Tafuta

Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Mtandao wa Vituo vya Radio Barani 2019 unajikita katika kutazama matarajio na changamoto za utangazaji Barani Afrika Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Mtandao wa Vituo vya Radio Barani 2019 unajikita katika kutazama matarajio na changamoto za utangazaji Barani Afrika  

Ruffini:Kuna haja ya kufikiria uzalishaji wa matangazo Afrika!

Kuanzia tarehe 27 hadi 29 Machi 2019,nchini Morocco unafanyika Mkutano mkuu wa 12 wa Shirikisho la Mtandao wa Vituo vya Radio Barani Afrika, ambapo Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Mawasiliano Vatican Bwana Paulo Ruffini katika ujumbe wake anaelezea changamoto zinazokabili vyombo vipya vya habari barani Afrika

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 27 Machi 2019, asubuhi, umefunguliwa  Mkutano wa 12 wa Shirikisho la Mtandao wa Vituo vya Radio Barani Afrika ambao utafungwa tarehe 29 Machi 2019 huko nchini Morocco, ambapo  Bwana Paulo Ruffini, Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano Vatican ametuma ujumbe wake. Mkutano huo unajaribu  kutazama matarajio na changamoto za utangazaji Barani Afrika kwa kuongozwa na kauli mbiu vyombo vipya vya habari na ushawishi wake katika sekta ya kusikiliza Afrika.

Kutokana na kauli mbiu hiyo, ujumbe wa Bwana Ruffini kwa lugha ya kifaransa ukatika fursa hiyo unaanza kwa salam kwa viongozi wakuu na wajumbe wote washiriki wa Mkutano huo hasa kusisitiza kuwa kuwa mada waliyoichangua ni mada kubwa ya sasa kwa sababu ya vyombo vipya vinatoa changamoto mpya. Na changamoto hizi zina ukuu wake. Mkutano huo kwa mantiki ya Afrika  katika mapinduzi ya kidigitali ni ya ulimwengu kwa maana iweka mbele ya hali halisi, hasa kwa upande  wa vyombo vya kiufundi ambavyo kwa miaka mingi iliyopita, leo hii karibu vimewekwa pembeni. Kwa jinsi hiyo mitindo ya kisasa ya vyombo vya kiteknolojia, vinaendelea kukua na kuwa msingi katika viwanda vya sauti na  katika picha.

Uzalishaji wa vyombo vya habari, vya wakati uliopita, ilikuwa vinaundwa kwa namna ya kujitolesheleza, lakini leo hii vinaelekea kuachwa kutokana na kwamba mwandiko wake , sauti zake na picha kwa sasa vinajikuta kuwa katika bandari moja au tovuti. Na wakati huo huo, biashara au uzalishaji wa vipindi unakabiliana na changamoto mpya ambayo kwa mfano, ni vigumu kuthibiti haki ya mtunzi au kulinda wazalishaji wa bajeti iliyo ya chini. Rais wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa maana hiyo anakazia ulazima wa kufikiria mfumo mzima wa uzalishaji na usambazaji. Hii ni changamoto kubwa kwa vyombo vya habari. Je ni kwa njia zipi Afrika inaweza kuwa sehemu ya mzunguko wa dunia, ambao kazi yake kubwa sana mara nyingi inakuwa na  ukiritimba wa uzalishaji na usambazaji? Au ni kwa njia zipi za kukabiliana kwa ujumla na uharibifu katika mapinduzi na makubaliano katika uwanja wa vyombo vya habari? Haya yote ndiyo maswali ya kujiuliza anabainisha Bwana Ruffini

Afrika isijiingize katika soko la ukiritimba wa wazalishaji wakubwa: Bwana Ruffini akiendelea na hotuba yake amebainisha kuwa kwa maana nyingine Afrika haipaswi kuadhibiwa katika masoko ya ukiritimba wa wazalishaji wakubwa na wakati huo huo vyombo vyake vya habari havipaswi kuhudumia kwa kurushwa na viwanda vyenye nguvu zaidi ambavyo vinaweza kuvamia soko la Afrika. Iwapo vyombo vipya vya habari vinaendelea kubadilika katika dunia ya mawasiliano, kwa namna ya pekee kwa njia ya mfumo kimantiki, mabadiliko hayo yasisahaulishe ukuu wa binadamu, hata katika uzalishaji wake kwa ngazi ya viwanda. Hata Hivyo katika katika ujumbe wake Bwana Paulo Ruffini anakumbusha juu ya Baba Mtakatifu Francisko akizungumza katika ujumbe wake kwa ajili ya siku ya 53 ya Mawasiliano ya kijamii duniani. “wataalam wengi kuhusiana na mabadiliko ya kina ya viwanda vya kiteknoloja, katika mantiki ya uzalishaji, mazungumzo na usambazaji wa dhana hiyo, inaonesha hatari inayotishia utafiti na ushirikishwaji katika ngazi ya dunia. Iwapo inteneti inawakilisha uwezekano maalum wa hufahamu na  ndiyo kweli kwamba umejionesha kuwa  sehemu yenye nafasi kuu ya kutoa habari za kugushi au kupindisha ukweli, katika mtazamo, matukio na mahusiano binafsi, ambayo mara nyingi hayatolewi kwa mtindo unao aminika.

Baba Mtakatifu anasisitiza katika ujumbe wake wa Siku ya 53 ya Mawasiliano  duniani,kuwa sura ya mtandao inapaswa itoa tafakari kwa wote na ushiriki wa wote. Mtandao unakuwepo, kwa sababu ya ushiriki wa vitu vyote. Vyombo vya habari vipya siyo tu viwanda vya sauti kwa ajili ya Afrika, bali vinasambazwa hata kwa namna ya kuwapo, kuishi, kuwa na mahusiani na wengine. Na hatuwezi kuhepukana na mambo hayo anathibtisha katika ujumbe. Hiyo ni kwa sababu katika mazungumzo yanaonesha ukweli na ukweli unamwilisha mazungumzo. Baba Mtakatifu anatafsiri  na kuwaona waandishi wa habari kama watafuta ukweli.

Ni matashi yake Bwana Ruffini kwamba, mazungumzo ya kubadilishana yaweze kuleta matunda mema  na kupata mwafaka katika kuanzisha vyombo vipya vya habari katika kiwanda cha usikivu wa Afrika.  Aidha amekumbusha  katika jukwaa lililofanyika nje ya mkutano huu na kuongozwa na mada ya Mchango wa wasimamizi katika mchakato wa mpito kutoka katika ulimwengu wa “analogia” kuingia katika ulimwengu wa “digitale”. Hata hivyo  Bwana Ruffini amethibitisha huo ni mwendelezo wa mchakato wa Jukwa  lililofanyika mjini Kigali Rwanda kunako 2018 na ambalo lilijikita zaidi kuhusu mabadiliko ya teknolojia kutoka katika ulimwengu wa “analogia” kuingia katika ulimwengu wa “digitale”.

27 March 2019, 14:39