Tafuta

Vatican News
Mafungo ya Kiroho ya Baba Mtakatifu Francisko na ndugu zake huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma Mafungo ya Kiroho ya Baba Mtakatifu Francisko na ndugu zake huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma  (ANSA)

Mafungo ya kiroho:Miji yetu iwe ishara ya amani,udugu na ukarimu

Ndoto ya Giorgio la Pira aliyekuwa Meya wa Mji wa Firenze ndiyo imekuwa tafakari ya asubuhi Jumatatu tarehe 11 Machi 2019 ya Abate Bernardo Maria Gianni kwa Baba Mtakatifu na ndugu zake waliounganika huko Ariccia katika nyumba ya mafungo ya kiroho. Abate anakazia juu kila mji kugundua wito wake duniania na kuwa mwanga juu ya mbingu mpya

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tafakari ya  asubuhi ya tarehe 11 Machi 2019 ya Abate Bernardo Francesco Maria Gianni kwa Baba Baba Mtakatifu na ndugu zake waliounganika katika wiki ya mafungo ya kiroho huko Ariccia nje ya mji wa Roma wamepewa wito wa kutazama sura ya Giorgio La Pira, ambaye alikuwa ni Meya wa mji wa Firenze, mjenzi wa amani na ambayye alikuwa anaota ndoto na alitaka ndoto hiyo iwe ishala ya uzuri, udugu wa kidunia na upendo wa kikristo katika mfano wa Yerusalemu  myoa kama Nabii Isaya anavyoeleza kwenye sura ya 60.

Hata hivyo katika mada hii ya ndoto  Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amekuwa amkumbusha katika ujumbe mzuri alio utoa kwa Baraza la Kipapa la  Maisha anapoandika kuwa: Jumuiya ya binadamu ni ndoto ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Jumuiya ya kibinadamu ni ndoto ya Mungu! Tunaweza kusema namna hii kwamba Giorgio la Pira alikuwa anaota  ndoto ya Mungu. Si katika mchezo wa maneno kwa sababu ndoto yake, shauku yake na ambayo haikutambuliwa haya kwa watu wa Kanisa wa nyakati zile na zidi anasema katika sekta nyingine ya raia wake, lakini yeye alikuwa na mtazamao wa hali ya juu katika fumbo la mji ambao wanauishi.

Padre Abate Maria Gianni anasema, ishara ya jana kama ilivyo ya leo , haikutafakariwa kwa kina katika mji wa  Firenze tu, lakini hata katika miji mingine ya ulimwengu kama nafasi ya mapatano, amani na makutano na ili kufanya lolote kwa kuzuia kujiachia na kukata tamaa hadi hisia za kiza ambacho walifikiri tayari kimeshinda. Kwa maana hiyo Abate anazungumzia pia juu ya huduma ya dunia ambayo inapelekea kila mji kugundua wito wake kwa kweli.  Ni katuka maana ya mwanga wa dunia ambayo ni Yerusalemu mpya mahali ambamo watu wanaisha kwa pamoja wakiongozwa na shauku hai ya matumaini makubwa.

Ni ndoto ambayo inapaswa kuwa ya kila moja, kuwa wazi katika ufunguzi wa upendo kwa matendo  ya Mungu, kutembelea mji, kuupyaisha kuanzia msingi hadi kufikia ncha yake kama alivyokuwa anaandika la Pira. Kwa kufanya hivyo ni kugeuka kuwa msingi kwa ajili ya wema wa mtu, wa kuwa mfumo wa kisiasa, kuwa mfumo wa kiufundi na kiuchumi. Na ndiyo mtazamo wa imani, mtazamo wa kutafakari. Ndiyo ishara inayojaribiwa kuchagua mchakato mpya wa historia takatifu, historia ya Kristo katika dunia, kwa kujaribu kuvumilia licha ya matatizo mengi ya mji wa binadamu na maelewano yake, uzoefu wake na mwanga wa Mungu ambao unatazamia kuja kwa ufalme wa Mungu na kama ilivyo duniani na mbinguni.

Akiendelea kutazama maandishi ya  Girogio La Pira na sehemu ya mshairi Mario Luzi, ambaye anamtafsiri kwa namna maalum ya ndoto, Abate Maria Gianni anaomba kuwa na mtazamo wa  mantiki hiyo katika muundo wa kiraia, lakini pia kwanza katika  Kanisa ambalo linatamani na kuwa na shauku ya Mungu kwa ajili ya watu wote. Kama Kanisa linapaswa kufanya zaidi na si kukata tamaan na ndiyo kujaribu kwa Mungu, bila kujibakiza, kukutana hasa kati yetu.Ndiyo ndoto ambayo taayri ilikuwa mekamilishwa wakati uliopita, ndoto ambayo inapaswa ipanuliwe katika mchakato  wa nyakati zijajo. Kuwa na mtazao ambao unajikita mizizi yake katuka imani ya utatu.  Na inaeleweka kwa sababu ni ishara moja daima na yenye mtindo, ishara ya Roho Mtakatifu amapo kwetu sisi inabaki wakati miwngine kuwa mbali na wazo, lakini ndiyo maisha kwa ajili ya kuishi binadamu wote na inawezekana kuwa chachu ya mageuzi.

Kwa kumaliza sehemu hii ya tafakari ya asubuhi sehemu ya kwanza, Abate anasema, Mungu ambaye anaishi katika nyumba zake, katika barabara zake na katika viwanja vyake. Yeye anaishi kati ya raia wake kwa kuhamasisha mshikamano, udugu, shauku ya wema, ya ukweli , ya haki. Uwepo wake huo hautakiwi ufanyike katika viwanda, bali ugunduliwa na kuoneshwa wazi. Mungu hajifichi kwa wale ambao wanamtafuta, kwa moyo wote, japokuwa wanafanya hivyo kwa njia ya mtindo wa hofu na ambao ndiyo umeenea amehitimisha.

12 March 2019, 09:30