Papa amemteua Balozi wa Kitume chini Malawi!
Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican
Tarehe 8 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Kitume nchini Malawi, Askofu Mkuu Gianfranco GALLONE, Askofu Mkuu wa Matola na Balozi wa Kitume nchini Zambia. Askofu Mkuu Gianfranco Gallone, alitangazwa kuwa Balozi wa Kitume nchini Zambia kunako tarehe 2 Februari 2019 na kupewa makao makuu ya ya Mottola.
Aliwekwa wakafu tarehe 19 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro katika mikono ya Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Askofu Mkuu Galloni alizaliwa huko Ceglie Messapica kunako tarehe 20 Aprili 1963 na kupewa daraja Takatifu la upadre tarehe 3 Septemba 1988 na Askofu Armando Franco.
Majiundo yake ni Shahada ya Sheria za Kanisa; Taalimungu ya Liturujia, mafunzo ya historia ya Kanisa mahalia katika Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kanisa Roma. Tangu 2000 ameshughulika na Masuala ya kidiplomasaia, kwa maana hiyo kijikita katika makao ya ubalozi nchi mbalimbali kama vile Msumbiji, Israeli, Slovakia, India na Sweeden na baadaye katika shughuli kidiplomasia za kitengo cha mahusiano na ushirikiano wa nchi katika Skretarieti Vatican.