Tafuta

Vatican News
Mwenyeheri  Angelo Cuartas Cristobal na wenzake wafiadini nchini Hispania kati ya mwaka 1936-1937 Mwenyeheri Angelo Cuartas Cristobal na wenzake wafiadini nchini Hispania kati ya mwaka 1936-1937 

Wafia dini 9 wametangazwa kuwa wenyeheri wapya nchini Hispania!

Tarehe 9 Machi 2019 katika Kanisa Kuu Katoliki la Oviedo nchini Hispania,wametangazwa Wenyeheri wapya ambao ni wafia dini,waliouwawa kati ya mwaka 1936-1937. Na kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko,maadhimisho hayo yameongozwa na Kardinali Angelo Becciu, Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Hakuna kilicho kikuu zaidi ya kujitoa maisha kwa kile ambacho unapenda na ndiyo mafundisho ya wafiadini ambao kati yao ni wale wapya wakiwa wotye ni vijana ambao walipendelea kufa zaidi ya kujificha kwa sababu ya kuteswa wakitete imani yao.  Hawa walikuwa ni waseminari waliompenda Bwana na walikuwa wamefanya uchaguzi wao kwa hakika kutoa maisha yao kwa Bwana. Hawa walifanya uchaguzi huo hadi sadaka ya mwisho.Uchaguzi wa imani kwa Kristo na ambapo inapaswa iwe mafundisho makubwa kwa mapadre wote  na kuwajibika kwa dhati katika wito wao.  Haya yamethibitishwa na Kardinali Angelo Becciu, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Wenye heri na Watakatifu, ambapo akihojiana na mwandishi wa habari tarehe 9 Machi 2019 kabla ya kuwatangaza wenye heri wapya Ángel Cuartas Cristóbal na wenzake waseminari waliouwawa kati ya mwaka  (1936-1937) Jimbo Kuu Oviado nchini Hispania.

Akianza kueleza historia ya hawa vijana wafiadini Kardinali Becciu anasema mwaka 1934 nchini Hispania ulikuwa ni mwaka mgumu sana ambapo mashambulizi dhidi ya wakristo yalikuwa ni makubwa mno. Vilevile kwenye miaka hiyo  itakumbukwa kwa vita vya kispanyola kati ya mwaka 1936-1939 na baadaye pia vifo vya wengine katika Vita ya pili ya Dunia katika mji wa Asturie. Kulikuwa na mapambano kila sehemu na umwagaji damu katika miji mingine ya Oviedo, mahali ambapo watu wengi, hasa mapadre na watawa waliuwawa bila sababu. Baada ya vita  inahesabikiwa kuwa waliuwawa watu 6,832 na waathirika hawa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe raia wa kispanyola  ambao kati yao walikuwa ni watawa, mapadre na walei walio uwawa kwa sababu ya kutetea imani ya dini katoliki, anathibitisha  Kardinali Becciu.

Waseminari wa Oviedo ni mashuhuda wa imani kwani mwisho wa kiangazi cha mwaka 1934, Angel Cuartas Cristóbal mmoja wa waseminari wengi alipomaliza likizo yake nyumbani alikuwa arudi katika  Seminari kuu ya Oviedo mahali ambapo kwa miezi kadhaa alikuwa amepewa daraja la ushamasi. Mseminari huyo alikua ni mmoja kati ya watoto 9 wa familia yake ambayo ilimshauri hasirudi Oviedo, kwa maana kulikuwa na mambo mabaya yakitokea. Yeye lakini hakutii wazazi wake, kwa maana alikuwa na  utambuzi  kuwa ndipo Bwana anamtaka wito wake na  hata kama angeuwawa. Uamuzi huo pia ndiyo ulikuwa sawa na wenzake watano ambao kama yeye walikuwa wameamua kurudi Seminarini. Wote hao walikuwa ni vijana wafiadini. Suárez Fernández, aliamua kuendelea na masomo kwani mwaka huo alikuwa afunge nadhiri, Jesús Prieto López, familia yake ilikuwa maskini na karo ilikuwa analipiwa na Parokoko wake;  César Gonzalo Zurro Fanjul, yeye alikufa akipaza sauti yake kuwa “Yesu ni hai, ukatoliki nchini Uhispania hoyee! José María Fernández Martínez, alikuwa ni mtoto yatima wa mama yake na baba yake alikuwa anafanya kazi katika mashimo ya machimbo;Juan José Castaňon Fernández, ndiye aliyekuwa mdogo zaidi katika kundi hilo kwa maana alikuwa mehitimisha miaka 18 tu na aliyekuwa mkubwa kati yao alikuwa na umri wa miaka 24.

Hali halisi ya vurugu na ghasia iliendelea  kueneza kama virusi nchini kote. Sura za kumkana Mungu ndizo zilikuwa zinataka zitawale na kuonekana ukisasa anaongeza Kardinali Becciu. Itikadi hizi iliendelea kusababisha waathirika wengi sana wakiwa ni walei na watawa kama ilivyo kuwa hata kwa hawa watatu ambao wanatangazwa wenye heri. Manuel Olay Colunga, alikuwa ameponea chuchupu kifo huko Asturie miaka miwili kabla, kwani aliweza kujificha kwa mwaka mmoja kabla ya kumkamata na kumuua; Sixto Alonso Hevia, alikamatwa pamoja na baba yake mkatoliki hai na wote wawili walifungwa kwa muda mrefu sana katika moja ya parokia ya kijiji waliyokuwa wameigeuza  kama gereza kala ya kufiadini mwaka 1937; na mwisho Luigi Prado García, ambaye alikuwa ameingia kufanya  huduma ya kijeshi na akauwawa katika forodha ya Gijon. Akihitimisha juu ya historia ya wafia dini hao, Kardinali Becciu anasema: “mbele ya  sura za vijana wadogo hawa nahisi kuwa mdogo kwa sababu ya na ushuhuda wao na unanialika na sisi sote makuhani  kuishi kwa ukamilifu na uwajibikaji katika wito wetu!

Katika mahubiri ya Kardinali Becciu wakati wa kutangaza wenye heri wapya  waseminari wa Oviedo nchini Uhispania, tarehe 9 Machi 2019 kwa kuongozwa na Injili iliyosomwa anasema: Injili tuliyosikia daima inatoa mshangazo wa wito wa Mtume Matayo ambaye alijukana kama Levi, (mtoza ushuru) kwa mujibu wa utamaduni,wale ambao walikuwa na uhusiano na mali, walikuwa wanachanganya jina la kiyahudi kwa naama ya kigiriki au kilatino. Mwinjili Luka anameeleza mambo msingi ya kukutana  kati ya Matayo, Mtoza ushuru na Yule ambaye alikuwa ambadilishe maisha yake kwa dhati.  Lakini kabla ya kukutana ni wakati huo mwaliko unatoka kwa Yesu ambaye anamwambia Matayo, ni mwaliko usio na kikomo kwa kusema: Nifuate! Na ndiyo mwanzo huo huo wa mtoto wa Alfeo kuanza wakati mpya wa maisha yake maana hatawaomba tenda kodi wazalendo wa Kafaranaum ili kutoa mchango wa mamlaka ya umma na ndiyo maana alijulikana mtoza ushuru. Hiyo ndiyo ilikuwa hali halisi ya maisha yake kwa wakati huo akiomba watu wampatie kilicho chake Mungu na katika imani yao.

Hata hawa wenye heri wapya  Angelo, Mariano, Jesus, César Gonzalo, José Maria, Juan José, Manuel, Sixto na  Luis, siku moja walisikia sauti ya Mwalimu Mungu akitamka Nifuate! Walijitoa maisha yao kwa wito wa Mungu na kuanza mchakato wa safari ili waweze kuwa makuhani wa Bwana. Lakini neno la nifuate, ili kuwa inatakiwa uwe hodari na shujaa, na kwa mara nyingine wao walitamka ndiyo. Hawakusita kukiri upendo kwa Yesu wakipanda na Yeye juu ya Msalaba. Katika kutoa sadaka yao ya mwisho wakiwa vijana wa maisha.  Kwa kuongozwa na ushuhuda wa imani katika Yesu, wafiadini wapya waliathirika na ukatili wa nguvu ambao ulikuwa ni kizingiti cha ukatoliki. Watesi wao walikuwa na lengo la kuondoa Kanisa kwa namna ya pekee makuhaji. Kuteswa kwao na kuwawa ilikuwa inatosha tu kutambua kuwa hiyo ni mseminari. Vijana waseminari wa Jimbo Kuu la Oviedo walikuwa na uhakika wa wito wao kuwa makuhani wa huduma ya sakaramenti na jitihada  katika safari yaoya majiundo  ili wawe wahudumu wa Injili.

Kardinali Becciu akiendelea na mahubiri anasema Zaburi ya maadhimisho hayo iliyosoma (Zab 85 ) imewawezesha kwa namna nyingnie kutazama  vipindi halisi vya ushuhudu wa wafia dini kwa vijana hao waseminari. Je ni mara ngapi watakuwa walisali Zaburi isemayo Bwana uyahifadhi maisha yangu maana mimi ni mchaji wako, uniokoe mimi mtumishi wako ninayekutegemea? Anaongeza kusema katika  saa zao za majaribu bila shaka waliendelea kusema:Wewe ni Mungu wangu basi unionee huruma, maana nakulilia mchana kutwa, unifurahishe roho yangu mimi ni mtumishi wako maana sala zangu naziekeleza kwako ee Bwana.

Na kwa maana hiyo wenye heri wapya wakati wa kufiadini ndipo waliokoa maisha yao. Walitoa maisha yao hapa duniani ili kupata maisha yao ya kweli ya milele na Kristo. Pamoja na Yesu katika sakramenti ya ubatizo walianza maisha yao mapya. Na tazama kwa kuanguka katika mikono ya watesi wao, waliweza kutoa ushuhuda wao wa mwisho katika ardhi hii, maisha ambayo yamo ndani mwao. Kifo cha mwili hakikuharibika. Kifo maana yake ni  mwanzo mpya wa maisha ambayo ni ya Mungu na kugeuka kuwa sehemu moja kwa ajili ya Kristo, aliyeteseka akafa na kufufuka. Waseminari 9 waliuwawa lakini kifo cha wasio na hatia hawa kinatangaza nguvu kwa namna ya pekee ukweli wa nabii Isaya katika somo la kwanza kuwa: Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui. (Is 58,10)

Leo hii Kanisa linatambua mwanga kwa  hawa wenye heri 9 ambao  unaangaza katika giza nene la usiku na kuendelea kumlikia njia za waamini wa leo. Kwa maana hiyo Kanisa linawatangaza Wenyeheri na kumshukuru Bwana kwa uweza wake  ambao aliuonesha kwa njia ya maisha yao ya kikristo, kifadhila na ushujaa wa kifo chao. Ushuhuda wao ni mkubwa wa sasa,wao hakukumbatia matatizo tu badala yake walichagua imani kwa Kristo. Ujumbe wa hawa waseminari wafiadini unazungumza kwa nchi ya  Uhispania na kwa Ulaya  nzima juu ya  mizizi yake ya kikristo. Hawa wanakumbusha kuwa, upendo wa Kristo unazidi zaidi ya kila chaguo lolote lile na udhati wa maisha unaweza kukupelekea hadi  kufikia kifo. Ha wanakumbusha kuwa hewezi kubakia katika hadi tu za kidhami na hakuna madaraka yoyote ya kibinadamu yanaweza kushindana na ya Ukuu wa Mungu. Katika utakatifu, wa maisha yao kwa hawa wenyeheri wapya wanazungumza kwa Kanisaleo hii. Damu yao imefanya makubwa katika Kanisa na walitoa mwangaza wa kikuhani.  Wote tuna wasi wasi juu ya kashfa ambazo utafikiri hazina mwisho wa kuharibu uso wa Mchumba Kristo. Kuna hata waseminari,mapadre na watu waliotoa wakfu, wachungaji wakarimu kama wafia dini hawa wa Oviedo. Kuna haja ya mapdre waaminifu na wawajibikaji ambao wapeleka  roho kwa Mungu na siyo kusababisha mateso kwa Kanisa na dukuduku  kwa  watu wa Mungu!

 Ujumbe wao na ufiadini, wa wenyeheri wapya, unazungumza kwetu sote na kukumbusha kuwa, kifo kwa ajili ya imani ni zawadi tu ambayo imepewa kwa watu wachache; lakini pia kuishi kiimani ni mwaliko kwa wote amethibitisha Kardinali Becciu. Kwa mifano yao na maombezo ya vijana hawa waseminari wenye heri watusaidie kupyaisha ufuasi wetu kwa Yesu, kwa kuonesha mifano ya maisha ya mtu mpya ambaye ameufikia kwa njia ya ubatizo. Wasaide kila mbatizwa kutembea katika njia ya utakatifu na kutazama  wao kama mifano wazi ya kuendelea kujitoa bila kujibakiza mbele ya wito wa Mungu. Kwa njia hiyo Kardinali Becciu amemamaliza kwa kusema kuwa tusali: Mwenyeheri Angelo Cuartas Cristobal  na wenzako 8 wafiadini mtuombee!

 

 

09 March 2019, 12:06