Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Serverus Jjumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Masaka, Uganda. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Padre Serverus Jjumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Masaka, Uganda. 

Mh. Padre Serverus Jjumba ateuliwa kuwa Askofu wa Masaka, Uganda

Askofu mteule Jjumba alizaliwa kunako tarehe 2 Agosti 1962 Jimboni Masaka. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja takatifu ya Upadre tarehe 20 Juni 1992. Katika maisha na utume wake kama Padre: amewahi kuwa Paroko usu, mlezi na mchumi wa Seminari ndogo Bukalasa, Mchumi wa Jimbo pamoja na hatimaye kuwa Makamu Askofu Jimbo la Masaka, Uganda.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilishwa kwake na Askofu John Baptist Kagwa wa Jimbo la Masaka la kutaka kung’atuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Mheshimiwa sana Padre Serverus Jjumba kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Masaka, Uganda. Askofu mteule Serverus Jjumba alizaliwa kunako tarehe 2 Agosti 1962 Jimboni Masaka. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa daraja takatifu ya Upadre tarehe 20 Juni 1992.

Baada ya upadrisho, katika maisha na utume wake kama Padre kwanza kabisa: alitumwa kujiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Makelele, Uganda na huko akajipatia Shahada ya Uzamili katika masuala ya elimu. Amewahi kuwa Paroko usu, mlezi na mchumi wa Seminari ndogo Bukalasa na kuanzia mwaka 2000-2014 akateuliwa kuwa mchumi wa Jimbo Katoliki la Masaka.  Kuanzia mwaka 2014 hadi kuteuliwa kwake, amekuwa ni Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Masaka.

Jimbo la Masaka
16 April 2019, 15:34