Tafuta

Vatican News
Padre Raniero Cantalamessa,Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa katika tafakari ya Kwaresima 2019 inaongozwa na mada “In te ipsum redi” yaani “Ingia ndani mwako” Padre Raniero Cantalamessa,Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa katika tafakari ya Kwaresima 2019 inaongozwa na mada “In te ipsum redi” yaani “Ingia ndani mwako”  

Padre Cantalamessa:Tatafuteni mtazamo wa Mungu na siyo wa binadamu!

Ni katika mapambano ya unafiki ambao ulihukumiwa na Yesu kwa nguvu zote ambapo Yeye anazidi kutoa ushuri wa kushinda vishawishi hivi kwa kufanya kazi kila siku na kutoa kipeumbecha cha Mungu kuliko binafsi.Ni katika tafakari ya kwanza ya Kwaresima mwaka 2019 aliyoitoa Padre Cantalemsaa kwa wahudumu wa nyumba ya Kipapa Vatican

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika tafakari ya kwanza ya Kipindi cha Kwaresima kwa Mwaka 2019 Padre Raniero Cantalamessa, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa kwa kuongozwa na kauli mbiu “In te ipsum redi” yaani “Ingia ndani mwako” ambayo ni sehemu ya maneno ya Mtakatifu Agostino, Askofu na Mwalimu wa Kanisa Padre anathibitisha kuwa ni mwendelezo wa mafungo ya mwaka jana. Kutokana na hivyo, tarehe 15 Machi 2019 wakati wa tafakari yake ameanza na swali moja kuwa: je ni hali gani msingi ya kuweza kuinua mtazamo kwa Mungu? Na katika katika kujibu swali hili ametumia mfano wa hotuba ya Yesu mlimani:“Heri wenye usafi wa moyo kwa maana watamwona Mungu”.

Aliye ishi kimwili amejaa tamaa za kimwili

Padre Cantalamessa katika  maana nyingi za usafi wa moyo, amependa kuchagua mbili, ya kwanza unyofu wa nia, na usafi wa kidesturi au  kawaida. Akifafanaua anasema, tofauti zake kwa upande mwingine ni unafiki na kwa upande mwingine ni katika matumizi ya ngono. Akifafanua masuala yanayozungukia nyanja ya ngono, Padre Cantalamessa anasema hiyo dhambi chafu kwa kawadia haitazami uso wa Mungu au kama inauona, daima  inaona kila kitu kimepinda. Mtu huyo mara nyingi  anajidanganya na  siyo rafiki, ni mshiriki na mlinzi, lakini pia mpinzani na adui.  Je ni kwanini? Hiyo ni kwa sababu mtu anayeishi kimwili amejaa tamaa za kimwili, anatamani vitu vya wengine na mwanamke wa wengine. Katika hali hii, Mungu anajionesha kama mwenye kufunga njia zake na walio wake: na kumwekea vizingiti kama vile “lazima wewe”…, au“hupaswi wewe”.... Na wakati huo huo, dhambi huamsha ndani ya moyo wa mwanadamu kuwa na chuki kali dhidi ya Mungu, na kwa uhakika kwamba, kama nafsi yake ingekuwa inamtegemea yeye nafasi hiyo, angependa Mungu asiwepo kabisa.

Utakaso ni kama unyoofu wa nia njema, hivyo  hepuka kuishi kinafiki

Pamoja na kufafanua hayo, ni jambo la utakaso kama unyoofu wa nia ambamo  Padre Cantalamessa amependa kusisitizia zaidi katika fursa hii kwa sababu ni kipindi cha Kwaresima ambacho kimeanza hivi karibuni na ambacho kinapendekeza na na  maonyo mengi kutoka kwa Yesu. “Basi wewe utoapo sadaka, usipige tarumbeta mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo”… kadhalika, “mnaposali msifanane na wanafiki”. … Padre Cantalamesaa anathibitisha kwamba hii kwa hakika inashangaza dhambi ya unafiki ambayo imeweza kutangazwa na kukemwa mara nyingi na Yesu katika Injili; na kwa hakika ni tabia ambayo mara nyingi  inaingia kidogo katika nafsi zetu kwa kawaida. Aidha anabainisha kuwa, japokuwa unafiki katika sehemu kubwa inaonesha kushinda, na ambayo kwa hakika unajulikana wazi. Kwa njia hiyo ni muhimu sana kutambua na kujua vema kuwa kila mmoja wetu ni kama anaishi na aina mbili hizi za maisha. Ya kwanza iliyo ya  kweli; ya pili ni ile ya  kufikirika, ikiwa na maana ya kuwa kile ambacho sisi ni nani kwa dhati, au nyingine kwa kile ambacho wengine wanafikiria juu yetu. Ni kwa jinsi gani sehemu hii ya pili inachukua nafasi katika maisha! Anasisitiza Padre Canatalamessa!

Dawa mbadala dhidi ya unafiki ni sali, funga na toa sadaka kwa siri, Bwana atakujaza dhawabu

Kristo anahukumu kwa kutumia maneno yenye ukali, kuhusiana na unafiki, hata hivyo, Padre Cantalamessa  anakiri kuwa si rahisi kuushinda, kwani, “hatuwezi kuepuka hisia za kuhisi tamaa za kuonekana wema katika nuru, kufanya watu wawe na hisia nzuri juu yako na kufurahisha wengine”. Ni muhimu kila siku kutumia silaha kama hiyo ya kurekebisha nia zetu. Kwa sababu wakati mwingine ni nia ya utashi wa mema na siyo hisia ya asili, ambayo inaleta utofauti machoni pa Mungu. Na inaonyesha mtazamo sahihi. Iwapo unafiki unajumuisha kuonesha hata mema  yasiyo fanyika, dawa mbadala ni ile ya  kupinga tabia hii na kuficha,  hata wema unaofanyika. Kwa hakikana hata  Yesu anapendekeza kwa haraka zoezi hili kwamba: “Sali  kwa siri, funga kwa siri, toa sadaka za siri, na Baba yako, ambaye anaona katika siri, atakupa thawabu. Padre Cantalesssa anaongeza kusema na hii siyo  suala la kufanya kuwa sheria maalum iliyowekwa bali ni kama wajibu . Yesu pia anasema:“Basi nuru yenu ingaze mbele ya wanadamu, na ili wapate kuona matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni" (Mt 5:16). Japokuwa ni suala la kutofautisha iwapo ni vema wengine kuona na wakati ni vizuri wao wasione anashuri Padre Cantalamessa

Kuwa na jicho rahisi kwa maana Mungu ni rahisi na ndiyo ushindi wa safari

Kuna jambo jingine ambalo Mungu anataka kukisisitizia zadia katika maisha ya mwanadamu na  ambalo ni  kinyume na unafiki, suala la kuwa ba  urahisi ambao hauna maana ya kuwa mpumbavu au kuwa mtu wa kijuujuu. Badala anasema:urahisi ni kupima wema unaotendeka kwa wengine; ni kuishi katika uwazi na katika ukweli, ni kutokuwa na hofu ya mwanga wa jua. Fadhila za kuwa na urahisi zina mitindo ya hali ya juu ambayo inaweza kufikiria hata Mungu mwenyewe. Katika Biblia na maandiko ya watakatifu, tunakutana na maneno yanayo tazama Mungu Na maneno hayo ni ujazo, unyofu, utimilifu na usawa kabisa. Kwa upande wa Padre Cantalamessa anabainisha kuwa na urahisi ndiyo ambao ni ushindi mkubwa zaidi na ndiyo safari nzuri kabisa ya kiroho, hivyo ni vema kuwa na jitihada kwa ajili yake.

Soma na kujilinganisha na zaburi ya 139 maana inakuweka wazi machoni pa Bwana

Mwisho wa kutafakari Padre Cantalamessa anashauri kusoma Zaburi 139 na kusema: iwapo unafiki na kuwa na njia mbili zinazo sababishwa na kutafuta mitazamo wa watu zaidi ya ule wa Mungu, hapa tunaweza kupata tiba mbadala zaidi. Kusali zaburi hiyo ni kama kwenda hospitali kwa namna moja kupiga picha ya mionzi na kusema: “ Ee Bwana umenichunguza kabisa, nawe unanijua. Wewe mwenyewe umepata kujua kuketi kwangu na kusimama kwangu. Umeichunguza fikira yangu tokea mbali. Umepima kusafiri kwangu na kulala kwangu nikiwa nimejinyoosha, Nawe umezijua njia zangu zote”. (Zab 139).

Jambo la kushangaza katika zaburi hii Padre Cantalamessa anasema ni kuwa na umakini katika dhamiri kwa maana ya  kupitiwa na mtazamo wa Mungu ambao haukupatii hisia za aibu au hofu, au hukumu, kama vile kuhisi unatazamwa na kugunduliwa katika mawazo yako sirini; kinyume chake ni kukupatia furaha kwa sababu ya kuhisi kuwa huo ni mtazamo wa  Baba au wa mama anayependa kukusafisha anayetaka uwe mkamilifu niwe kama yeye alivyo mkamilifu.

Wazo la mwisho ni ushauri wa kusali zaburi hii na kuifanya iwe ya kwako

Padre Cantalamessa akitazama jinsi zaburi inavyomalizika amewaomba wawe na mazoea ya kusali na kuifanya kama ya kwao: “tazama Mungu na kujua moyo wangu, nijaribu na kuona mawazo yangu, tazama kama ninapitia njia za ulaghai na nielekeza katika njia ya maisha. Kwa maana hamna neno hata moja katika ulimi wangu, lakini, tazama! Ee Mungu, tayari unajua yote. Nyuma na mbele umenizingira; Nawe unauweka mkono wako juu yangu. Ujuzi wa namna hiyo ni wa ajabu mno kwangu. Ni wa juu sana hivi kwamba siwezi kuufikia. Ni wapi ninapoweza kwenda mbali na roho yako. Na ni wapi ninapoweza kukimbilia mbali na uso wako?  Kama ningepanda mbinguni, ungekuwa huko; Na kama ningetandika kitanda changu katika Kaburi, tazama! ungekuwa huko”.

 

15 March 2019, 14:47