Tafuta

Kardinali Sandri alikuwa akisubiliwa na kwa shangwe kuu na  Kiongozi mkuu Patriaki Tawadros II katika  lango Kuu la Monasteri ya Mtakatifu Bishoy nchini Misri Kardinali Sandri alikuwa akisubiliwa na kwa shangwe kuu na Kiongozi mkuu Patriaki Tawadros II katika lango Kuu la Monasteri ya Mtakatifu Bishoy nchini Misri 

Misri:Kardinali Sandri aitembelea Monasteri ya Mt.Bishoy

Kardinali Sandri alitembelea Monasteri ya Mtakatifu Bishoy nchini Misri tarehe 2 Machi 2019 ambapo Patriaki Tawadros II amepokelea wageni wake kwa kuwasubiri mbele ya mlango wa kuingilia na kuwakumbatia kwa shangwe kindugu.Wakiwa pamoja,amemzungusha na kumwonesha nafasi zote za jengo hilo pamoja na maktaba ampya ambayo imezinduliwa

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Baada ya Misa Takatifu aliyoadhimisha katika Kanisa dogo la Ubalozi wa Vatican, Cardinali Leonardi Sandri Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki, ambaye amekuwa ziarani katika mji wa Cairo nchini Misri  kama mjumbe maalumu wa Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya kutimiza miaka 800 tangu mkutano wa Mtakatifu Francis wa Asisi na Sultani Al-Kamil huko Damietta, Jumamosi tarehe 2 Machi 2019 kwa kusikindikizwa na Balozi wa Vatican, Askofu Mkuu Bruno Musarò, katibu wa Balozi, Padre Jan Thomas Limchue na Msaidizi wa Upatriaki Hani Bakoum walikwenda katika Monasteri ya Mtakatifu Bishoy, karibu na barabara inayounganisha Cairo na Alessandria. Ni Monasteri ambayo alikuwa mmonaki na alikaa kila wiki Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox Tawadros II kiongozi mkuu wa Alesandria na Patriaki Mkuu wa Mtakatifu Marko.

Kardinali Sandri alikuwa ametembelea Monasteri hiyo kunako Januari 2013 wakati Mkuu wa Kanisa hili alikuwa amechanguliwa punde na tangu wakati huo wakajenga Monasteri mpya mahali ambapo Patriaki amepokelea wageni wake kwa  kuwasubiri mbele ya mlango wa kuingilia na kuwakumbatia kwa shangwe kindugu. Wakiwa pamoja, Patrika Tawadros II, amemzungusha na kumwonesha nafasi zote za jengo hilo pamoja na maktaba ampya ambayo imezinduliwa hivi karibuni. Baada ya kuingia katika jengo sehemu ya kwanza kufikia ilikuwa ni Kanisa dogo mahali ambapo Kardinali Sandri amependa kusali sala ya Baba Yetu kwa nia za kiongozi mkuu huyo na baadaye wamekwenda kutembelea ukumbi  mkubwa wenye uwezo wa kukaa watu 500, kwa sasa unatumika katika mafunzo ya kudumu kwa makundi ya mapadre, mamonaki na walei wanapomtembelea Patriaki. Aidha ametembelea jumba dogo la makumbusho mahali ambapo linapokea zawadi na ushuhuda kutoka katika makanisa na watu wa karibu na mbali kutoka duniani.

Wakiwa katika ukumbi mdogo, wameanza mazungumoz ambapo kwa upande wa Kardinali Sandri ameonesha sababu ya ziara yake na kuelezea vituo mbalimbali alivyotembelea katika majimbo ya Misri na kuwapongeza  kwa uwepo wao katika kila sehemu ambapo walikuwapo maaskofu au mapadre wa kikoptiki -kiorthodox, hadi kukumbuka maadhimisho ya tarehe 1 Machi 2019 huko Damietta  katika kumbukumbu ya miaka 800 tangu Mtakatifu Francisko wa Assisi kukutane na Sultani Ali –Malik. Hata hivyo kumbukumbu hiyo imemrudisha Kardinali Sandri katika kipindi ambacho alikuwa shuhuda wa kumsindikiza Baba Mtakatifu Francisko katika Ziara yake ya Kitume ya hivi karibuni huko Abu Dhabi na kusahiniwa kwa hati juu ya undugu ambapo amewatakia matashi mema ya matumaini na upyaisho katika mahusiano kati ya wakristo na waislam na zaidi kwa ujumla namna ya mtindo mpya wa kushirikiana kati ya dini kwa ajili ya amani na upatanisho wa watu duniani.

Kardinali Sandri vile vile hakukosa kutaja hata baadhi ya matatizo ambayo hadi sasa yameweza kuoneshwa  ndani ya mazungumzo na mapadre wa kikoptiki katoliki katika mahusiano yao na jumuiya ya kiorthodox, lakini wamesema ni uhakika kwamba mchakato wa safari umekwisha anza, pamoja na utambuzi wa matatizo ambayo kwa vyovyote hayawezi kuzuilika, muhimu watambue kutazama upeo kwa ajili ya kufikia hatua mpya katika mahusiano kwenye makanisa tofauti. Katika mazungumzo aidha wameonesha lazima wa kuwa na uvulimivu ambao kwa takwimu chanya kwa miaka hii imeonesha matokeo mazuri katika mihimili yote ya makanisa, pia kama ilivyo hata kwa kila familia amethibitisha  haiwezi kukosa kutoelewana na ugumu, japokuwa hizi ni njia za kuweza kurudisha na kudumisha  uhusiano asili ambao daima ni ushindi. Kardinali Sandri ameonesha kwa masikitiko na uchungu  juu ya waathirika wa nguvu kwa namna ya pekee wale kwa miaka ya hivi karibuni ndani ya Kanisa la Kikoptiki, kutokana na mashambulizi ya kigaidi, hadi yale ya  ndani ya Kanisa ,wakati wa maadhimisho ya kiliturujia; kwa maana hiyo amewakilisha salam zake kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko.

Kadhalika baada ya mazungumzo ya Kardinali Sandri, hata Kiongozi Mkuu wa Alessandria Tawadros II amekumbusha kuguswa sana na uzoefu wa kuwapokea Askofu wa Milano Italia, akiwa na mapadre vijana 130 waliotaka  kushirikishana nao uoefu wa siku za mikutano na  ushuhuda wao katika makao makuu ya upatriaki kwenye mji wa Cairo. Aidha kumbukumbu ya Mkutano huko Bari mwaka jana tarehe 7 Julai kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko na mapatriaki wote katoliki na siyo wa nchi za Mashariki ili kusali kwa pamoja na kuweza kukabiliana kwa pamoja mantiki ambayo ilipokelewa kwa utulivu mkubwa na kwamba ni matumaini na matashi mema  kwamba kuwa suala hili lisibaki kuwa tupu, bali linaweza kurudiwa kwa mara nyingine tana katika kutoa mchango wa kuishi kwa pamoja na amani.

Aidha amejikita kuelezea sura ya ncha nne za msalaba kwa ajili ya kuelezea shughuli za kiekumene ambazo lazima zianzie katika mkutano na kukuza urafiki wa dhati, baadaye kupitia katika mafunzo ya vyanzo kwa pande zote za kiutamaduni. Mazungumzo mbayo yanapaswa kujikita katika hatua hizi mbili ili hatimaye kuweza kulinda sala na ili wote katika mantiki ambazo ziongozwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo katika mazungumzo ya Patriaki wa Kikoptiki - Kirothodox amekumbusha watu wa Misri mbali na dini tofauti ya muda mrefu wa historia, lakini hata uwepo wa muungano kwa  utambuzi kwamba Mto Nile ni kama Baba wa kuishi na ardhi ambayo imenyeshewa na mama. Uwepo wa kina ni wema kwa wote na matendo ya kigaidi dhidi ya Kanisa, zaidi kutesa dini ni sababu za sera za kisiasa ambazo zinataka kugawanya jumuiya na watu ambao wanahisi na kutaka kuwa wamoja.

Baada ya kipindi cha kwanza Patriaki mwenyewe alimsindikiza uwakilishi katika Maktaba ambapo Patriaki Tawadros II amesema alihisi furaha kwa sababu ni nafasi ambayo imezinduliwa hivi karibuni na kwa mara ya kwanza inatembelewa na Kardinali wa Kanisa katoliki, hivyo ameelezea shauku yake kuwa wanaweza kupokea watu wengi ambao wanaweza kutajirisha  ufahamu na mafunzo ya kisayansi.  Na wakati huo huo Kardinali Sandri ametoa ahadi ya kuweza kuleta hata toleo za vitabu vya  kingereza na kiitaliano ambavyo vitakabidhiwa kuchapichwa na Kampuni ya uchapisha katoliki huko mashariki, kama vile  machapisho mengine yenye kuhaririwa na Baraza la Kipapa la Taasisi za Mashariki.

Uwakilishi umeshangazwa sana na mapokezi ya Patriaki hadi kusimama na kukaa kula chakula cha mchana nao. Kipindi ambacho kilikuwa rahisi na kuendelee na maongezi kuhusiana na mada nyingine kwa namna ya pekee juu ya hali halisi ya Umonaki, juu ya miito na juu ya ngazi halisi ya mafunzo ya kibinadamu na nidhamu kwa kizazi cha vijana ambao pia wanajiunga na Monasteri au wanapewa daraja la upadre.

05 March 2019, 13:52