Ijumaa 12 April Baba Mtakatifu alifanua ziara yake katika kituo cha wagonjwa wa alzeima Roma Ijumaa 12 April Baba Mtakatifu alifanua ziara yake katika kituo cha wagonjwa wa alzeima Roma  

Ijumaa ya matendo ya huruma:Papa ametembelea wagonjwa wa Alzeima

Siku ya Ijumaa tarehe 12 Aprili 2019 jioni kama kawaida ya kufanya matendo ya huruma,Baba Mtakatifu Francisko alitembelea Kijiji cha Emanuele,kilometa chache kutoka mjini Vatican katika mtaa wa Bufalotta Roma,unaojikita katika shughuli ya kuwasaidia watu wenye dalili za ugonjwa wa Alzeima.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni Ijumaa ambayo inajikita katika matendo ya huruma ambapo Baba Mtakatifu Francisko, jioni ya tarehe 12 Aprili 2019 amewza kufanya ziara ya ghafla katika kijiji cha Emanuele. Ni katika Kijiji hiki ambacho watu siku hadi siku wanazidi kupoteza kidogo kidogo kumbu kumbu na maisha. Ni katika siku hii maalum ambayo inafanywa njia ya msalaba wa ugonjwa na matumaini ya pasaka, mwanga wa nguvu ndiyo unawaongoza kwa furaha na mshangao wa wenyeji wa Kijiji cha Emanuele. Katika mtaa huu wanaishi watu wenye ugonjwa wa Alzeima ambo kila siku ugonjwa huo unazidi kudonoa akili na kumbu kumbu zao na katika mkutano na Baba Mtakatifu Francisko imekuwa ni mshangao mkubwa kwao, na kukumbatiwa na kuwasalimiwa naye.

Furaha na mashangao 

Baba Mtakatifu amefika na gari na kutelemka katika uwanja wa Kijiji hicho. Wenyeji wa jengo hilo walimkaribia Baba Mtakatifu na kumsalimia naye kuwapa maneno ya kuwafariji kwa furaha wote. Baba Mtakatifu akiwa na Rais msataafu ambaye ni Mwanzilishi wake Bwana  Emmanuele Emanuele,ambapo kwa sasa rais wa chama hicho ni Franco Parasassi, wameweza kutembelea maeneo yote ya jengo hili na wanaoishi ndani ya mtaa huo. Badhi ya wageni walikuwa wanapumzika katika vyumba  vyao, wameingia ndani na kuwasalimia. Na wengine waliokuwa katika shughuli zao za ubunifu, pia wamemwonesha Baba Mtakatifu Francisko kazi yao ya kila siku. Na mwisho wa ziara yake hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amewapa zawadi ya Baraka ikiwa imeandikwa wazo lake, kwa mkono wale na juu ipo picha inayoonesha kuzaliwa kwa Bwana. Naye Rais mtaafu na mwanzilishi wa Chama cha Roma cha Kijiji hicho Profesa Emmanuele Emanuele, amesisitiza kwamba, imekuwa siku ambayo haitasahaulika. Katika kijiji hicho kwa maana  kuna mateso mengi yanayo gawanyika katika sehemu, lakini  kila mmoja ni sehemu ya jumuiya hiyo kama familia moja.

Mtaa na radha ya familia

Katika kijiji la Emanuele ni mtaa ambao unaishi karibu watu 100 na wenye nyumba ndogo ndogo 14 zilizo pakwa rangi, katikati kuna uwanja mkubwa na kisima, bar, na hotel, pia ukumbi wa pamoja. Kuna saloon na ukumbi wa shughuli za michezo na mazoezi, pamoja na soko dogo (minmarket. Kijiji hiki kinakaribishwa watu wenye dalili za ugonjwa wa Alzeima. Hiki ni kutuo cha kwanza nchini Italia wanapokaa watu wasio kuwa na kumbu kumbu. Hii ni tunda la mpango wa Chama cha Roma na baadhi ya mashirika mengine ya Umma. Wazo lilitolewa na Wakili Profesa Emmanuele Francesco Maria Emanuele ambaye aliiga mfano wa kituo kimoja huko Holand, karibu na mji wa Amsterdam ili kuwasaidia wagonjwa Alzeima  kwa  kuwakaribisha kwenye mantiki ya kifamilia. Katika kituo hiki kuna  aina sita  na ambazo zinapendekezwa katika mitindo mitatu ya kuishi,kiutamaduni, kijini na mjini. Na hii ni kutokana na asili ya wagonjwa wanapotokea ili kuweza kutoa huduma ya kusaidia kulingana na mazingira ya kijamii, kisaikolojia, elimu,madaktari bingwa  na baadhi ya mambo mengine yanayo jikita katika suala la kitaaluma. Shughuli nyingi zinazo zinazofanyika kwa watu wanaoishi katika kijiji hicho, baadhi ni kama vile kuchora, muziki na kucheza. Nyumba za kifamilia zimeundwa kwa mtindo wa makundi madogo  wanaoishi humo,kilometa za mraba 250 na bila kuwapo na mipaka ndani mwake mfumo wa ujenzi.

Ugonjwa wa Alzeima (Alzheimer)

Ugonjwa wa Alzeima ,(pia hujulikana kama Udhaifu wa Kiakili utokanao na uzee wa aina ya Alzeima, Kusawijika wa Kimsingi wa Kudhoofika wa Kiakili, au Alzeima tu) ni aina ya kawaida sana ya shida ya akili. Huu ugonjwa usiotibika, wa kusawijika na unaoua, ulielezewa kwa mara ya kwanza na mtaalamu wa magonjwa ya kiakili na ya mfumo wa neva Alois Alzheimer kunako mwaka wa 1906 na ukapewa jina la mtaalamu huyo. Kwa jumla, huwa unatambuliwa kwa watu walio na zaidi ya umri wa miaka 65, ingawa kuna Alzeima ya nadra inayoanza mapema. Kwa mujibu wa ngazi ya dunia ugonjwa huu unawaathiri watu milioni 47. Nchini Italia tu kuna kesi  ya zaidi ya mioni moja na 240. Kwa hakika ugonjwa huu unaua watu kila wiki katika dunianzima na  Alzeima inakadiriwa kuwa itakuwa inaathiri mtu 1 kati ya watu 85 kote duniani kufikia mwaka wa 2050.

Kupoteza kumbu kumbu taratibu ndiyo dalili la mwanzo

Ingawa chanzo cha ugonjwa wa Alzeima ni tofauti kwa kila mtu, kuna dalili kadhaa za kawaida. Dalili za mwanzo zinazoonekana mara nyingi hudhaniwa kimakosa kuwa matatizo 'yanayotokana na umri', au kuonyesha kuwa mtu anafadhaika. Katika hatua za mwanzo, dalili za kawaida zinazotambuliwa ni kukosa uwezo wa kupata kumbukumbu mpya, kama vile matatizo ya kukumbuka mambo yaliyofanyika hivi karibuni. Wakati Alzeima inakisiwa, utambuzi kwa kawaida huwa unathibitishwa na tathmini ya tabia na vipimo vya utambuzi wa mambo, mara nyingi zikifuatiwa na skani ya ubongo kama inapatikana. Ugonjwa unapoendelea, dalili huwa ni pamoja na kuchanganyikiwa, kukerwa na uchokozi, mabadiliko ya hali ya moyo, kutatizika kwa lugha, kupoteza kumbukumbu ya muda mrefu, na mgonjwa kujitenga sana kadiri hisia zake zinavyoendelea kupungua. Hatua kwa hatua, kazi za kimwili hupotea, na hatimaye kusababisha kifo. Ni vigumu kubashiri hatima ya mgonjwa binafsi kwa vile muda wa ugonjwa unatofautiana. Alzeima hukua kwa muda wa kipindi kisichojulikana kabla ya kudhihirika kabisa, na inaweza kukua bila ya kutambuliwa kwa miaka mingi. Muda wa kuishi baada ya utambuzi ni takriban miaka saba. Chini ya asilimia tatu ya wagonjwa huishi kwa zaidi ya miaka kumi na nne baada ya utambuzi. Chanzo na kukua kwa Alzeima huwa havieleweki vizuri. Utafiti unaonyesha kuwa ugonjwa huu unahusiana na tando na mifungamano kwenye ubongo. Kwa sasa matibabu yanayotumika hupunguza dalili ya ugonjwa lakini hakuna matibabu ya kuchelewesha au kusimamisha kuendelea kwa ugonjwa huu.

Hutunzaji wa wagonjwa wa Alzeima ni muhimu

Kwa sababu Alzeima haiwezi kutibiwa na husababisha kusawijika, utunzaji wa wagonjwa ni muhimu. Wajibu mkuu wa mlezi mara nyingi kuchukuliwa na mke au jamaa wa karibu. Ugonjwa wa Alzeima unajulikana kwa kuwatwika walezi wa wagonjwa mzigo mkubwa na shinikizo zaweza kuwa za aina nyingi, zikiwemo za kijamii, kisaikolojia, kimwili, na kiuchumi katika maisha ya mlezi huyo. Katika nchi zilizoendelea, Alzeima ni mojawapo ya magonjwa yenye gharama kubwa sana kwa jamii.

 

13 April 2019, 10:41