Tafuta

Vatican News
Tarehe 8 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua  Askofu Mkuu Gianfranco Gallone kuwa balozi wa kitume nchini Malawi ambapo pia ni balozi wa Zambia Tarehe 8 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu Mkuu Gianfranco Gallone kuwa balozi wa kitume nchini Malawi ambapo pia ni balozi wa Zambia 

Papa amemteua Balozi wa Kitume chini Malawi!

Tarehe 8 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Kitume nchini Malawi,Askofu Mkuu Gianfranco GALLONE,Askofu Mkuu wa Mattola na Balozi wa Kitume nchini Zambia.Askofu Mkuu Gianfranco Gallone,alitangazwa kuwa Balozi wa Kitume nchini Zambia kunako tarehe 2 Februari 2019.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 8 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Kitume nchini Malawi, Askofu Mkuu Gianfranco GALLONE, Askofu Mkuu wa Matola na Balozi wa Kitume nchini Zambia. Askofu Mkuu Gianfranco Gallone, alitangazwa kuwa Balozi wa Kitume nchini Zambia kunako tarehe 2 Februari 2019 na kupewa makao makuu ya ya Mottola.

Aliwekwa wakafu tarehe 19 Machi 2019 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro  katika  mikono ya  Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican. Askofu Mkuu Galloni alizaliwa huko Ceglie Messapica kunako tarehe 20 Aprili 1963 na kupewa daraja Takatifu la upadre tarehe 3 Septemba 1988 na Askofu Armando Franco.

Majiundo yake ni Shahada ya Sheria za Kanisa; Taalimungu ya Liturujia, mafunzo ya historia ya Kanisa mahalia katika Taasisi ya Kipapa ya Mafunzo ya Kanisa Roma.  Tangu 2000 ameshughulika na Masuala ya kidiplomasaia, kwa maana hiyo kijikita katika  makao ya ubalozi nchi mbalimbali kama vile Msumbiji, Israeli, Slovakia, India na Sweeden na baadaye katika shughuli kidiplomasia za kitengo cha mahusiano na ushirikiano wa  nchi  katika Skretarieti Vatican.

 

 

08 May 2019, 16:27