Mafungo ya Kiroho:Kwaresima ni kipindi cha kuacha Mungu akarabati uzuri wetu!
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Katika moyo wa tafakari ya subuhi Jumanne 12 Machi 2019 Anbate Bernardo Fancisko Maria Gianni anawaalika Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu watafakari juu ya sintofahamu, na vinyago vya kujifunika machoni ambavyo vinazuia usijali au kuwatazama wengine, vilevile uwajibikaji wa hali halisi, katika kisimika mizizi ya kwenye mji ili kutafuta uuri na vipimoa ambavyo hivyo vinatambuliwe na walio wengi ambao wamependwa na Mungu, aidha kutambua hata sisi sotw kwa namna ya kumpenda Mungu. Mada ya tafakari ya asubuhi waliogozwa na ubaya wa sasa, wa damu na sintofahamu katika kudadavuliwa kutoka shairi la Mario Luzi lenye kichwa cha “ Furaha zilizotibuliwa ni katika shiiri ambalo linajikita kutazama Monasteri ya Firenze kunako mwaka Desemba 1997 mahali ambapo Abate Maria Gianni anaishi.
Kutazama majeraha ya miji, hali halis ambayo inatazama wazo
Abate akifafanua juu ya shairi hili anasema, mtunzi Luzi alipoandika machoni mwake alikuwa na hali halisi ya janga la kimafya lililokuwa limetokea miaka minne iliyopita na kusasabisha mauaji wa waathirika wanne wasio kuwa na hatia na uharibifu mkubwa wa sehemu moja yenye thamani ya kisanaa ya mji wao. Katika janga hilo, anathibitisha, wote wanaalikwa kutazama ni kwa jinsi gani kumekuwapo daima na jitihada za kutuliza majeraha ya miji katika dunia yote, hata majeraha magumu zaidi, ambayo yanasababishwa na ukosefu wa usawa wa kila aina katika sayari nzima. Aidha anatoa mfano wa jinsi gani Baba Mtakatifu Francisko amewafundisha kuheshimu na kujali juu ya wazo la majeraha hayo.
Sintofahamu, vinyago binafsi vya kujilinda na wengine
Akiendelea na tafakari yake amejikita kueleza ishara tatu za ubaya katika sayari hii , kwamba ni sintofahamu ambayo inakwenda kinyume na upendo, kwa mujibu wa shairi la Luzi,na matendo ya kisiasa ya Giorgio La Pira aliyekuwa ni Meya wa Mji. Sintofahamu ambazo mara nyingi kwa namna ya kichini chini inagandisha mioyo yetu na kutufanya mitazamo yetu iwe na kivuli au ukungu. Ni ukungu ambao Charles Taylor alikuwa akiuita kama kinyago nafsi. (Ikiumbukwe Charles Taylor (Montréal, 5 Novemba 1931) ni mwanafalsa wa Canada ambaye alijihusisha hasa na falsafa ya kisiasa na falsafa ya kisayansi. Na kwa maana hiyo anaongeza kusema ni kama kwamba utu wetu unavaa moja ya ngao ya kujilinda dhidi ya wengine, hasa katika mtazamo wa ule uwajibikaji ambao ni matatizo makubwa ya wakati wetu. Na badala yake ni kutafuta kuvaa mwanga ule ambao unatokana na shauku ya kiinjili ambayo Bwana anataka kuwasha kwa nguvu za Roho Mtakatatifu wake katika mioyo yetu.
Kutazama hali halisi bila kuota ndoto za mawazo ya mji
Akimtaja mtaalimungu wa Kiluteri, Dietrich Bonhoeffer na dukuduku zake juu ya maisha ya kizazi kijacho, bate Gianni anathibitisha kuwa lazima kuweka suala hili moyoni la kuwa na uwezekano wa kuwaachia kizazi kipya na endelevu wakati ulio bora kuanzia wa sasa ambamo tunaishi, kwa kuwakabidhi tukiwa na roho inayopinga utofauti, lakini kila kitu kiwe na msukumo wa ushiriki hai kabisa. Hata hivyo mwandishi mwingine Romano Guardini aliyekuwa ametaja katika tafakari zilioanza, alikuwa anawaalika wapokee kwa dhati uwajibikaji ambao ndiyo mkuu katika wakati ujao ili kuweza kutiumiza ikiwezekana na Bwana.. Kipeo cha hali nzuri ya serikali na watu cha kuwazika tu, si matarajio ya dhati ya kiinjili anathibtisha kwani Yerusalemu ya mbingu ndiyo muono wa Ufunuo kwa maana ni kutakari kwa dhati na siyo wazo tu, badala yake ni ahadi halisi, inayoaminika na ambayo Bwana alikabidhi kwa Kanisa lake kama jaribio.
Matendo ya Kanisa kwa namna hiyo kwa wanaume na wanawake wenye mapenzi mema ndiyo kweli matunda yanayotokana na kusikiliza kwa utiii na kwa shauku ya Injili ya Maisha ya Yesu. Na kwa mujibu wa Abate anasema shairi la Luzi linaonesha wazi utambuzi wa utamaduni wa sasa na moto wa watakatifu wa kale. Ni zile cheche na utakatifu ambao kwa sasa unaweza kurudia kuwa kweli na kuwasha mwanga wa matumaini katika giza nene la mji wa dunia yetu. Kwa kushinda vishawishi vya sintofahamu,vinyago binafsi na kusimiaka mizizi ambayo inawakumba hata watu wa Kanisa, ni kuhisi wito hasa wa kuwa kiungo hai na mtoleo yake, ambayo ni migongano katika njia kwa maana hiyo wote wanaalikwa kuishi kwa gharama zozote zile , Neno la Mungu ambao limekuja kwetu. Hilo ndilo pendekezo lake yaani nni dawa ya uzito na kipimo cha ukuu na kwa pamoja wanaweza kuzuia ule ubinafsi wa kila aina na kuwa mashuhuda wakubwa wa Kanisa ambao hauwezi kukosa na kuwa mzizi mkuu wa kidugu.
Mtakatifu Agostino kumpend mungu na kugeuka kuwa wazuri
Aidha akiendelea na tafakari yake anasema Mtakatifu Agostino wakati wa kutafakari Barua ya kwanza ya Mtakatifu Yohane, anakumbusha ni uzuri gani wa kweli tutakuwa nao kwa ajili ya Kupenda iwapo yeye ametupenda akiwa wa kwanza? Kwa kupenda, tumekuwa marafiki, lakini yeye alitupenda sisi wakati tukiwa maadui zake ili tuweze kuwa marafiki. Na kwa upya, Mungu ametupenda, ametutengeneza, ametupamba na uzuri wake. Alitupenda akiwa wa kwanza na kutupatia uwezo wa kumpenda!
Kuzungumzia uzuri kwa vijana ndiyo moja ya kipimo cha njia ya kujikubali na kukubali wegine
Katika dunia ambayo inapendelea sana maisha ya kijuu juu tu, uzuri wa ndiyo moja ya kipimo ambacho vijana wanakubali na wanawakubali vijana wengine. Kwa maana hiyo ni kurudi katika wazo la Mtakatifu Agostino: roho zetu ni mbaya kwa sababu ya dhambi; na hiyo inakuwa nzuri kwa kumpenda Mungu. Je ni kwa namna gani tutakuwa wazuri? Kwa kumpenda Yeye tutakuwa daima wazuri. Kadri upendo huo utakavyokua ndani mwako ndivyo hata uzuri zaidi z wa roho utazidi kuongezeka. Hivyo Mtakatifu Agostino alitambua kwa dhati ni jinsi gani Bwana Yesu pamoja na kutupatia uzuri huo, yeye alijifanya mbaya na alifanya hivyo kuonekana Msalabani na kukubali i hata kuhusishwa mwili wake.