Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI na Baba Mtakatifu Francisko Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI na Baba Mtakatifu Francisko  (Vatican Media)

Benedikto XVI:Mrudieni Mungu ili kuondokana na mgogoro wa unyanyasaji!

Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto wa XVI katika maandishi marefu amekabiliana na suala la kashfa ya unyanyasaji katika Kanisa na kwa maana hiyo wanawalika katika uongofu wa kweli na kwamba mgogoro unawezekana kupungua kwa njia ya kuwa na imani thabiti kwa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nguvu ya ubaya inazaliwa kutokana na kukataa upendo wa Mungu (…) Kujifunza kupenda Mungu ndiyo njia ya kufikia wokovu wa watu. Ndiyo mwanzo wa mandishi ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI katika maandiko  mrefu yanayomeka gazeti mola la Kijerumani liitwalo “Klerusblatt”, na kutolewa na Gazeti la Cna, mahali ambapo nakabiliana na janga unyanyasaji wa watoto uliofanywa na makleri wa makanisa. Katika maandishi yake, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI ananzia kujikita kwenye  mkutano wa mwezi Februari uliopita kuhusu Ulinzi wa watoto katika Kanisa, mkutano ulio pendekezwa na Baba Mtakatifu Francisko, kama “Ishara ya nguvu  na ili kulifanya Kanisa lipate kuaminika kwa mara nyingine tena kama mwanga wa watu na kama nguvu inayosaidia katika mapambano dhidi ya nguvu haribifu”. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu mstaafu anathibisha kuwa yeye anataka kutoa mchango wake katika utume huo japokuwa yeye kwa sasa ni msataaha na hana majukumu ya moja kwa moja. Kutokana na hili anamshuruBaba Mtakatifu Francisko kwa yote ambayo anendelea kuyatenda ili  kutuonesha kila wakati mwanga wa Mungu ambao hata leo anasema bado haufifia. Hata hivyo maandishi yake marefu ya Baba Mtakatifu Mstafu Benedikto XVI yamegawanyika katika sehemu tatu.

Sehemu ya kwanza anazungumzia mantiki ya kijamii, mapunduzi ya unyanyasaji iliyoanza miaka ya 60

Sehemu ya kwanza anazungumzia mantiki ya kijamii, mapinduzi ya kijinsia  iliyoanza miaka ya 60.  Katika kipindi hiki, anaandika, unyanyasaji wa kijinsia ulikuwa unafikiriwa “Kama unaruhusiwa” pia “ni rahisi”. Katika kipindi hiki kinarekodiwa hata “kupunguka kwa miito ya kikuhani”. Na idadi kubwa ya kujiuzuru uhukani, pamoja na kushuka kwa taalimungu maadili  Katoliki, ambapo anabainisha kwamba ilianza kuwa na vishawishi vya mahusiano. Kwa mujibu wa baadhi ya taalimungu anasema, hapakuzekana hata kuwa na kitu chochote kilicho chema, hata kitu daima kibaya, bali walithamini mahausiano. Kulikuwa hakuna tena mema, lakini kile cha wakati tu na kwa mujibu wa wakati huo ambao ulitegemeana na hali. Hata Hivyo Baba Mtakatifu Mstaafu pia anataja kuhusu Tamko la Cologne, nchini Ujerumani, mwaka 1989,uliotiwa sahini na wataalimungu 15 wakatoliki, ambao ulibadilisha kuwa kilio na  maandamano dhidi ya magisterium ya Kanisa na dhidi ya Mtakatifu Yohane Paulo II. Kufuatia hili ndipo ulizaliwa Waraka wa “ Veritatis splendor”, yaani “Mng’ao wa ukweli” mwaka 1993 ambao unatoa uthibitisho kwamba, kuna mambo ambayo hayawezi kuwa mema kamwe. Waamini na watu wenye mapenzi mema wanahamasishwa kukumbatia kweli za Kiinjili na Kanuni maadili kwa mujibu wa Waraka huo.  Katika sekta kubwa ya kitaalimungu maadili, inajikita kufafanua kazi  ambayo Kanisa haijapata wala haiwezi kuwa na maadili yake mwenyewe, uelewa ambao unawekwa kwa kina katika  masuala ya mamlaka ya Kanisa, katika  kambi za kimaadili na hatimaye kuwa kimya, mahali ambapo kuna mchezo kati ya ukweli na uongo.

Sehemu ya pili ya maandishi ya Baba Mtakatifu Mstaafu anazungumzia matokeo ya mchakato

Sehemu ya pili ya maandishi ya Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI anazungumzia matokeo ya mchakato huo wa mafundisho na maisha ya mapadre. Katika baadhi ya seminari anasema,walikuwa wakiunda vyama vya mashoga vingine vilivyoneka wazi  au  siyowazi.Vatican ilikuwa inajua matatizo, lakini bila kuwa na taarifa zidi.  Hisia ya upatanisho kwa hakina ndiyo ilikuwa lengo kama mtazamo muhimu au mbaya mbele ya utamaduni imara hadi wakati huo, ambao sasa ulipaswa kubadilishwa na uhusiano mpya, kwa kiasi kikubwa kuwa wazi na katika  ulimwengu hadi kufikia kuendeleza aina mpya ya kisasa  ya ukatoliki. Hata hivyo Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI anasisitiza kuwa, masuala ya ushoga, anacho kumbuka yeye yalianza kuwa moto katikati ya mwaka 80 na kwa mara ya kwanza ilikabiliwa kwa  taratibu,kuhakikisha hasa haki za mtuhumiwa ambazo ikiwa kama hukumu haiwezekani. Kwa sababu hiyo, anakubaliana na Mtakatifu Yohane Paulo II, juu ya fursa ya kuwakabidhi jukumu la masuala ya unyanyasaji kwa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ili kuweza kutoa adhabi na kama kesi ya kweli ya jinai kwa njia ya mchakato wa wa hukumu na kujiuzuu kwa kuhani.Hata hivyo ilionesha ucheleweshaji na amba haukuweza kuzuilika. Kwa namna hiyo anasema Baba Mtakatifu Francisko ameendeleza kwa kina mageuzi.

Sehemu ya tatu ya maandishi, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI anajiuliza ni majibu gani sahihi ambayo yanaweza kuwa ya  Kanisa

Katika sehemu ya tatu ya maandishi, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI anajiuliza ni majibu gani sahihi ambayo yanaweza kusaidia  Kanisa. Anatoa jibu kwamba, dawa ya mpango wa uovu unaotishia sisi na ulimwengu wote katika siku hizi hauwezi kuwa tofauti na ukweli kwamba tunapaswa kujiachia katika upendo wa Mungu. Hiyo ndiyo dawa ya kweli dhidi ya ubaya. Katika ulimwengu bila kuwa na Mungu haiwezekani ikawa dunia ya maana na ambayo hakuna tena mantiki ya wema na ubaya, bali ni sheria ya wenye nguvu zaidi. Nguvu basi ndiyo inakuwa kanuni pekee msingi. Hakuna anayejali ukweli na zaidi haupo kabisa. Mashitaka makubwa dhidi ya jamii ya Magharibi ambao kwa ujumla wake katika uwanja wa umma, Mungu hayupo na ambapo hawana kitu zaidi cha kusema. Na kwa hiyo ni jamii ambayo kigezo na kipimo cha mwanadamu hupotea zaidi na zaidi na dhahiri kuweza kugeuka uovu na kumharibu mtu  kama kesi ya ushoga.

Kanisa lililofanywa na sisi haliwezi kuwakilisha matumaini yoyote

Uthibitishaji, usio wa muda mrefu uliopita, kama haki  kwamba jibu kwa haya yote, anaandika Baba Mtakatifu Mstaafu ni  kurudia tena kujifunza kutambua Mungu kama msingi wa maisha yetu. Kwa mtazamo huu wa kurudi kwa Mungu, Baba Mtakatifu mstafu anazungumza pia juu ya haja ya kupyaisha imani katika Ekaristi ambayo mara nyingi hupunguzwa maana yake  kwa ishara ya maadhimisha ambayo inaharibu ukuu wa fumbo la  kifo na ufufuko wa Kristo. Badala yake, ni muhimu kuelewa kwa mara nyingine tena ukuu wa mateso yake na ya sadaka yake. Na tunapaswa kufanya kila kitu ili kulinda zawadi ya Ekaristi Takatifu dhidi ya unyanyasaji  wake. Ikiwa tunafikiri juu ya nini cha kufanya, amesema  ni wazi kwamba hatuhitaji Kanisa lingine ambalo linatengenezwa na sisi”.

Mgogoro wa manyanyaso umeleta wasiwasi 

Kanisa leo hii linaonekana kama aina ya vifaa vya kisiasa. Mgogoro uliosababishwa na matukio mengi ya unyanyasaji kwa upande wa makuhani unatoa msukumo wa kufikiria na kushangazwa Kanisa kama limeshindwa na ambalo tunapaswa kuchukua maamuzi na majukumu kwa mikono yetu wenyewe na kufundisha kwa mtindo mpya. Lakini pia Kanisa lililofanywa na sisi haliwezi kuwakilisha matumaini yoyote. Baba Mtakatifu Benedikto XVI anaelekeza matendo ya shetani, mshitaki ambaye anataka kuonesha kuwa hakuna watu wenye haki na ambaye alifanya hivyo hata kwa Mungu. Hapana, Kanisa leo hii, siyo kwamba lina samaki walio haribika au magugu mabaya. Katika Kanisa la Mungu hata leo ni chombo ambacho Mungu anatuokoa. Ni muhimu kupambana na mlaghai na ukweli nusu nusu wa shetani. Ndiyo dhambi na ubaya katika Kanisa upo. Lakini hata leo hii pia kuna Kanisa Takatifu ambalo haliwezi kuharibiwa. Kanisa leo hii, lina mashahidi wengi na mashuhuda wa Mungu aliye hai.

Mwanga wa Mungu hata leo hii bado haujafifia

Na mwisho wa maandishi yake Baba Mtakatifu Mstaafu ambaye anaona na kupata Kanisa, anasema ni kazi nzuri ambayo inaongeza nguvu ndani mwetu na daima mpya ambayo inawafanya tuwe wema wa imani. Anahitimisha akimshukuru Baba Mtakatifu Francisko kwa kile ambacho anafanya ili kuonesha kwa wote kuwa mwanga wa Mungu hata leo hii bado haujafifia. Asante Baba Mtakatifu!

11 April 2019, 15:41