinadamu katika mtego wa uchungu na mateso!

13 May 2019, 10:34