Tafuta

Vatican News
Papa Francisko katika  salam za rambi rambi kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran anaeleza masikitiko yake na kuwaombea Papa Francisko katika salam za rambi rambi kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran anaeleza masikitiko yake na kuwaombea   (AFP or licensors)

Papa ametuma msaada kwa waathirika wa mafuriko nchini Iran

Papa ametuma salam za rambi rambi zilizotiwa sahini na Katibu wa Vatican.Anawaombea waathirika na majeruhi wote nchini Iran na kwa niaba ya Baba Mtakatifu,Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu limetuma msaada kwa watu walio athirika na mafuriko nchini Iran.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika  salam za rambi rambi zilizotumwa na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, anaelezea masikitiko na uchungu wake kwa ajili ya waathirika wa mafuriko nchini Iran na kusali sana kwa ajili ya wote ambao wanafanya kila jitihada ya dharura, ili kusaidia, na wakati huo huo anawakabidhi katika huruma ya Mungu mpaji  watu wote wa Iran.

Mchango wa Euro 100,000

Na zaidi Baba Mtakatifu Francisko kwa kupitia Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, ametuma mchango wa Euro 100,000 kwa ajili ya msaada wa watu hao. Jumla ya kiasi ya kiasi hicho ni kutaka kuonesha hisia za ukaribu kiroho mbele ya watu wote waliokumbwa na tukio hili la asili. Fedha hizo zitawafikia kupitia ushirikiano na Ubalozi wa vatican ili fedha ziweze saidia sehemu zilizo athiriwa na majanga na kuwasaidia watu wa maeneo mbalimbali.

Hali halisi ya mafuriko

Kwa wiki mbili za mwisho, mafuriko ya nguvu yamekumba kanda za Kaskazini Mashariki na magharibi mwa nchini Iran na bado kuna hatari ya kuendelea katika siku zijazo. Watu wa wilaya za Golestan, Lorestan na  Kuzestan ndizo zimekumbwa sana na ile ya Kermanshah ambayo ilikuwa tayari imekwisha jaribiwa wakati wa tetemeko la ardhi mwaka jana. Zaidi wa tu milioni 10 wamepata hasara na kupoteza nyumba na mali zao, wakati milioni 2 wanahitaji msaada wa haraka kufutia mafuriko hayoe.

Hadi sasa uthibitisho wa wathirika ni 77 na majeruhi karibia 1,070. Zaidi ya watu 200000 wameokolewa katika vijiji na Waziri wa mambo ya ndani ametangaza dharura katika mji wa Ahwaz. Kuna uharibifu mkubwa wa majengo na kilimo. Hata hivyo nchi nyingi zinaendelea kujibu wito wa msaada kwa ushirika wa Chama cha msalaba mwekundi Iran na Ofisi ya Taifa ya Tehran.  Hata Caritas nchini Iran imeweza kutembelea maendeo yaliyo kumbwa  na mashirika mengine mengi yanaendelea kupelekea msaada kwa watu.

13 April 2019, 12:31