Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu Baraza la Makardinali washauri wa Baba Mtakatifu 

Gisotti:Ni matarajio ya mwisho wa mwaka kutangazwa Katiba mpya ya Kitume!

Msemaji wa mpito wa vyombo vya habari Vatican,Bwana Alessandro Gisotti ametoa mhutasari kwa waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa XXIX wa Baraza la Makardinali washauri na Baba Mtakatifu Francisko,uliohitimishwa tarehe 10 Aprili 2019.Kikao kingine kinatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25-27 mwezi Juni.

Tarehe 10 Aprili 2019 mchana saa saba, Msemaji wa mpito wa vyombo vya habari Vatican, Bwana Alessandro Gisotti amewaeleza waandishi wa habari kuhusiana na mkutano wa 29 wa Baraza la Makardinali washauri  na Baba Mtakatifu Francisko uliohitimishwa na mbao umekuwa ni mwendelezo wa mtazamo na marekebisho kuhusu mchakato wa Katiba ya Kitume ,inayoongozwa na kauli mbiu ya muda: “Praedicate evangelium”. Kikao kingine kijacho kinatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 25-27 Juni 2019.

Mwendelezo wa mchakato wa Katiba mpya ya Kitume

Bwana Gisotti anafafanua kuwa, Baraza la Makardinali washauri wameendeleza mchakato wa kutazama Katiba mpya ya Kitume, jitihada za nguvu zaidi kuhusu upamoja katika Kanisa na pia kuhusu uwepo wa wanawake katika mihilimili ya Vatican. Hizi ndizo mada ambazo zimekuwa kitovu cha mkutano wa 29 wa Makardinali washauri, wakiwa na Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 8-10 Aprili. Washiriki wa Mkutano huo ni Kardinali Pietro Parolin, Kardinali Óscar Andrés Rodríguez Maradiaga, Kardinali  Reinhard Marx, Kardinali Seán Patrick O’Malley, Kardinali Giuseppe Bertello na Kardinali Oswald Gracias.  Wengine zaidi walioudhuria ni Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Askofu Marcello Semeraro, Katibu msaidizi Monsinyo Marco Mellino.

Kikao kipana cha maoni na mitazamo

Kwa kufafanua zaidi katika baraza hilo, Bwana Gisotti amesema,katika siku tatu za mkutano zilikuwa zimegawanywa katika sehemu mbili: asubuhi na mchana,kwa maana hiyo  wajumbe hawa waliendeleza mchakato juu Katiba mpya ya Kitume. Hata hivyo  Muswada uliokubaliwa na Baraza la Mardinali, utaweza kutumwa kwa Mabaraza ya Maaskofu kitaifa, Sinodi ya Makanisa ya Mashariki, Mabaraza ya Kipapa Vatican, mabaraza  ya Mikutano mikuu ya Mashirika ya kike na kiume na badhi ya Vyuo Vikuu vya Kipapa ambavyo wakati huo vitaombwa kutuma maoni na mitazamo yao, baada ya kusoma muswada huo wa Katiba ya Kitume.

Kazi ya ushauri inaendelea

Bwana Gisotti aidha amebainisha kwamba, licha ya kutazama kwa mapana Katiba ya Kitume, lakini pia mada nyingine ziliweza kukabiliwa kwa mapana zaidi wakati wa kazi yao. Mada hizo ni kama vile mwelekeo wa kimisionari ambao Kanisa daima linapaswa kujikita kwa mwanga mpya wa Katiba ya Kitume, juhudi zaidi na kuongeza nguvu katika mchakato wa upamoja wa Kanisa( Synodaliy) katika ngazi zote, vile vile wamegusia  juu ya   mahitaji ya kuongeza wanawake zaidi katika nafasi mbalimbali za uongozi, kwenye  kiungo cha Vatican. Hatimaye  Bwana Gisotti amefafanua kwamba,  Baraza la Makardinali ni kiungo ambacho kina jukumu la kusaidia Baba Mtakatifu, katika kuongoza Kanisa la Ulimwengu, kwa namna hiyo uwajibu wake hauondolei kutoweza kutangaza Katiba ya Kitume.

Shukrani za Kardinali O'Malley

Kadhalika, tarehe 10 Aprili kwa namna ya pekee Karidinali Seán Patrick O’Malley ambaye ni Rais wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na watu wazima wathirika, ameweza kumwonesha Baba Mtakatifu Francisko na Baraza zima, kuhusu kazi yao ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la Tume ya Kulinda Watoto, iliyohitimishwa hivi karibuni. Kardinali amemshukuru Baba Mtakatifu Francisko kuhusu mkutano mjini Vatican ulikuwa unahusu Ulinzi wa Watoto katika Kanisa, ambao ulifanyika 22-24 Februari 2019 pia hata  hivi karibuni, kwa kutangazwa kwa Kanuni mpya ya sheria  kwa ajili ya Serikali ya Vatican, ambayo amethibitisha kwamba inaongeza jitihada zaidi katika Kanisa dhidi ya kupinga kila aina ya manyanyaso ya watoto na watu walio katika mazingira Magumu.

10 April 2019, 16:00