Tafuta

Kwanini Kanisa ni la kimisionari?Je nini maana ya utume leo hii?:Alituma kwenda kufanya umisionaria ni Yesu mwenyewe,kabla ya kuondoka hapa duniani Kwanini Kanisa ni la kimisionari?Je nini maana ya utume leo hii?:Alituma kwenda kufanya umisionaria ni Yesu mwenyewe,kabla ya kuondoka hapa duniani  

Dal Toso:Utume wa kimisionari unaendelea kuwa kipaumbele cha Kanisa!

Kuanzia tarehe 1-6 Aprili 2019 inafanyika Kozi kwa wajumbe wa shughuli za Kimisionari kutoka Afrika,Amerika na Asia,iliyo zinduliwa na Askofu Mkuu Giampiero Dal Toso,Rais wa Baraza la Kipapa la shughuli za Kimisionari kwa mada pana ya kitaalimungu iliyoongozwa na tema ya Utume wa Kanisa na Matendo ya Kimisionari (POM).

Ni washiriki 33 wanaotoka katika nchi 17 zinazo zungumza  lugha ya kifaransa katika bara la  Afrika, Amerika na Ulaya. Ni wajumb viongozi kitafia kwa ajili ya shughuli ya kipapa za kimisionari,(POM) wanaoshiriki kozi  mjini Roma, kwenye kituo cha Kitaifa ya kuhamasisha shughuli za umisionario (CIAM.  Kozi hii inafanyika kwa ajili ya mtazamio wa Mwezi Maalum wa Kimisionari, Oktoba 2019. Kozi imeandaliwa na Sekretarieti ya shughuli ya kipapa za kimisionari,(POM) na CIAM kuanzia tarehe 1-6 Aprili 2019 na mabayo ilizinduliwa na Askofu Mkuu Giampiero Dal Toso, Rais wa Baraza la Kipapa la shughuli za Kimisionari kwa kutoa mada pana ya kitaalimungu ilyoongozwa na tema ya Utume wa Kanisa na shughuli za matendo ya Kimisionari (POM).

Nini maana ya utume leo hii?

Askofu Mkuu Dal Toso akianza tafakari yake katika kozi hiyo  amejikita katika  maswali mawili: Kwanini Kanisa ni la kimisionari? Je nini maana ya utume leo hii? Kwa kujibu anasema, anayeliyetuma kwenda kufanya umisionaria ni Yesu mwenyewe, wakati wa kipindi cha mwisho wa maisha yake hapa duniani. Na kwa maana hiyo utume huo bado unaendelea kupewa kipaumbele cha dhati kwa wabatizwa wote, tangu wanaposhiriki na kuwa sehemu ya Kanisa.  Utume wa Uinjilishaji ambao Kanisa lomepokea kutoka kwake Kristo, ni wito wa kuchuka umbo katika kipindi na katika nafasi, mahali pa kweli, ili kuweza kuweza kufikia watu kwa dhati, ambao  ni binadamu wanaoonekana na kuguswa. Na huo anathibitisha Askofu Mkuu Dal Toso, ndiyo moyo wa utume wao kama utume wa shughuli za kimisionari na pia baadaye kusisitiza na kuonesha huduma yak arama na hduma ya kimisionari. Neno POM linajihusisha kama mtandao duniani wa huduma ya Baba Mtakatifu kwa ajili ya kusaidia utume na Makanisa vijana kwa njia ya sala na sadaka ya kweli. Aidha amesema kwamba hivi karibuni katika ujumbe kwa njia ya video, Baba Mtakatifu Francisko, amethibitisha kwamba POM  ni chombo muhimu , japokuwa hakijajulikana! Hata hivyo naye Askofu Mkuu amethibitisha kwamba ni kweli kutokana na uzoefu wake.

Kambi tano za shughuli za POM

Akiendelea na ufafanuzi, Askofu Mkuu Dal Toso amekumbusha malengo nyeti ambayo yalifanya kuanzishwa kwa chombo cha  POM, waanzilishi wake, hati za Kanisa kuhusu umisionarii na kwa kuonesha muundo na karama yake. Aidha amebainisha hata kambi zake tano za shughuli za POM kwa ngazi ya kitaifa, na kwamba ni kuhifadhi uhai wa roho ya kimisionari kwa njia ya kuhamasisha, na mafunzo ya kimisionari; kutia moyo katika sala; kukukuza mafunzo ya kimisonari; kukuza kwa namna ya pekee utoaji na makusanyo ya sadaka kwa ajili ya Siku ya Kimisionari duniani;na kushirikiana na Shirika la habari za kimisionari Fides, kiungo muhimu cha kutoa habari za POM. Katika sehemu ya pili ya tafakari yake, Askofu Mkuu Dal Toso amesimama kuhusu baadhi ya misingi ya kitaalimungu, ambayo ni msingi wa kazi za kimisionari. Kwa kuanza na Kanisa kama Sakrameni na sura tofauti ambazo zinazingatia Hati za mtaguso wa Baba kwa mfano Lumen gentium ( mwanga wa Mataifa. Anasema kuwa ni kuona kwamba huo ni wakati uliopita wa uhusiano kati ya Kanisa mahalia na Kanisa la ulimwengu kuungana pamoja katika zoezi la kimisionari.  Hata hivyo anabainisha pia kuwa ni hali mbili tofauti, lakini ambazo hazitengani kama POM ambayo kwa mara nyingine tena ni shughuli za Kanisa la  ulimwengu na wakati huo huo  za Kanisa mahalia. Mwelekeo wa tatu wa kitaalimungu umegusia uhusiano kati ya imani na utume  wa watu (Missio ad gentes). Na mwisho uhusiano kati ya ubatizo na kutumwa  vitu ambayo ni tema katika mwezi maalum wa Kimisionari,Oktoba, 2019.

Kubatizwa na kutumwa

Askofu Mkuu Dal Toso akijikita kuzama tema ya Mwezi Maalum wa Kimisionari kuhusu “ Kubatiwa na kutumwa, anasema,Baba Mtakatifu Francisko alichagua tema hii kwa utambuzi wa mambo msingi ya kuzingatia katika mpango mzina  na kutimiza mipango. Wabatizwa na kutumwa, ni kwa maana ya kwamba sisi sote  katika ubatizo  tumepokea maisha matakatifu, neema ambayo sisi tunakuwa manabii yaani waenezaji  wa fumbo la Kristo, waliotumwa na Yeye mwenyewe. Kristo ambaye anatuma, ndiyo mantiki msingi wa utume kwa hakiaka. Hiyo ni kwa sababu Kanisa halitangazi Ujumbe wake binafsi, bali linatangaza na kuonesha kile ambacho kimepokelewa kutoka kwa Kristo, yaani Kristo mwenyewe! Katika kuhitimisha tafakari yake, Askofu Dal Toso amebainisha jinsi gani Kanisa kwa asili ni la kimisionari, hivyo utume ni wa Kanisa kwa ajili yake na ili uweze kuupanuka katika udhati wake, kwenye uzoefu wa kibinadamu, na matendo ya Kristo ambayo yanapitia kwa njia ya watu wa dhati. Kwa wakristo wabatizwa hili ni suala la ushuhuda wa Yesu hasa kuacha yeye aweze kuangaza na kuonekana kwa njia yetu, na ili uso wake uweze kuoneka na na kufuatwa na wanaume na wanawake wa dunia hii!

Missio ad gentes  kamwe siyo propaganda

Kadhalika wakati wa mahubiri ya Misa takatifu ambayo aliongoza asubuhi ya tarehe 1 Aprili 2019, Askofu Mkuu Dal Toso ametoa tafakari kuhusu masomo ya liturujia ya siku na  kusisitizia kwamba utume wa watu ( Misio ad gentes) kwa ajili ya Kanisa hauwezi kamwe kuwa propaganda. Badala yake ni kujitoa sadaka na uhuru wa mtu ambaye anaomba maisha na milele,yaani  katika safari yake ya  maisha na  umilele katika Kristo. Kristo hakubaki katuka shughuli za wayahudi.. Lakini aliweza kuwasadia. Mantendo ya utume ya kimisionari , yanasaidia shughuli za Kanisa ambalo linataka kuwafikishia wote ule uponyaji ambao Kristo Mwana wa Mungu peke yake anaweza kuutoa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

05 April 2019, 14:49