Cerca

Vatican News
Mafungo ya kiroho huko Ariccia nje ya Mji wa Roma kwa Baba Mtakatifu na waandamizi wake wa karibu Mafungo ya kiroho huno Ariccia nje ya Mji wa Roma kwa Baba Mtakatifu na waandamizi wake wa karibu 

Mafungo ya Kiroho:Kwaresima ni kipindi cha kuacha Mungu akarabati uzuri wetu!

Katika tafakari ya tatu ya asubuhi tarehe 12 Machi 2019 iliyotolewa kwa Baba Mtakatifu na waandamizi wake wa karibu kwenye mafungo ya kiroho huko Ariccia,Abate Maria Gianni akitumia mshairi Luzi anawaalika watafakari sintofahamu,ambao ni magonjwa ya miji yetu na sura ya La Pira aliyekuwa Meya wa mji ili kusimika mizizi ya maisha katika miji

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika moyo wa tafakari ya subuhi Jumanne 12 Machi 2019 Anbate Bernardo Fancisko Maria Gianni anawaalika  Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu watafakari juu ya sintofahamu, na vinyago vya kujifunika machoni ambavyo vinazuia usijali au kuwatazama wengine, vilevile  uwajibikaji wa hali halisi, katika  kisimika mizizi ya kwenye  mji ili kutafuta uuri na vipimoa ambavyo hivyo vinatambuliwe na walio wengi ambao wamependwa na Mungu, aidha kutambua hata sisi sotw kwa namna ya kumpenda Mungu. Mada ya tafakari ya asubuhi waliogozwa na ubaya wa sasa, wa damu na sintofahamu  katika kudadavuliwa kutoka shairi la Mario Luzi  lenye kichwa cha “ Furaha zilizotibuliwa ni katika shiiri ambalo linajikita kutazama Monasteri  ya Firenze kunako mwaka Desemba 1997 mahali ambapo Abate Maria Gianni anaishi.

Kutazama majeraha ya miji, hali halis ambayo inatazama wazo

Abate akifafanua juu ya shairi hili anasema, mtunzi Luzi alipoandika machoni mwake alikuwa na hali halisi ya janga la kimafya lililokuwa limetokea miaka minne iliyopita na kusasabisha mauaji wa waathirika wanne wasio kuwa na hatia na uharibifu mkubwa wa  sehemu moja yenye thamani ya kisanaa ya mji wao. Katika janga hilo, anathibitisha, wote wanaalikwa kutazama ni kwa jinsi gani kumekuwapo  daima na jitihada za kutuliza majeraha ya miji katika dunia yote, hata majeraha magumu zaidi, ambayo yanasababishwa na ukosefu wa usawa wa kila aina  katika sayari nzima. Aidha anatoa mfano wa jinsi gani Baba Mtakatifu Francisko amewafundisha kuheshimu na kujali  juu ya wazo la majeraha hayo.

Sintofahamu, vinyago binafsi vya kujilinda na wengine

Akiendelea na tafakari yake amejikita kueleza ishara tatu za ubaya katika sayari hii , kwamba ni sintofahamu ambayo inakwenda kinyume na upendo, kwa mujibu wa shairi la Luzi,na matendo ya kisiasa ya Giorgio La Pira aliyekuwa ni Meya wa Mji. Sintofahamu ambazo mara nyingi kwa namna ya kichini chini inagandisha mioyo yetu na kutufanya mitazamo yetu iwe na kivuli au ukungu.  Ni ukungu ambao Charles Taylor alikuwa akiuita kama kinyago nafsi. (Ikiumbukwe Charles Taylor (Montréal, 5 Novemba 1931)  ni mwanafalsa wa Canada ambaye alijihusisha hasa na falsafa ya kisiasa na falsafa ya kisayansi. Na kwa maana hiyo anaongeza kusema ni  kama  kwamba utu wetu unavaa moja ya ngao ya kujilinda dhidi ya wengine, hasa katika mtazamo wa ule uwajibikaji ambao ni matatizo makubwa ya wakati wetu. Na badala yake ni kutafuta kuvaa  mwanga ule ambao unatokana na shauku  ya kiinjili ambayo Bwana anataka kuwasha kwa nguvu za Roho Mtakatatifu wake katika mioyo yetu.

Kutazama hali halisi bila kuota ndoto za mawazo ya mji

Akimtaja mtaalimungu wa Kiluteri, Dietrich Bonhoeffer na dukuduku zake juu ya maisha ya kizazi kijacho, bate Gianni anathibitisha kuwa lazima kuweka suala hili moyoni la kuwa na uwezekano wa kuwaachia kizazi kipya na  endelevu  wakati ulio bora kuanzia wa sasa ambamo tunaishi, kwa kuwakabidhi tukiwa na roho inayopinga utofauti, lakini kila kitu kiwe na msukumo wa ushiriki hai kabisa. Hata hivyo mwandishi mwingine  Romano Guardini aliyekuwa ametaja katika tafakari zilioanza, alikuwa anawaalika wapokee kwa dhati uwajibikaji ambao ndiyo mkuu katika wakati ujao ili kuweza kutiumiza ikiwezekana na Bwana.. Kipeo cha hali nzuri ya serikali na watu cha kuwazika tu, si matarajio ya dhati ya kiinjili anathibtisha kwani  Yerusalemu ya mbingu  ndiyo muono wa Ufunuo kwa maana ni kutakari kwa dhati na siyo wazo tu, badala yake ni ahadi halisi, inayoaminika na ambayo Bwana alikabidhi kwa Kanisa lake kama jaribio.

Matendo ya Kanisa kwa namna hiyo kwa wanaume na wanawake wenye mapenzi mema ndiyo kweli matunda yanayotokana na kusikiliza kwa utiii na kwa shauku ya Injili ya Maisha ya Yesu. Na kwa mujibu wa Abate anasema shairi la Luzi linaonesha wazi  utambuzi wa utamaduni wa sasa na moto wa watakatifu wa kale. Ni zile cheche na utakatifu ambao kwa sasa unaweza kurudia kuwa kweli na kuwasha mwanga wa matumaini katika giza nene la mji wa dunia yetu. Kwa kushinda vishawishi vya sintofahamu,vinyago binafsi na kusimiaka mizizi ambayo inawakumba hata watu wa Kanisa, ni kuhisi wito hasa wa kuwa kiungo hai na mtoleo yake, ambayo ni migongano   katika njia kwa maana hiyo wote wanaalikwa kuishi kwa gharama zozote zile , Neno la Mungu ambao limekuja kwetu. Hilo ndilo pendekezo lake yaani nni dawa ya uzito na kipimo cha ukuu na kwa pamoja wanaweza kuzuia ule ubinafsi wa kila aina na kuwa mashuhuda wakubwa wa Kanisa ambao hauwezi  kukosa na kuwa mzizi mkuu wa kidugu.

Mtakatifu Agostino kumpend mungu na kugeuka kuwa wazuri

Aidha akiendelea na tafakari yake anasema Mtakatifu Agostino wakati wa kutafakari Barua ya kwanza ya Mtakatifu Yohane, anakumbusha ni uzuri gani wa kweli tutakuwa nao kwa ajili ya Kupenda iwapo yeye ametupenda akiwa wa kwanza? Kwa kupenda, tumekuwa marafiki, lakini yeye alitupenda sisi wakati tukiwa maadui zake ili tuweze kuwa marafiki. Na kwa upya, Mungu ametupenda, ametutengeneza, ametupamba na uzuri wake. Alitupenda akiwa wa kwanza na kutupatia uwezo wa kumpenda!

Kuzungumzia uzuri kwa vijana ndiyo moja ya kipimo cha njia ya kujikubali na kukubali wegine

Katika dunia ambayo inapendelea sana maisha ya kijuu juu tu, uzuri wa ndiyo moja ya kipimo ambacho vijana wanakubali na wanawakubali vijana wengine. Kwa maana hiyo ni  kurudi katika wazo la Mtakatifu Agostino: roho zetu  ni mbaya kwa sababu ya dhambi; na hiyo inakuwa nzuri kwa kumpenda Mungu. Je ni kwa namna gani tutakuwa wazuri? Kwa kumpenda Yeye  tutakuwa daima wazuri. Kadri  upendo huo utakavyokua  ndani mwako ndivyo hata uzuri zaidi  z wa roho utazidi kuongezeka. Hivyo Mtakatifu Agostino alitambua kwa dhati ni jinsi gani Bwana Yesu pamoja na kutupatia uzuri huo, yeye alijifanya mbaya na alifanya  hivyo kuonekana Msalabani na kukubali  i hata kuhusishwa mwili wake.

13 March 2019, 13:34