Tafuta

Kongamano la IV la Ekaristi Kitaifa huko Taiwani limehitimishwa kwa Misa Takatifu 1 Machi 2019 Kongamano la IV la Ekaristi Kitaifa huko Taiwani limehitimishwa kwa Misa Takatifu 1 Machi 2019 

Kongamano la Ekaristi Kitaifa nchini Taiwan limehitimishwa!

Kardinali Ferdinando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la uinjilishaj wa watu,ambaye alikuwa mwakilishi wa Papa katika kufunga Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa,Taiwan tarehe 1 Machi 2019 katika mahubiri yake amehimiza umuhimu wa shughuli za kimisionari katika Kisiwa hicho mahali ambapo hali halisi ya Kanisa bado ni changa

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 1 Machi 2019 Kardinali Ferdinando Filoni Rais wa Baraza la Kipapa la uinjilishajiwa watu, ambaye alikuwa mwakilishi wa Papa katika kufunga Kongamano la IV la Ekaristi Takatifu Kitaifa huko Taiwan, katika mwanzo wa mahubiri yake  ameelezea furaha yake ya kushiriki tukio la Kanisa na kuwapa salam za ukaribu wa kiroho wa Baba Mtakatifu Francisko na baadaye kuanza kutafakari maana maneno mawili Kongamano na Ekaristi. Akifafanua anasema neno kongamano,linaturudisha katika kumbukumbu ya tukio kwa namna ya pekee maalum na ambalo ni kama la siku hiyo kwa maana kuunganika kama  wabatizwa wote; neno Ekaristi ni kurudishwa katika  kumbukumbu ya ishara aliyoiweka Yesu mwenyewe na ambayo aliwaachia wafuasi wake na Kanisa lililokuwa linazaliwa wakati huo na ili ishara hiyo iwe ya utambulisho kwa wakristo na waweze kuunganika na Yeye, kuwa familia moja ya Mungu, katika mapatano yaliyo wazi kwa wanaume na wanawake wa kila nyakati, na mahali popote,ikiwa inaunganishwa na sadaka yake kuu ya Yesu aliyetoa  maisha yake  yote kwa Baba yake.

Yesu alifundisha mambo ya Mungu kama baba na mama anaye wapenda

Kardinali Filoni akigusia kuhusu Injili ya Siku, iliyosomwa, amesisitiza kwa ni kwa jinsi  gani umati ulishangazwa na  neno na nafsi yake mwenyewe na kwa maana hiyo walikuwa na shauku ya kumsikiliza hadi kujisahu kwenda kutafuta mahitaji yao kwa sababu, kuzungumnza kwake kama Mungu kulikuwa kuna leta mshangao mkubwa. Kardinali Filoni anasema kilichowavutia watu wa nyakati za Yesu Kristo, ilikua ni kwamba yeye alikuwa anawambia mambo ya Mungu na si kama wazo, ubunifu au mafundisho yaliyo makavu, bali kama baba au mama ambaye anawapenda watoto wake… Yeye alikuwa anaonesha sura ya Mungu kama Mungu hasiye mwacha kiumbe wake au kukosa kuwajali; Mungu ambaye hana ubaridi, wala  utofauti na mateso ya kibinadamu, badala yake alikuwa anashirikishana hali halisi ya kibinadamu.

Kristo aweze kuzungumza na kila hali ya mateso mengi ya watu

Kwa maana hiyo Kardinali Filoni anathibitisha  katika Kongamano hili anapendelae kuwa Kristo aweze kuzungamza nao. Kwana anatamani kwa namna ya pekee anazungumze katika maisha yao wote kuanzia wanandoa ambao hawajijuhi na hawapendani kama ilivyo kuwa mwanzo; kwa mama na baba ambao wamejaa na matatizo ya watoto wao kwa sababu ya madawa ya kulevya na ulevi; kwa yule anayetaabika na ugonjwa wa saratani au magonjwa makuu, kwa yule ambaye hana ajira au fursa na matatizo mengi ya umasikini; na zaidi aweze kuzungumza na wazee au ambao wako hatari ya kifo japokuwa bado hawana utambuzi wa kujua nini  maana ya maisha.

Kongamano la Ekaristi siyo tukio la ziada ni sikukuu ya furaha ya uwepo wa Bwana

Kongamano la Ekaristi  anasema siyo tukio la ziada la kuadhimisha tu, bali ni ukuu wa furaha ya wakati kwa sababu ya uwepo wa Bwana na kukutana na Yesu aliye hai katika Maumbo ya Ekaristi Takatifu. Ekaristi ni zawadi kuu aliyoicha Yesu mwenyewe kwa Kanisa kama kumbukumbu pia ya kujitoa sadaka daima kwa Baba. Akitaja somo la kwanza kutoka kwa Matakatifu Paulo kwa Wakorinto, mahalia ambapo anafafanua juu ya maadhimisho ya Karamu ya mwisho wa maisha yake Yesu, hivyo Kardinali  anasisitiza kwamba Mtakatifu  Paulo kwa namna hiyo anataka kuonesha utimilifu wa fumbo la Uinjilishaji. Isingekuwa inatosha kupeleka ujumbe wa Kristo kwa maneno ya Yesu tu,  lakini pia kulikuwa na ulazima hata wa kutoa Ekaristi katika Jumuiya kwa maana bila matendo ya wokovu utume usingekuwa umekamilika!  Ni kwa njia ya huduma ya utume wa kimisionari wa kutangaza Injili na kuadhimisha Ekaristi ambayo Kanisa lilipata ukamlifu na kuingia mswada wa ushuhuda wa Yesu na utume wake kati ya watu. Ni Ekaristi na kumbukumbu ya kila siku ambayo Kanisa linafanya kwa ajili ya Yesu na kupeleka neema katika jitihada za shughuli za kimisionari.

Katika Kisiwa cha Taiwan, utume wa uinjilishaji uwe wa kushirikishana kwa wote

Kardinali mara baadaya kusisitiza juu ya umuhimu wa shughuli za kimisionari amehimiza kwamba ni  lazima katika kisiwa hicho cha Taiwan mahali ambapo hali halisi ya Kanisa bado ni changa. Japokuwa amebainisha kuwa pamoja na miaka mingi ya uinjilishani na sifa nyingi za shughuli za kijamii kwa upande wa elimu lakini, anasisitizia  kuwa uinjilishaji hawezi kuachiwa kwa baadhi ya wamisionari tu, badala yake  lazima uwaunganishe wate na ushiriki wa maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume, walei, familia  hadi kufikia  utoto mtakatifu wa kimisionari kati yao. Utume wa kimisionari, ukimwilishwa na Ekaristi unaleta matunda ya Kiinjili anasisitiza. Na ndiyo   kisima cha utume wa kuinjilisha anabainisha! Umisionari yaani tangazo la Yesu kwa wote siyo uchaguzi, au wavu wa maisha ya Kanisa badala yeke ni sehemu msingi kwa sababu Kanisa bila pigo linalodunda la kimisionari ni tasa.

 

02 March 2019, 14:54