Tafuta

Vatican News
Katika sikukuu ya somo wa Papa, tarehe 23 Aprili ametoa zawadi kwa vijana wa Jimbo Kuu la Milano Rozari.Hizi zilitengenezwa Bethlehemu katika fursa ya Siku ya Vijana Panama Katika sikukuu ya somo wa Papa, tarehe 23 Aprili ametoa zawadi kwa vijana wa Jimbo Kuu la Milano Rozari.Hizi zilitengenezwa Bethlehemu katika fursa ya Siku ya Vijana Panama  

Siku ya Somo wa Papa:Zawadi ya rozari kwa vijana wa Jimbo Kuu Milano!

Katika fursa ya kumbukumbu ya Mtakatifu George somo wa Baba Mtakatifu Francisko,tarehe 23 Aprili ametoa zawadi ya rozari elfu sita kwa vijana wa Milano ambao wako hija mjini Roma wakiwa na Askofu wao Mkuu.Rozari hizi zilitengenezwa huko Bethlehemu katika fursa ya Siku ya Vijana Panama.Papa anawahimiza wasali rozari!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kwa mujibu wa msemaji mkuu wa mpito wa vyombo vya habari Vatican Dr. Alessandro Gisotti amesema kuwa katika Siku ya kumbukumbu ya Mtakatifu George, Somo wa Baba Mtakatifu Francisko kupitia mfuko wa  Sadaka ya Kitume, ametoa Rozari elfu 6 na ambazo pia zilikuwa zimetengenezwa katika fursa ya Siku ya Vijana Diniani huko Panama, kwa vijana wa Jimbo Kuu Katoliki la Milano, ambao tarehe 23 Aprili 2019 wameshiriki Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican, kwa kuongozwa na Askofu Mkuu Mario Delpini wa jimbo Kuu Katoliki Milano Italia.

Vijana waoneshe matunda mema na kwa mfano wa watakatifu Ambrosi na Karoli

Katika Ishara hiyo, Baba Mtakatifu anawaomba vijana kwa namna ya pekee kumkumbuka katika sala, na  kumkabidhi kwa namna ya Pekee kwa Bikira Maria, siku chache kabla ya kuanza mwezi wa Mei ambao ni wa Bikira Maria. Na tarehe 24 Aprili 2019, Vijana wa Jimbo Kuu Katoliki Milano wameshiriki Katekesi ya Baba Mtakatifu, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, ambapo Baba Mtakatifu amewatia moyo ili wakue katika imani na upendo kwa kujikita zaidi kuonesha matunda mema. Injili iwe ndiyo Kanuni ya maisha yao na kama ilivyokuwa kwa watakatifu wao Ambrosi na Karoli, ambao kwa upendo wao mkuu, anasema walibadilisha dunia!

23 April 2019, 14:44