Tafuta

Vatican News
Tarehe 25 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Genova katika uwanja wa Mtakatifu Marta mjini Vatican Tarehe 25 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Genova katika uwanja wa Mtakatifu Marta mjini Vatican 

Baba Mtakatifu amekutana na watoto wa kipaimara kutoka Jimbo Kuu Katoliki Genova!

Tarehe 25 Mei 2019 mbele ya Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko amesalimiana na kundi kubwa la watoto wa kipaimara ambao wamesindikizwa na Kardinali Angelo Bagnasco Askofu Mkuu wa Jimbo la Genova.Baba Mtakatifu amewaalika vijana hao watazame mama Maria ambaye anawaelekeza kwake Yesu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Mei 2019 mbele ya uwanja wa Mtakatifu Marta mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanakipaimara kutoka Jimbo la  Genova Italia wakisindikizwa na Kardinali Angelo Bagnasco Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. Vijana wameonesha kwa dhati furaha na shukrani kwa Baba Mtakatifu Francisko ambapo pia naye amemshukuru Kardinali kuwaleta vijana hao na hasa fursa ya kuwaona vijana ambao wanataka kwenda katika barabara ya Yesu.

Mama Maria ni mama ambaye anawapeleka kwa Yesu

Katika mazungumzo na wanakipaimara hao, Baba Mtakatifu Francisko amewashauri waendelee kumjua Mama Maria kama mtu mwenye uwezo zaidi wa huruma na mwema na kukaa naye karibu ili aweze kuwapeleka wote kwa Yesu. Amewambaa kwamba wao  wanakwenda kusalimia Mama Maria katika Groto ya Lourdes iliyopo mjini Vatican, pale kuna Mama Maria na hivyo wasali kwa sababu ni mama . Aidha amesema: "wote tuna maisha magumu daima, lakini unapokuwa na tatizo ni vema kumkimbilia Mama daima”.  Vile vile, amesema hali hiyo ni sawa na ile ya mtoto anapokuwa na matatizo anamkimbilia mama yake na mama anakumbatia". Na kwa njia hiyo, hata Mama Maria anafanya hivyo kwa ajili ya kutaka kuwapeleka kwa Yesu na ndiyo ishara ya haraka ambayo Maria anafanya kwa ajili ya watoto wake wote ili awapeleke kwa Yesu.Baba Mtakatifu amebainisha.

Wafikirie wale wasio wapenda

Baba Mtakatifu Francisko amesali sala ya Salam Maria na vijana hao na baadaye kabla ya kuwabariki amwapatia majukumu muhimu kwamba: kila mmoja afikirie wapendwa wake zaidi, ambao wako ndani ya mioyo yao karibu. "Fikirieni vizuri… na baadaye labda kuna wale ambao hawawapendi, au mwingine ambaye ninyi hampendi: fikirieni hata watu hao, kwa maana ninawabariki ninyi nyote, wapendwa wenu na wale ambao hamuelewani au mmegombana nao" amesema Baba Mtakatifu na kuhitimisha kwa kuwabariki na baraka Takatifu.

25 May 2019, 14:19