Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko alipokutana  na Rais Salva Kiir Mwezi Machi 2019 mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na Rais Salva Kiir Mwezi Machi 2019 mjini Vatican 

Mafungo ya kiroho kwa viongozi wa Sudan Kusini mjini Vatican

Kuanzia tarehe 10-11 Aprili 2019 katika nyumba ya Mtakatifu Marta (Domus Sanctae Marthae),yanafanyika mafungo ya kiroho yaliyo pendekezwa na Askofu Mkuu wa Canterbury,kwa ushiriki wa viongozi wa ngazi za juu wa umma na Kanisa wa Sudan Kusini.Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kutoa hotuba yake siku ya Alhamisi mchana.

Baba Mtakatifu Francisko amekubali pendekezo lililowakilishwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby kuandaa mafungo ya kiroho mjini Vatican katika nyumba ya Mtakatifu Marta, kuanzia tarehe 10-11 Aprili 2019, kwa ushiriki wa viongozi wa ngazi za juu wa umma na kanisa wa Sudan Kusini. Ni katika uthibitisho wa Dk. Alessandro Gisotti, Msemaji wa Vattican wa vyombo vya habari  ambaye wiki iliyopita alikuwa amegusia uwezekano wa tukio hilo mjini Vatican.

Viongozi washiriki wa umma na wa Kanisa

Kwa upande wa viongozi wa ngazi za juu wa umma Bwana Gisotti anasema, watakuwa viongozi wa Jamhuri  ya Sudan Kusini kwani: chini ya Mkataba wa suluhisho la Mgogoro nchini Sudan Kusini na watakao wajibika kuchukua majukumu ya kitaifa kunako tarehe 12 Mei 2019 ni:  Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini, na makamu rais watano walio chaguliwa: Riek Machar Teny Dhurgon, James Wani Igga, Taban Deng Gai na Rebecca Nyandeng De Mabior. Kwa upande viongozi wakuu wa Kanisa nchini humo, watakuwapo wajumbe 8 wa Baraza la Makanisa Sudan Kusini. Mhubiri wa mafungo ya kiroho atakuwa Askofu Mkuu John Baptist Odama,wa Jimbo Kuu Katoliki la Gulu nchini Uganda na  padre Agbonkhianmeghe Orobator, rais wa Baraza la mikutano mikuu ya Afrika na Madagascar.

Sala,tafakari na mapatano

Tukio hili likiwa la kiekumene na kidiplomatiki, limeandaliwa kwa makubaliano ya pamoja, kati ya Sekratarieti ya Vatican na Ofisi ya Askofu Mkuu wa Canterbury, Uingereza, kwa lengo la kuweza kutoa fursa ya kwa upande wa Kanisa tafakari na sala, vile vile kwa ajili ya kukutana na upatanisho katika roho ya heshima na imani, kwa wale ambao kwa muda huu wana utume na uwajibikaji ili kuweza  kufanya kazi kwa ajili ya wakati endelevu  wa amani na matarajio mema ya watu wa Sudan kusini.

Hotuba ya Baba Mtakatifu

Hata hivyo,katika hitimisho la mafungo ya kiroho kwa viongozi hawa,ambayo inahitimishwa siku ya Alhamisi 11 Aprili mchina, inatarajiwa majira ya saa 11 Jioni Baba Mtakatifu kuhutubia. Na baada ye washiriki wa mafungo hayo watakabidhiwa Biblia itakayosahiniwa na Baba Mtakatifu Francisko, Askofu Mkuu Justin Welby, wa  Canterbury, na mchungaji John Chalmers,  ambaye alikuwa ni msimamisi wa Kanisa la Presbiterian huko Scotlan na kwa ujumebe usema:tafuteni kinacho unganisha. Shinda kinacho gawanya. Na mwisho viongozi wa Sudan Kusini ambao watachukua majukumu ya pamoja kwa ajili ya amani katika nchi yao, watapewa baraka ya Mungu.

09 April 2019, 16:00