Tafuta

Mafungo ya kiroho ya kwaresima kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu katika nyumba ya mafungo Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma Mafungo ya kiroho ya kwaresima kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu katika nyumba ya mafungo Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma 

Mafungo ya kiroho:Abate anakazia kuonesha uzuri wa kumbu kumbu!

Ikiwa ni Tafakari ya nne ya mchana tarehe 12 Machi 2019 katika mafungo ya kiroho ya Kwaresima inayotolewa na Abate Bernardo Francesco Maria Gianni kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu huko Ariccia,anawashauri watazame maisha kama kielelezo na siyo ubinafsi,bali kama ushuhuda wa huduma ya Neno la Mungu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika Tafakari ya nne mchana,Jamanne tarehe 12 Machi 2019  katika mafungo ya kiroho ya Kwaresima yanayotolewa na Abate Bernardo Francesco Maria Gianni  kwa Baba Mtakatifu Francisko na waandamizi wake wa karibu huko Ariccia,wameongozwa na mada ya Kumbu kumbu Abate Maria Gianni amesema ili kuweza  kujua mtu wa leo hii anavyoishi na uhusiano wake na wakati huu,ni muhimu kutumia maelezo ya mtaalam wa elimu ya kijamii kutoka ufaransa aitwaye Marc Augé ambapo kwa mujibu wake anasema, leo imeenea itikadi moja ya wakati. Wazo lake ni kuonesha kuwa, wakati uliopo siyo njia ya kuleta mabadiliko kutoka  wakati uliopita, wala kuacha utazame kile ambacho kimetayarishwa kwa  wakati ujao. Wakati uliopo ni enzi kuu lakini kumbu kumbu na matumaini anasitiza, ni mambo ambayo kwa dhati yamefifia katika wakati uliopo.

Ni vigumu kuwafanya kumbu kumbu

Mtaalam wa elimu kijamii Marc Marc Augé anahusisha kwa dhati udikteta wa kutokuwa na uhakika wa wakati uliopo na wakati huo huo ni uthibitisho wa maambukizo ya kweli kwa binadamu wa sasa, ambaye amezungukwa na teknolojia tawala. Katika enzi kuu  ya wakati wa sasa, anasema Abate Maria Gianni ni vigumu kufanya kumbu kumbu, ni vigumu kukumbuka na kuweka moyoni, hati kuwa makini na kushukuru yale matukio ya wakati uliopita. Ugumu wa kufanya kukumbuku anasisitiza ni ugumu wa kuvumulia ni ungumu wa kuvumilia kukaa katika wakati na katika historia. Hata hivyo Abate pia anatazama maneno  ya shairi ya Leuzi na matendo ya kisiasa ya Giorgio la Pia kwa kuelekeza njia za kumbukumbu ambazo zinapeleka njia kuelekea wakati endelevu.

Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi

Akiendelea kutafakari juu ya msingi wa ukuu wa kumbu kumbu, Abate Gianni Maria anakumbuka kwa namna ya pekee anavyo andika Baba Mtakatifu Francisko katika Hati ya Kitume ya Evangelii Gaudium. Katika hati hiyo inasema:” Kumbu Kumbu ni ukuu wa imani yetu ambao tunaweza kuuita yakutoka inayofanana na kumbukumbu ya wana wa Israeli. Yesu aliacha Ekaristi kama kumbu kumbu ya kila siku ya Kanisa, ambayo inatuingiza daima katika Pasaka ( Lk 22,19). Furaha ya kiinjili inaangaza daima juu ya msingi wa kumbu kumbu ya shukrani. Ni neema ambayo tunapaswa kuiomba.”

Ushuhuda wa Kikanisa

Kumbu kumbu inafanya kwa wakati huuu shuhuda wa wengi na kweli. Kati yao kuna baadhi ya watu ambao wameweza kuonesha kwa dhati na kufanya furaha hiyo ya waamini ichanua. Kwa maana hiyo  anataja kuwa Kanisa ni mojawapo, Monastri yeye binafsi anapoisio, katika mji wewnye uweo wa kupyaisha kizazi. Uwezekano wa kujikita ndani ya wakati uliopita, uliopo na ujao kwa upendo wa matumani. Kwa maneno mengine makanisa ni nafasi wazi ambamo anayeinai anahisi ule uhai, maisha yanayosimika mizizi katika kumbu kumbu ya Pasaka ya Bwana Yesu. Abate Gianni Maria kwa njia hiyo ametoa swali, je vijana wahajisi kweli ushuhuda katika makanisa hayo, wanihisi kukumbuku aminifu ambayo inaonesha wakati ujao na mwaminifu?

Uzuri wa kumbu kumbu

Kwa mujibu wa Abate Maria Gianni anathibtisha njia ya kupitia  ni ile ya uzuri wa kumbukumbu, kwa kushinda tabia ya mbaya ya kuona kila kitu ni kibaya, ili kutazamia matumanini ambayo yanatafuta kwa pamoja njia mpya za imani kwa Bwana, kutajirishwa na kiini ambacho kinatokana na utamaduni lakini bila kuogopa. Lazima kuonesha kama alivyokuwa anasema Mtakatifu Yohane Paulo II kwamba uzuri wa kumbu kumbu,ni nguvu ambayo inatokana na Roho na ambaye anatufanya tushuhudie kwa kuwa sisi ni watoto wa shuhuda. Inafanya uone mambo mema kutoka kwao ambayo Roho alipanda ndani ya historia hiyo. Nijinsi gani ilivyo muhimu kwamba jumuiya ya Kanisa vijana wahisi matumanini ambayo yanawaelekeza maisha, katika matarajio  mazuri ambao si kuhisi upweke bali kusindikizwa na jamii nzima na Kanisa.

Wakati ni Mungu

Akizidi kukazia juu ya kumbu kumbu anasema utamaduni unapendekeza mwendelezo na wakati ulipita na ambao unazidi kupanuka hadi kufikia siku ya Bwana na kufunguliwa kwa wakati ujao. Abate Maria Gianni anakumbusha kilichoandikwa tena na Mtakatifu Yohane Paulo II katika Barua yake ya Kitume,Orientale Lumen. “Anasema Kanisa lazima lipambane dhidi ya kishawishi cha kuwa na amri peke yake kwa kile kinachotimizwa na kwa maana ya kujigamba au kujichimbia katika huzuni”.Badala yake kipindi ni Mungu na chochote  kinachotimizwa kisitambulike kamwe kama utimilifu wa ufalme, badala yake ni zawadi ya Bure ya Mungu”. Na kwa mtazamo huo ndipo kuna  onyo zuri ambalo ni mana ya kuwa na imani kubwa yaani umani uliyopyaishwa. Ni kujua kupiga makasia hadi kuupelekea mtumbwi ambao Bwana ametutengeneza bila kuwa na hofu na kubaki na si kubaki umesisima tu kama umegngwa misumari fukweni badala yake ni kuendelea mbele katika wakati ujao bila kuogopa dhini ya msukumo wa roho ya kufikiria mantiki za majivuno.

Tukio moja la pekee ni Pasaka ya Bwana

Leo hii hii kila aina ya tukio linalotokea au maandamano ya aina yoyote ni tukuo lakini  Abate Maria Gianni anatoa onyo kwamba kuna kupoteza machoni petu tukio lilo la kweli. Kurudi katika uzoefu wa utamaduni ulipopyaishwa na kumbu kumbu hai, na ubunifu hasa ule uzoefu wa nguvu kwa ajili yetu na ambao mwisho wa maisha yetu ni Liturujia , kwa maana ya Ekaristi pekee ambayo ni lazima uiwe amnifu na ndiyo tukio moja kwa sababu sisi sote tuna tukio moja na kubwa la ukweli wa  Pasaka ya Bwana Yesu.

Mapatano na wakati uliopo ambao Mungu anatuzawadia

Abate Bernardo Francesco Maria Gianni anahitimisha tafakari lake kwa kuwatikia wawe na radha ya sala, kwamba mafungo yao ya kiroho yawe kumbu kumbu kwa njia ya kusikiliza Neno la Mungu, kuadhimisha liturujiana masifu katika maisha yao kwa sababu ushuhuda  wa kweli uweze kulala juu watu wote wa  nyakati zietu kuwa na upatanisho kwa njia ya uwepo wa Mungu, bila hofu, bila manunguniko na bila kusita kuelekea katika wakati ujao ambapo Bwana anatundalia.

13 March 2019, 13:30