Tafuta

Papa Francisko amemteua Padre Toussaint Iluku Bolumbu, M.S.C. kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bokungu-Ikela, DRC. Papa Francisko amemteua Padre Toussaint Iluku Bolumbu, M.S.C. kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bokungu-Ikela, DRC. 

P. Toussaint I. Bolumbu ateuliwa kuwa Askofu, Bokungu-Ikela

Padre Toussaint Iluku Bolumbu ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Bokungu-Ikela, nchini DRC. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteuleToussaint Iluku Bolumbu alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kanda ya Afrika, kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa. Alizaliwa mwaka 1964; Nadhiri: 1994 na Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 23 Julai 1995.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Toussaint Iluku Bolumbu, M.S.C., kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Bokungu-Ikela, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteuleToussaint Iluku Bolumbu alikuwa ni Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, Kanda ya Afrika, kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa.

Askofu mteule Toussaint Iluku Bolumbu alizaliwa kunako tarehe 18 Novemba 1964 na baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa, akaweka nadhiri za daima mwezi Agosti 1994 na tarehe 23 Julai 1995 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Katika maisha na utume wake kama Padre, kuanzia mwaka 1995-1997 alijiendeleza kwa masomo ya juu huko Kinshasa; akawa mlezi wa Wanovisi na Paroko. Kati ya Mwaka 1999 hadi mwaka 2000 akateuliwa kuwa Gombera msaidizi.

Kati ya Mwaka 2000 hadi mwaka 2002 alipelekwa kujiendeleza zaidi kwenye Chuo kikuu cha Kipapa la Gregorian, kilichoko mjini Roma na kujipatia Shahada ya uzamivu kwenye taalimungu ya maisha ya kiroho. Kati ya Mwaka 2002-2003 alijiendeleza zaidi kwenye kozi ya malezi ya vijana, Chuo Kikuu cha Kipapa la Gregorian, kilichoko mjini Roma. Kati ya Mwaka 2003 hadi mwaka 2009 alichaguliwa kuwa Makamu wa Rais, Shirikisho la Wakuu wa Mashirika, (ASUMA) Jimbo kuu la Mbandaka-Bikoro. Katika kipindi cha Mwaka 2005, aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Katibu mkuu wakati wa maadhimisho ya Mkutano mkuu wa Shirika uliofanyika mjini Roma.

Papa: DRC
14 May 2019, 15:36