Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ameitisha mkutano wa viongozi wakuu wa Kanisa nchini Ukraine, utakaofanyika tarehe 6-7 Julai 2019 mjini Vatican. Baba Mtakatifu Francisko ameitisha mkutano wa viongozi wakuu wa Kanisa nchini Ukraine, utakaofanyika tarehe 6-7 Julai 2019 mjini Vatican. 

Papa Francisko kukutana na viongozi wa Kanisa Ukraine, Julai!

Papa Francisko ameamua kumuita Askofu mkuu, wajumbe wa kudumu wa Sinodi pamoja na Maaskofu wakuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki nchini Ukraine, ili kukutana kwa pamoja mjini Roma kuanzia tarehe 5-6 Julai 2019. Viongozi wandamizi kutoka Sekretarieti kuu ya Vatican wanaohusika na eneo hili watashiriki pia. Mkutano huu ni alama ya uwepo wa karibu wa Papa kwa Ukraine.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Familia ya Mungu nchini Ukraine haina budi kusimama kidete katika fadhila ya imani, matumaini na mapendo, licha ya changamoto nyingi zinazoikabili kwa wakati huu. Kuna haja ya kuendelea kujikita katika mchakato wa haki, amani na maridhiano, kwa kudumisha umoja, udugu na mshikamano wa kitaifa. Bado Ukraine inakabiliana na hali tete sana kutokana na hali ya machafuko ya kisiasa.

Baba Mtakatifu Francisko ameamua kumuita Askofu mkuu, wajumbe wa kudumu wa Sinodi pamoja na Maaskofu wakuu wa Kanisa Katoliki la Kigiriki nchini Ukraine, ili kukutana kwa pamoja mjini Roma kuanzia tarehe 5-6 Julai 2019. Viongozi wandamizi kutoka Sekretarieti kuu ya Vatican wanaohusika na eneo hili watashiriki pia. Mkutano huu ni alama ya uwepo wa karibu wa Baba Mtakatifu Francisko kwa familia ya Mungu ndani na nje ya Ukraine. Mkutano huu utakuwa ni fursa makini ya kuweza kufanya upembuzi yakinifu kuhusu hali ya maisha na mahitaji halisi ya Ukraine kwa wakati huu katika mchakato wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu. Kanisa linataka kuchangia kwa hali na mali, ili kuwasaidia wale wote wanaoteseka kutokana na vita, kwa kushirikiana na Makanisa pamoja na Jumuiya mbali mbali za Kikristo, kielelezo cha uekumene wa huduma kwa maskini!

Papa: Ukraine
06 May 2019, 09:55