Tafuta

Vatican News
Timu ya wadau wa Vatican news katika lugha ya kimakedonia.Kutoka kushoto ni Padre Goce Kostov, Jadranka Cadinovska, Dance Icheva na Goran Gogov Skopje,Makedonia kaskazini Timu ya wadau wa Vatican news katika lugha ya kimakedonia.Kutoka kushoto ni Padre Goce Kostov, Jadranka Cadinovska, Dance Icheva na Goran Gogov Skopje,Makedonia kaskazini 

Kuongezeka lugha ya kimakedonia,Vatican News inakuwa na lugha 34

Kabla ya mwezi mmoja wa ziara ya Baba Mtakatifu Francisko ya kwenda katika Jamhuri ya nchi ya Makedonia Kaskazini,inayotarajiwa kufanyika tarehe 7 Mei 2019, katika mtandao wa Vaticannews.va, umeongeza ukurasa mpya na kufanya lugha ziwe 34 zilizo ganyika katika alfabeti 12 zilizokuwapo tayari.

Katikati ya kigiriki, Kiburgaria, Kiserbia, Kikosovo na Kialbania,nchi ya Makedonia Kaskazini na yenye kuwa na wakatoliki 20,000 (kati yao 15,000 wa liturujia ya kibizantino), tangu sasa ipo katika mtandao wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kuhusu shughuli za Baba Mtakatifu Francisko, maisha ya Kanisa la ulimwengu, lakini hata juu ya maisha ya Kanisa lake mahalia. Yote hayo yamewezekana kutokana na ushiriki na  mkakati ulioundwa na Kanisa la Makedonia, na kwa hiyo mtandao utaweza kuwapelekea neno la Papa katika jumuiya ndogo ya  watu wa Mungu. Kwa mujibu wa Askofu Skopje Kiro Stojanov anasema, ukurasa  huu, juu ya Vaticanew ni kama tunda la kwanza ambalo ni tayari kabla ya ziara ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko.

Uwepo wa upyaisho na unaondelea

Naye Mkurugenzi wa uhariri Vatican, Bwana Andrea Tornielli akizungumza kuhusu ukurasa mpya wa lugha ya Makedonia amesema:“Lugha ya kimakedonia ilikuwapo tangu awali katika mtandao wa Vatican, kabla ya kuhamia Vatican News. Lakini kwa sasa tunataka kupendekeza upyaisho na zaidi kuwa na  uhai". “ Shukrani kwa uwezekano wake Askofu Stojanov na kikundi cha kusaidia, ambao wamewezesha kukamilisha shughuli hii muhimu kwa ajili ya jumuiya ndogo kwa mtazamo wa idadi yao, lakini walio hai kwa  maana kubwa katika nchi hiyo”, amethibtisha.  Wakatoliki nchini Makedonia kwa hakika wanawakilisha karibia asilimia moja ya jumla ya watu wote.

Umakini wa Vatican News kwa jumuiya ndogo

Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko, na ambaye alisema mwenyewe kabla ya kuchaguliwa kwake wakati wa Baraza la makardinali wapiga kura kwamba: “Kanisa linaitwa kutoka ndani mwake na kulekea pembeni, siyo katika mtazamo wa kijiografia, lakini hata katika maisha ya mwanadamu”. Na katika uaminifu wa utume wa Radio Vatican ambayo karibu ya  miaka 90 imefungualia microphone (kikuza sauti) zake kwa waamini wa dunia nzima,Vatican News sasa inafungua ukurasa wa mtandao wake ili kueneza Habari Njema kwa watu  wote kila kona ya dunia.

09 April 2019, 10:30