Tafuta

Papa Francesco na Kardinali Sean Patrick,Rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi Watoto Papa Francesco na Kardinali Sean Patrick,Rais wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi Watoto  

Hitimisho la Mkutano wa Mwaka wa Baraza la Tume ya Ulinzi

Katika hitimisho la Mkutano Mkuu wa 10 wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto,wamejiwekea mipango kadhaa.Wameweza kufanya mazungumzo na Mashirika na Mabaraza la Kipapa Roma.Hata hivyo katika mantiki ya Tume kuhusu Ulinzi wa Watoto inaonesha ni jinsi gani bado ipo kazi ya kufanya!

Katika taarifa iliyotolewa kuhusu Mkutano Mkuu wa Mwaka uliomalizika tarehe 7 Aprili 2019, Tume inakumbuka kile ambacho kimethibitishwa na Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 24 Februari 209 wakati wa hitimisho la Muutano mjini Vatican kuhusu Ulinzi wa watoto kwamba: “matokeo mazuri na suluhisho mwafaka ambayo tunaweza kutoa kwa waathirika, watu wa Mama Kanisa na dunia nzima, ni jitihada za uongofu wa kichungaji na wa pamoja, kwa unyenyekevu wa kujifunza kusikiliza, kusindikiza na kulinda walio katika mazingira magumu”.

Kusikiliza na kujifunza

Katika mwendelezo wa kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko alithibitisha katika Mkutano wa mkuu wa 10 wa mwaka  wa Tume ya Kipapa ya Kulinda Watoto, ambao ulianza mjini Roma, Alhamisi tarehe 4 Aprili, walianza kusikiliza ushuhuda wa mama mmoja asili ya kutoka Afrika chini ya jangwa la sahara, mwaathirika wa manyanyaso ya kijinsia akiwa mdogo kutoka kwa padre.  Ushuhuda huo ni sehemu ya jitihada za kazi ya Tume inayojikita kwa nguvu zote  kwa lengo la kuwa makini kuwasikiliza waathirika wa manyanyaso. Wajumbe wa Tume walionesha hisia za shukrani kwa sababu ya ushuhuda huo, na ili kuweza kukabiliana na masuala haya magumu ambayo waathirika wengi wameguswa katika mantiki maalum za utamaduni.

Kusindikiza na kulinda

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi ilifunguliwa na  Rais  wake, Kardinali Séan Patrick O'Malley, ambaye alipata kuwakilisha hata salam kutoka kwa  Baba Mtakatifu Francisko. Na zaidi kuonesha shukrani kutoka kwa Papa kutokana na usindikizaji wa Tume katika kuanzisha mipango na mapendekezo ya Mkutano wa mwezi Februari 2019  wa Marais wa Mabaraza ya Maaskofu duniani kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Katika mkutano huo umepata mistari kiongozi na zaidi hata sheria mpya kuhusu ulinzi wa watoto iliyotangazwa hivi karibunu kwa ajili ya  serikali ya Vatican, Vikarieti ya Mji wa Vatican na Jimbo Kuu Roma. Matokeo ya mkutano wa mwezi Februari  anasema unaonesha kwa dhati  utambuzu wa nafasi ya maoni  kuhusu maisha na utume ya Kanisa waliyo nayo kwa mantiki ya Ulinnzi wa Watoto, na wakati huo huo umejionesha wazi ni kwa jinsi gani bado kuha haja ya kupiga hatua mbele zaidi katika mchakato huo.

Mipango ya Tume na mazungumzo  na Vatican

Kwa mwanga huo na kutumwa kwa Baraza maalum la Baba Mtakatifu Francisko na kwa njia ya kuongonza viongozi wa Kanisa mahalia, Tume kwa sasa inapeleka mbele idadi kubwa ya mipango mingi amethibitisha.  Kadhalika shughuli ya tume wakiwa katika makundi tofauti wameendeleza mazungumzo katika Mashirika na Mabaraza ya kipapa, Roma na hasa yale yanayohusika kwa mantiki ya ulinzi wa Watoto kama vile: Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, Baraza Kipapa la Walei Familia na Maisha, Baraza la Kipapa Kipapa la Mashirika  ya Kitawa na  Taasisi za vyama vya Kitume, Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri na Baraza la Kipapa kwa ajili ya maaskofu. Tume pia imemshukuru Askofu Mkuu Charles J. Scicluna wa Malta  kwa kushirikisha wajumbe muda wake na utaalam wake wakati wa Mkutano Mkuu wao. Ikumbukwe kwamba:Tume ya Kipapa ya utetezi wa Watoto, iliunduwa na Baba Mtakatifu Francisko mwezi Machi 2014 , ili kutoa mapendekezo msingi wa kuanzisha ulinzi wa watoto wote na watu wazima katika  mazingira magumu, kwa lengo la kuhamasisha uwajibikaji na kwa namna ya pekee katika makanisa mahalia.

09 April 2019, 10:39