Cerca

Vatican News
Mafungo ya kiroho Ariccia kwa Baba Mtakatifu na waandamiziwake  yanaendelea Mafungo ya kiroho Ariccia kwa Baba Mtakatifu na waandamizi wake yanaendelea  (ANSA)

Mafungo ya kiroho:Umuhimu wa tamaa ya kufunguliwa fumbo la Mungu!

Ikiwa ni Tafakari ya tano asubuhi tarehe 13 Mach 2019 kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu,katika nyumba ya mafungo huko Ariccia nje ya mji wa Roma, Abate Maria Gianni amejikita kusisitizia juu ya kiini cha mategemeo ya shauku ambazo zinamfungulia mtu katika fumbo la Mungu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tamaa kali ndiyo pendekezo la tema ya Abate Bernardo Francesco Maria Gianni katika tafakari ya asubuhi ya Jumatano 13 Machi 2019  kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu, katika nyumba ya mafungo huko Ariccia nje ya mji wa Roma. Kama ilivyo kwa siku nyingine kuongozwa na shairi la Mario Luzi mahali anapozungumza juu ya shauku za kuweza kushinda kila ina ya mtindo wa ubinafsi, na ili kuweza kuelekeza katika uso na moyo wa Mungu. Kwa kufanya hivyo ni kuwa baadaye mashuhuda waaminifu katika njia ambazo wote wanaalikwa kuwa wamisionari wa  undugu ambao unabadili namna ya kujifungia binafsi na ili kushuhudia,kushirikishana upendo ambao tumepokea kutoka kwa Bwana. Kwa upande huo Abate Maria Gianni anatazama kwa namna ya pekee Kanisa na kwa ajili ya jumuiya nzima ambayo wanafanya uzoefu wa mafungo ya kiroho, kwamba waweze kweli kurudi katika uwajibikaji wao binafsi kama nyota ya nabii Baruku ambaye alikuwa atajwe kesho yake. Nyota ya nguvu inayo ongaza usiku kutoka katika Shairi la Maria Luzi. Nyota zinazoangaza zinafanane na furaha yao ili kuweza kurudia kusema tazama mimi hapa mbele ya Bwana na  ili wawe vimondo, mwanga na mwelekeo katika usiku wa ubinadamu.

Mtakatifu Benedikto na tamaa za Mungu

Akiendelea na tafakari yake Abate Maria Ginni anataja Kanuni ya Mtakatifu Benedikto ambaye anafungua matarajio ya shauku na kusimulia kwamba: shauku za Mungu zinazotamaniwa, ndizo shauku ambazo zinamsukuma Mungu katika mzunguko huo aliyeshuka toka juu ili kutazama kama kuna mtu anayetamani kuona siku za furaha. Abate anathibitisha kuwa, hii ni sehemu nzuri sana wa hakika inatuweka katika hali ya kujigundua kuwa tumetafutwa na kutamaniwa na Bwana. Ni uzoefu katika hali halisi na ambayo si tu kwa wamonaki,bali kwa ubinadamu wote, hata kama mmoja anaweza kusema  asante kwa namna ambavyo sisi ni mashuhuda waaminifu wa shauku ya Mungu kulingana na moyo wa kila mwanaume na mwanamke wa nyakati zetu. Shauku kwa maana nyingine ni kujigundua hatimaye kuwa tunatamaniwa na Bwana. Hii Abate anaitaja kwamba ni aina ya wehu wa Mungu, lakini ambao unapelekea kujivua nafsi yake katika kuwa na  shauku za mtu (...). hii ina maana kwamba, Bwana anapotea kwa sababu ya kumtafuta mtu aliyepotea! Hii inajionesha katika picha ya Mchungaji mwema ambaye anatajwa na Mtatifu Yohane katika Barua yake ya kwanza. Yeye anasema kuwa  huo ndiyo upendo. Siyo sisi tulio mchagua Mungu, bali ni yeye aliyetupenda na kumtuma Mwanaye kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi zetu. Na iwapo sisi tunaweza kuendelea na tamaa hiyo ni kwasababu tumetamaniwa kwanza. Ndiyo utambuzi ambao unaweza kushinda kila aina ya ubaridi wa kiroho ambao tunakutana nao leo hii na zaidi, amethibitisha Abate Maria Gianni.

Katika nyakati zetu uwezo wa kutamani umepotea

Katika nyakati hizi uwezo wa kutamani umepotea  anabainishaAbate Maria Gianni.  Leo hii kumeenea hisia za kufikiria:sina haja ya kitu chochote,mimi ni tajiri. Katika dunia ya leo kwa namna ya pekee anatoa mfano wa jamii ya  Italia na hasa kwa upande wa vijana ambao wanaishi uzoefu wa kukinai kila shauku na tamaa za mambo mengi ya kuduma na muhimu. kwa kuonesha  uhakika anataja ripoti ya 44 ya Takwimu za watu wa Italia,inaonesha  ni jamii iliyoko hatarini  ambayo inakabiliwa na utupu kwa mtamzamo wa mzunguko kihistoria ulio jaa na kutafuta mafao binafsi, migogoro kijamii. Miaka ya sitini na sabini  na kipimo kidogo cha miaka ya 80-90 imeonesha pia mzunguko wa kubatilisha na uwepo wa kutafuta mafao binafsi na migogoro ya ndani. Kutokana na uthibitisho huo, Abate Maria Gianni anasema kuna haja ya kutoa chachu ili  kurudi kutamani nahasa inahitajika fadhila ya kiraia na  lazima kwa ajili ya kupyaisha jamii ambayo kwa bahati mbaya imesimama.

Kuelimisha vijana wapanue mitazamo yao

Abate Maria Gianni akindelea tafakari bado anatazama vijana na kutaja moja ya maandishi ya Padre Luigi Giusani ambaye alikuwa anasema kwamba utafikri wao hawapo katika wakati uliopo na kama vile hawajafikia dhamiri ya kujitegemea, ikiwa na maana ya kwamba wana hisia kuwa hawapendwi. Na akitoa mfano wa vijana katika sehemu anayoishi ya Mtakatifu Miniato amethibitisha juu ya ukosefu huo wa utambuzi kwa walio wengi na ulazima wa kujikita katika kambi za elimu na kuthubutu katika na siyo katia mchzo wa maisha hasa katika mwendelezo wa upendo na kuwekezwa kwao kwa uvumilivu  lakini ambao ni kinyume na vijana hao kutokana na kuedekezwa sana na wazazi wao. Kwa maana hiyo anasisitiza juu ya kuwafungulia milango mpanana na siyo finyu ya kuweza kuwakomboa ili watamani yaliyo mema na yenye kuleta wakati endelevu wa maisha yao. Zoezi lenye thamani kwao anathibitisha ni ile ya kupanua mipaka kwa ajili ya upeo kwa kizazi kipya. Katika hili anapendekeza moja ya maneno kutoka kwa Mama wa Mtaguso wa II wa  Gaudium et spes usemo: Inawezekana kufikiria kisheria kuwa wakati endelevu wa binadamu upo katika mikono ya wale wenye uwezo wa kuonesha maisha na  matumanini kwa vijana wa kesho. Na ndiyo sasa mwaliko wa Kanisa katika tamaa kali za kazi za mji,  tamaa kali katika dunia ya sasa, tamaa kali kwa kuamsha haraka iwezekanavyo,  tamaa kali za Mungu kwa wale ambao tunakutana nao na  kuwakumbusha wao neema na fumbo ya kuwa wametamaniwa japokuwa na uwepo wa dharura, mabonde , na magumu ambayo labda walikutana nayo wakati wakiwa wadogo.

Hitimisho la shukrani kwa zawadi ya  Baba Mtakatifu Francisko

Leo hii ni mwaka wa sita tangu kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu na hivyo Abate Maria Gianni wazo wale limemwendea kutoa shukrani kwa Bwana kwa zawadi hiyo na kuthibitisha kwa dhati Baba Mtakatifu anatufundisha kutokushindwa, lakini zaidi analika kwa nguvu za Roho Matakatifu kushinda vizingiti hivyo kwani moyao wa mtu hauna mipaka. Hayo yote anatukumbusha kila siku kwa imani na uaminifu wa Injili.

14 March 2019, 12:48