Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amemteua Askofu Dabula Anton Mpako kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Pretoria na Askofu wa Jimbo la Kijeshi Afrika ya Kusini. Papa Francisko amemteua Askofu Dabula Anton Mpako kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Pretoria na Askofu wa Jimbo la Kijeshi Afrika ya Kusini.  (AFP or licensors)

Askofu William Slattery ateuliwa kuwa Askofu mkuu wa Pretoria

Baba Mtakatifu amemteua Askofu Dabula Anton Mpako kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Pretoria na Askofu wa Jimbo la Kijeshi Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Dabula Anton Mpako alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Queenstown, Afrika ya Kusini. Alizaliwa mwaka 1959, Akapadrishwa mwaka 1986, Mwaka 2011 akateuliwa kuwa Askofu wa Queenstawn.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu William Mathew Slattery, O.F.M wa Jimbo kuu la Pretoria na Askofu wa Jimbo la Kijeshi Afrika ya Kusini. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu Dabula Anton Mpako kuwa Askofu mkuu mpya wa Jimbo kuu la Pretoria na Askofu wa Jimbo la Kijeshi Afrika ya Kusini. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Dabula Anton Mpako alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki Queenstown, Afrika ya Kusini.

Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Dabula Anton Mpako alizaliwa tarehe 6 Septemba 1959. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 28 Juni 1986 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo kama Padre akafanya utume sehemu mbali za Jimbo kuu la Pretoria kama Paroko-usu, Mlezi na Gombera. Kati ya mwaka 1991-1994 akatumwa na Jimbo kuu la Pretoria kwa masomo ya juu zaidi, Chuo Kikuu cha Loyola kilichoko nchini Marekani ili kujiendeleza katika Taalimungu ya shughuli za kichungaji.

Kati ya Mwaka 1994-1998 akateuliwa kuwa Gombera wa Seminari kuu ya Falsafa ya St. Peter, huko Garsfontein. Kati ya mwaka 1999-2004 akateuliwa kuwa Paroko na Dekano. Kati ya Mwaka 2005-2010 akateuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya St. Columba, na Mwaka 2010-2011, akahamishiwa kwenye Parokia ya Mt. Thomas Moore. Tarehe 6 Agosti 2011 akateuliwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Queenstown. Askofu mkuu mteule Dabula Anton Mpako ni Makamu wa Rais, Baraza la Maaskofu Katoliki Afrika ya Kusini.

Papa: Uteuzi Afrika

 

 

30 April 2019, 14:40