Tafuta

Vatican News
Mei Mosi 2019:Askofu Mkuu Protase Rugambwa akiwa na mashemasi wapya, Atta Okyere, Frank John Gilagiza na Dogratias Method  Nyamwihula mara baada ya kuwekwa wakfu Mei Mosi 2019:Askofu Mkuu Protase Rugambwa akiwa na mashemasi wapya, Atta Okyere, Frank John Gilagiza na Dogratias Method Nyamwihula mara baada ya kuwekwa wakfu 

Askofu Mkuu Rugambwa:Tendo la kutiwa wakfu limesimika mizizi katika ubatizo!

Katika fursa ya Sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi vijana watatu Frank John Gilagiza wa Jimbo Katoliki Kigoma,Dogratias Method Nyamwihula,Jimbo Kuu Katoliki Mwanza,Tanzania na Atta Okyere Samuel Jimbo Kuu Katoliki la Kumasi Ghana,wamepewa daraja takatifu la ushemasi katika mikono ya Askofu Mkuu Protace Rugambwa.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Mei Mosi ikiwa ni siku Kuu ya Mtakatifu Yosefu Mfanyakazi sambamba na siku ya wafanyazi duniani, Mama Kanisa amewapokea vijana wake waseminari katika daraja la ushemasi. Hawa ni vijana watatu Frank John Gilagiza wa Jimbo Katoliki Kigoma Tanzania, Dogratias  Method  Nyamwihula  wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza Tanzania, na Atta Okyere Samuel wa Jimbo Kuu Katoliki la Kumasi nchini Ghana. Mafrateli hawa wamepewa daraja la Ushemasi na Askofu Mkuu Protase Rugambwa Katibu wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu katika Basilika ya Mtakatifu Apolinari mjini Roma. Nyimbo za kilatini, kiitaliano, Kiswahili na kingereza zimeweza kutumbuizwa na kutuliza mioyo ya waamini ambao walikuwa wameundwa na mapadre wengi ambao wanasoma katika vyuo vikukuu mbalimbali hapa Roma, watawa na walei wengi walioshiriki kikamilifu kwa kuwaombea vijana hawa katika Misa Takatifu ya pekee. 

Masomo yaliyosomwa ni kutoka katika Kitabu cha Matendo ya mitume, (Mdo 6, 1-7b) kwa  lugha ya kiswahili; Zaburi ya 83/84 (Kilatini), somo la pili kutoka katika  Barua ya pili ya wakorinto (2Kor 4,1-2.5-7 kwa kingereza na Injili ya Yohane, (15,9-17) kwa lugha ya Kiitaliano. Baada ya mahubiri limefuata tendo rasmi la kutiwa wakfu likifuatiwa na Sala ya Litania ya Watakatifu wote  ambayo iliimbwa wakati  mafrateli wamelala kifudifudi. Aidha baada ya sala rasmi na Askofu Mkuu ulifuatiwa  tendo la kuvalishwa nguo mashemasi ambapo pia kuwekwa mikono kichwani. Hata hivyo ni tangu zama za Mitume wa Yesu mamlaka inashirikishwa kwa tendo la kumwekea mtu mikono kichwani, kufuatana na mfano wa Musa kwa Yoshua katika Agano la Kale. Tendo la kuwekwa mikono linafuatana na sala maalum ambayo, katika kumuomba Roho Mtakatifu amshukie mhusika, inaweka wazi daraja gani linatolewa!

Mahubiri ya Baba Askofu yameanza na kufafanua hatua ya tendo la daraja takatifu la ushemasi 

Kama kawaida ya utaratibu wa kila daraja takatifu, mara baada ya mahojiano na mafrateli, Askofu Mkuu Protace Rugambwa alianza mahubiri yake akifafanua kila hatua yao na tendo hili la daraja takatifu kwa waamini hasa walengwa zaidi wanaotiwa wakfu kwamba “kwa njia ya Sakramenti ya kutiwa wakfu, mashemasi hao watawekwa katika mpangilio mtakatifu wa huduma ya  Mtumishi mkuu Yesu Kristo. Na miongoni mwa maswali atakayo wauliza yanajikita  katika “shughuli za wateule", ikiwa la  kwanza ni lenye tabia ya mwisho kwa ufupi. Maswali hayo yanasema: "Unataka kuwa na wakfu katika huduma ya Kanisa kwa kwa njia ya kuwekwa mikono yake na zawadi ya Roho Mtakatifu?

Je ni nani mwenye wakfu? Ina maana gani kuwa na wakfu? Askofu Mkuu akiuliza maswali hayo na kujibu kwamba: Kuna maneno mawili yanayounganishwa katika neno “aliye na wakfu”, yaani “na” na “mbarikiwa”. Katika sala yake kwa Baba, kabla ya  kutoka ulimwenguni huu kwenda kwa Baba, Yesu alisema: “Na kwa ajili yao najiweka wakfu mwenyewe, ili na hao wawekwe wakfu katika kweli”. Kwa maana hiyo tendo la wakfu wetu umesimika mizizi katika Ubatizo. Yesu ni mwenye wakfu wa Baba na na kwake Yeye anatupatia wakfu.  Kwa upande wa wateule, Askofu Mkuu Rugambwa amesema kuwa, kuwekwa wakfu huko kumesimikwa mzizi katika ubatizo wao na kuwa na thamani maalum leo hii na ambayo imechukuliwa katika safari yao waliyoanza nayo kwa kutoa  jibu la wito binafsi kwa Bwana wa kumtumikia katika huduma ijayo ya ukuhani.

Wameacha kila kitu na kujitoa maisha yao ili kufuata utakatifu na huduma kwa watu

Aidha Ashofu Mkuu Rugambwa amesema: ni kwa jinsi gani wao wamekuwa na jitihada katika mitindo tofauti ya kuweza kuitikia wito wa Kristo na kumfuata, kuacha namna  yao, kila kitu na kijitoa maisha yao ili kufuata utakatifu na huduma kwa watu wake. Ni Yesu aliyewaita na ni Yeye aliyewachagua na amewafanya kwa jinsi  walivyo. Yeye ndiye leo hii anawafanya kuwa mashemasi wake. Na huduma ambayo wataipokea ni zawadi ya huruma ya Mungu. “Hamkunichagua mimi, bali nimewachagua”: hii ndiyo kuwa mtakatifu na Bwana, yaani aliyetolewa milele kwa Mungu na ili kuanzia kwa Mungu na njia ya Yeye wanaweza kuwatumikia watu. Kutokana na hiyo Askofu Mkuu Rugambwa anabainisha kuwa hii, inawataka wawe na uhusiano wa ndani na muungano wa Moyo: “Kaeni ndani ya upendo wangu”. Kubaki katika upendo wa Kristo ni wa lazima ili kwenda zaidi yetu binafsi, kujikana kile ambacho ni chetu, ili kuhepukana na  ubatili wa kujitosheleza.

Hali kadhalika ameongeza  kusema: “Tunahitaji kwamba sisi /mimi nisijivunie maisha yangu, kwa ajili yangu mwenyewe, bali yawe ni kwa ajili ya mwingine, ya Kristo, kama alivyo  yakabidhi moja kwa moja kwa Baba yake na  Baba yetu. Na katika mpango wa Mungu aliyewaita, wameitika  ndiyo. “Tazama mimi hapa” yao, inajikita kwa  “tazama mimi hapa” ya Mwana wa Mungu, mwenye wakfu na Baba, Mtumishi mtiifu wa Baba amesisistiza Aaskofu Mkuu. Shemasi amewakwa wakfu kwa ajili ya huduma ya upendo. Katika Injili ni Bwana mwenyewe anaye zungumza juu ya upendo:“hii ndiyo amri yangu:pendaneni ninyi kwa ninyi”. Upendo huo ambao Bwana anatuomba sisi sote, unainamia ( Katika matendo ya Mitume) kwa mashemasi, kwa njia ya kutoa huduma mezani. Je inasaidia nini katika altare ya Bwana, kwenye Kanisa Takatifu, iwapo hujuhi  kutoa huduma ya Bwana duniani? Sisi tumetiwa wakfu kwa hakika katika maisha yetu kwa ajili ya dunia, mahali ambamo tunaishi. Mtakatifu Yosefu mfanyakazi, ambaye leo hii anaadhimishwa  siku kuu yake, anatufundisha kwamba, kazi inayotimizwa kwa haki, yaani kwa uaminifu ni takatifu na ndiyo njia ya kutakatifuza.

Upendo una maana gani? Ni katika huduma!

Bwana wetu na Mwalimu Yesu anatueleza nini maana ya upendo. Yeye anaelezea utume wake  kwa ufupi katika njia ya huduma. Wakati wa Karamu yake ya mwisho na Mitume wake, akihitimisha utume wake, yeye aliinuka na kusimama mezani, ishara ya mamlaka yake, alivua nguo zake, ishara  ya unyenyekevu wa mamlaka na kuwaosha miguu Mitume. Kwa kufanya hivyo anatuonesha kwamba, Mwana wa Mtu alikuja kutumikia; anatufundisha uzuri wa huduma. “Yeyote anayetaka kuwa mkubwa kati yenu atakuwa mtumishi wenu na yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati yenu atakuwa mtumwa wa wote.” Kigezo cha ukubwa na  cheo cha ukuu, kwa mujibu wa  Mungu siyo mamlaka, bali ni katika  huduma na  Msalaba. Ushemasi ni sheria msingi ya mfuasi na jumuiya ya Kikristo. Licha ya  utume kuwa ni  kwa ajili ya  wabatizwa wote, lakini na kwa ajili wapendwa wateule, Askofu Mkuu Rugambwa anasisitiza, huduma yao ya ushemashi inachukua mwelekeo maalum. Katika Mtaguso wa  Pili wa  Vatican, unaelezea kuwa neema ya sakramenti iliyotolewa kupitia kwa tendo la kuwekewa mikono unawawezesha kutoa huduma yao ya neno, katika altare na upendo katika fursa maalum (tazama Ad Gentes, 16). Huduma ya shemasi ni huduma ya Kanisa la kisakramenti. Huduma yao siyo moja tu ya huduma nyingi, bali, lazima iwe nguvu ya injini na ya kweli kwa ajili ya ushemasi wa Kanisa. Kwa kuwekwa wakfu, wao watafanana na Kristo mtumishi katika nafsi yake ya huduma. Kwa njia hiyo wao wameitwa na wanawekwa wakfu ili kuwa ishara hai ya huduma na katika Kanisa lake.

Ishara mbalimbali zinazokuwapo katika tendo la kuwekwa wakfu

Askofu Mkuu Mkuu Rugambwa akiendelea na mahubiri yake, ameelezea pia ishara mbalimbali zinazo kuwapo wakati wa tendo la kuwekwa wakfu, kwa maana hiyo anadema: kupokea Kitabu cha Injili ya Kristo kwa maneno: “Pokea Injili ya Kristo ambayo umekuwa mtangazaji: amini daima unacho kitangaza, fundisha kile ulichoelewa katika imani na uishi unachofundisha”. Ushamasi wa upendo ambao haupaswi kukosekana katika Kanisa, lazima ufungamane daima na tangazo la Neno na katika mafundisho ya mafumbo matakatifu. Hii ina maana kwamba huduma ya matendo katika upendo, hawali ya yote ni huduma ya kiroho.  Askofu anawahimiza wateule wamwilishwe na Neno la Mungu ili kuweza kufanana  nalo katika maisha yao. Yesu anasali kwa Baba yake kuwa ili sisi sote “tuwekwe wakfu katika ukweli” kwa sababu Neno lake ni ukweli. Ukweli huu ni fumbo la imani ambalo sisi tumewekwa wakfu ( Yh 17,17-19), na ndiyo katika ukweli sisi sote tunaitwa kukua na kwa msaada wa neema ya Mungu ambayo kila siku kwa uaminifu wa Neno lake ndani ya Muungano hai wa Kanisa.

Licha ya hayo yote hayo hata hivyo Askofu Mkuu Rugambwa anabainisha:ni kwa jinsi gani safari  hiyo ya wakfu ilivyo ngumu! Inahitaji uongofu wa kuendelea, kufa kwa kujisadaka. Kutiwa wakfu ni sadaka ya kudumu, ya kuendelea kufa nafsi na ambayo ni hali ya kushiriki kikamilifu kwa Mungu; ni mabadiliko ya akili na moyo ambayo huleta uhuru wa kweli na upana wa maono mapya. Katika utambuzi kwamba ni Neno la Mungu pekee linaweza kubadilisha kwa kina moyo wa mwanadamu, wateule hao wawe wasikilizaji wa kweli, watangazaji na mashuhuda wa Neno hili na ili waamini waweze kuingia ndani yake na kuwa na uhusiano unao endelea kukua daima kwa kina. Hatimaye katika hitimisho la mahubiri yake, Askofu Mkuu Rugambwa anasema: “Tumwombe Maria Mtumishi wa Bwana, mnyenyekevu na mtiifu, ambaye alifananana na mapenzi ya Mungu, kwa kumzaa Kristo na kumtoa katika dunia, ili awasindikize kila siku katika maisha yenu kwenye huduma yenu. Shukrani za upendo wa Mama huyu mpole, wa nguvu mnaweza kuwa na furaha ya uaminifu wa kujikabidhi na kama mashemasi leo hii na kesho makuhani, mnapewa kile ambacho kinafanana na Kristo mtumishi, ambaye alitambua kutii mapenzi ya Baba na kupenda binadamu hadi mwisho”.

Askofu Mkuu Rugambwa
02 May 2019, 11:49