Tafuta

Vatican News
Tarehe 27 Aprili 2019 ametangazwa Mwenyeheri Askofu Enrico Angelo Angelelli Carletti na wenzake watatu nchini Argentina Tarehe 27 Aprili 2019 ametangazwa Mwenyeheri Askofu Enrico Angelo Angelelli Carletti na wenzake watatu nchini Argentina 

Argentina:Kanisa la Argentina kuwapata wenye heri wapya!

Tarehe 27 Aprili 2019 huko Rioja nchini Argentina Kardinali Angelo Becciu Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu ameongoza Misa Takatifu ya kuwatangaza wenyeheri wapya Askofu Enrique Angelelli,watawa wawili Carlos Murias,Gabriel Longueville na mlei mmoja Wencislaus Pedernera wafia dini kwa ajili ya kutetea imani yao

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 27 Aprili 2019 huko Rioja nchini Argentina Kardinali Angelo Becciu Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu, amemwakilisha Baba Mtakatifu katika maadhimisho ya misa Takatifu ya kuwatangaza wenyeheri wapya wa Kanisa, Askofu Enrique Angelelli,watawa wawili ambao ni Carlos Murias, Gabriel Longueville na mlei mmoja Wencislaus Pedernera waliouwawa kunako mwaka 1976 katika mwaka wa udikteta wa kijeshi.

Katika mahubiri:liturujia inawaalika kujipyaisha kipindi cha Pasaka

Katika mahubiri yake,Kardinali Becciu kwa kuongozwa na maandiko matakatifu anasema Liturujia inawaalika kujipyaisha kila wakati katika kipindi cha Pasaka na ambacho kwa siku hiyo wanajikuita katika  kuadhimisha hata siku ya kuwatangaza  wafiadini wanne kama jibu kwa namna ya pekee ya utayari na furaha. Ni furaha na kushangilia katika Bwana kwa ajili ya zawadi ya wenye heri wapya, hawa ambao kwa ujasiri waliweza kushuhudia Kristo na  sasa wanastahili kupewa sifa na Kanisa na kuigwa na watu wote waamini. Kila mmoja anaweza kurudia maneno ya Kitabu cha ufunuo katika somo la Kwanza: “Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake (Uf 12,10) anasema Kardinali Becciu. Nguvu ya Kristo mfufuka ambayo inaendelea kwa karne nyingi kwa njia ya Roho Mtakatifu inandelea kuishi na tena kwa waamini na kuwasukuma kuelekea katika matendo ya Ujumbe wa Kinjili.

Wenyeheri wapya walitambua daima msaada wa Mungu wakati wa kuteswa kwao

Kardinali Becciu anasema kwa utambuzi wao, wenye heri wapya daima walitambua msaada wa Mungu ambao waliupata wakati wa kuteseka kwa ajili ya haki ( 1Pt3,14) na kwa maana hiyo daima walikuwa tayari kujibu kwa kila sababu ya matumani ya wito wao (1Pt 3,15). Walijitoa sadaka wenyewe kwa Mungu na kwa jirani katika ushujaa wa kushuhidia  kikristo hadi kufikia taji la kifo dini . Kanisa leo hii lina utambuzi kuwa,Enrique Angel Angelelli, Askofu wa  Rioja, Carlos de Dios Murias, Mfransisikani Gabriel Longueville, padre mmisionari wa fidei donum na Katekista Wenceslaus Pedernera, baba wa familia walikashifiwa na kuteswa kwa ajili ya Yesu na hali ya Kiinjili (rej Mt 5,10-11), na sasa wanapokea zawadi yao mbinguni  (Mt 5,12).  Heri ninyi ! (Mt 5,11; 1Pt 3,13) Je ni kwa namna gani tusiweze kuhisi maneno hayo yakitolewe kwa wanyeheri wapya hao katika sisi? Anauliza Kardinali Becciu. Wao walikuwa mashuhuda wa Injili na kubaki imara katika upendo wa Kristo na Kanisa lake kwa zawadi ya mateso na sadaka ya maisha yao yote. Hiyo yote ilitokana na  kazi ya mafunzo  ya imani, jitihada za kidini na kijamii na kwa  kubaki na msimamo wa Injili kwa ajili ya amani zaidi. Hii pia ilitokana na kujikita kwa kina katika matendo ya mwanga wa Mtaguso wa  II wa Vatican na kuishi na matashi ya kuweza kuendeleza uhai wake wa mafunzo hayo. Kutokana na hlo, Kardinali anasema, hawa tunaweza kusema kwa maana nyingine ni mashahidi wa Hati ya mtaguso! Waliuwawa kwasababu ya kuendeleza shughuli ya kuhamasisha uhai kikristo. Na kwa maana wakati ule jitihada za kudai haki kijamii na uhamasishaji wa hadhi ya binadamu ulikuwa unatiliwa vikwazo vingi na viongozi wa raia.

Mwenyeheri Enrique Angel Angelelli alikuwa ni mchungaji jasiri

Mwenye Enrique Angel Angelelli alikuwa ni mchungaji jasiri mara baada ya kufika Rioja na ambapo aliweza kujikita kusaidia watu walio masikini na waathirika wa ukosefouwa haki. Padre Carlos de Dios Murias na Gabriel Longueville walikuwa na uwezo wa kupokea na kujibu changamoto za uinjilishaji ambao unajikita kwenye ukaribu wa watu. Wenceslao Pedernera, katekista alikuwa ni mjumbe hai wa chama katoliki cha vijijini na  ambaye alitumia muda wake wote na ukarimu katika shughuli za kijamii na kwa imani; Mnyenyekevu na mpenda watu wote. Wenyeheri wapya Kardinali Becciu amesema ni mfano wa kuigwa wa maisha ya kikristo. Mfano wa Askofu anafundisha wachungaji leo hii kutoa huduma yao kwa moto wa upendo na kuwa na nguvu ya imani mbele ya matatizo. Mapadre wawili wanatoa ushauri kwa mpadre wa leo hii kujikita kwa nguvu zote katika sala na ili kuweza kukutana na Yesu  na upendo wake na zaidi kuwa na nguvu ambayo haikosi kamwe kuwa muhudumu wa kikuhani. Kuwa waaminifu kwa gharama zozota katika utume na utayari wa kukumbatia msalaba. Baba wa familia anafundisha walei wote kutambua namna ya kutengenisha uwazi wa imani na kuacha kuongozwa nayo katika maamuzi muhimu ya maisha.

Waliishi na kufa kwa ajili ya upendo

Hawa waliishi na kufa kwa ajili ya upendo. Maana ya kifodini leo hii ni kwamba wao walikuwa mashuhuda ambao hawakuishi na ubinafsi au kijenga mitindo ya kijamii iliyofungwa bila kuwa na mwongozo wa thamani za kimaadili na kitasaufi. Wafia dini wanatusahuri sisi na kizazi kijacho kufungua moyo wa Mungu na dni na kuwa na ashauka ya amani, wahaudumu wa haki na ushuhuda wa mshikamani, licha ya ukosefu wa ulewa, majaribi na ugumu. Wafiadini hawa wa jimbo hilo anasema wanakiumbusha kwa dhati kuwa  ni vema kwa hakika kama Mungu anataka uteseke ukiwa unatenda mema kuliko kutenda ubaya  (1Pt 3,17). Kardinali Becciu amehitimisha akiwashukuru uaminifu wa hawa wafiadini na kuwaomba waamini wote waendelee kuonesha mfano, kama ilivyo hata kwa watu wote nchini Aregentina na kuwajibika! Aidha mfano wao na sala za wenye heri hao wandelee kuwahasa waamini wawe na imani na mashuhuda wa Injili, wajenzi wa jumuiya, wahamasishaji wa Kanisa linalo jikita kushuhudia Injili katika kila mantiki ya  jamii  na kujenga madaraja ya mshikamani, ushirikoshwa na wakati huo huo wakiangusha kuta za sintofahamu. Mwenyeheri Enrique Angel Angelelli na wenzake watatu watuombee!

29 April 2019, 09:47