Tafuta

Vatican News
Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati imeridhia Mkataba na Vatican na unaanza kutumika rasmi tarehe 5 Machi 2019 Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati imeridhia Mkataba na Vatican na unaanza kutumika rasmi tarehe 5 Machi 2019  (Vatican Media)

Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati yaridhia Mkataba na Vatican

Utekelezaji wa Mkataba huu kadiri ya sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwenye Ibara 21§Kipengele cha1, inaweka mambo msingi ya uhusiano kati ya Kanisa na Serikali; kwa kuheshimu na kuzingatia uhuru wa kila upande. Serikali na Kanisa vinapania kushirikiana kwa pamoja katika kukuza na kudumisha: ustawi na maendeleo ya familia ya Mungu Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican pamoja na Rais Faustin Archange Touadèra wa Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Jumanne, tarehe 5 Machi 2019 wamefanya mkutano wa pamoja uliowawezesha kubadilishana nyenzo za kutekeleza Makubaliano ya Mkataba Kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Vatican. Itakumbukwa kwamba, Mkataba huu ulitiwa sahihi kunako tarehe 6 Septemba 2016 huko mjini Bangui, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati.

Mkutano huu, umekuwa ni fursa kwa viongozi hawa kuboresha zaidi utekelezaji wa Mkataba huo kama ulivyofafanuliwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kuwasilishwa kwenye Ubalozi wa Vatican nchini Jamhuri ya Watu wa Afrika ya kati. Utekelezaji wa Mkataba huu kadiri ya sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kwenye Ibara 21§Kipengele cha1, inaweka mambo msingi ya uhusiano kati ya Kanisa na Serikali; kwa kuheshimu na kuzingatia uhuru wa kila upande. Serikali na Kanisa vinapania kushirikiana kwa pamoja katika kukuza na kudumisha: ustawi na maendeleo ya familia ya Mungu Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati katika maisha ya kiroho, kimaadili, kitamaduni na kiutu, kama sehemu ya mchakato wa kutafuta na kudumisha: ustawi, maendeleo na mafao ya wengi!

Mkataba Vatican: Afrika Kati
06 March 2019, 14:38