Tafuta

Baba Mtakatifu na Dk Alessandro Gisotti Baba Mtakatifu na Dk Alessandro Gisotti 

Gisotti:Papa Francisko ni mjenzi wa madaraja katika njia za watu

Katika kuelekea kilele cha miaka 6 tangu Baba Mtakatifu Francisko achaguliwe, kunako tarehe 13 Machi 2013, Msemaji Mkuu wa mpito wa Vyombo vya habari Vatican Dk. Alessandro Gisotti anasimulia kuhusu mtazamo wake wa kina juu utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Francisko kwa miaka sita tangu achaguliwe kuliongoza Kanisa Katoliki.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika kuelekea kwenye kilele cha kumbukumbu ya miaka sita tangu kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu FRancisko kunako tarehe 13 Machi 2013,  Dk. Alessandro Ghisotti Msemaji mkuu wa Mpito wa Vyombo vya habari Vatican amejaribu kuelezea juu ya shughuli za Baba Mtakatifu kwa kipindi hiki cha miaka sita. Dk. Gisotti anasema ni kipindi cha utulivu, umakini kwa watu katika kuwasikiliza na mikutano ambayo kwa hakika ni ufunguo wa shughuli za utume wa Papa Francisko. Ikumbukwe tarehe 13 Machi 2013 mara baada ya kuchaguliwa alitokeza kwenye dirisha la Kati juu ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na kuwasalimia  kwa mara ya kwanza waamini wote walio kuwa wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican kutoka duniani kote, wakisubiri matokeo hayo ya uchaguzi  kwa hamu. Ni tukio ambalo lilijionesha kama safari ya kidugu, ya upendo na matumaini. Hata hivyo ushuhuda huo ulionekana mara baada ya mwezi mmoja katika ziara kwa kuwaona wahamiaji huko Lampedusa kisiwani  nchini Italia. Ziara ambayo aliifanya tarehe 8 Julai 2013, ziara ambayo haikuwa imepangwa bali yeye alihisi ukaribu wa kuwaona ndugu na kutoa heshima kwa waathirika.

Baba Mtakatifu Francisko kwa upande wa wahamiaji anasema ni watu na siyo idadi , Dk. Gisotti anasema, anafanya hivyo kwa sababu ya umakini daima kwa wale ambao kwa bahati mbaya vyombo vya habari vinashughulikia iwapo kuna kipeo kigumu au kuna ajali ya kuzama kwa mitumbwi au hali za dhaura kama vile vita. Zaidi ya ziara yake ya kwanza huko Lampedusa, zimekuwapo ishara nyingi sana za ukaribu wa dhati kwa ajili ya waamiaji , kwa mfano katika ziara yake kwenye kambi ya wakimbizi uko Lesbo hadi kufikia karibu na mpaka wa Morocco. Na wiki chache karibu atakuwa na ziara ya kitume katika Kituo cha Caritas kwa ajili ya wahamiaji: vilevile ziara nyingine ijayo nchini Burgaria na katika Jamhuri ya Macedonia Kaskazini, atakuwa na uzoefu huo huo wa ukaribu kwa maana atatembelea hata kambi ya wakimbizi.

Dk Gisotti aidha anelezea juu ya sifa kuu aliyoifanya huko Bangui, katika ufunguzi wa Mlango Mtakatifu, upatanisho nchini Colombia na Rohingya katika bara la Asia. Vilevile hata miaka sita iliyopita anaonesha ni kwa jinsi gani wote walishangazwa na uchaguzi wa jina la Mtakatifu Francisko wa Asisi, mtu wa amani, maskini na  ambaye alitafuta kwa njia zozote kukuza matumaini katika mtindo wa mazungumzo. Katika muono huo anathibitisha kuwa, inaweza kufikiriwa katika mkutano wa Sultan Al-Kamil Al-Malek  ambaye amekuwa ndiyo  mwongozo wa ziara ya Baba Mtakatifu Francisko, hivi karibuni katika Nchi za Falme za Kiarabu huko Abu Dhabi. Kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu anaonesha kwa dhati heshima ya jina lake katika huduma ya kichungaji. Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko ni mjenzi wa madaraja na mara nyingi anasma Dk. Gisotti kuwa tunasahau ukuu wa mapapa. Kwa hakika Baba Mtakatifu Francisko mara nyingi ameonekana si tu katika maneno, lakini  zaidi kwa njia ya  matendo na ishara hasa mahali penye ukuta na wito wake wa kila wakati wa kutaka kwamba wajenge madaraja na siyo kuta na ndiyo wito wake wa kila mara.

Katika kuelezea juu ya mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa la Mtakatifu Marta mjini Vatican Dk Gisotti  kwa upande  wake anasema ndiyo moyo wa Papa kwa maana Baba Mtakatifu pale anakutana na watu wa Mungu ambao ndiyo jambo msingi kama padre, kama askofu na kama Papa, na  ndiyo Askofu wa Roma. Katika mkutano wa ekaristi na waamini, ndipo mahubiri yanazaliwa ndani ya moyo wake kwa sababu iwapo unakwenda kutazama Hati zake kubwa za kipapa utaona kuwa daima zinajirudia mafundisho au karibu zinakwenda moja kwa moja kutokana na mahubiri yake katika Misa kwenye Knisa la Mtakatifu Marta. Na kwa maana hiyo Dk. Gisotti anaamini kwamba baada ya miaka 6 anaweza kuthibiitsha kweli ni moja ya jambo ambalo ni zuri  na kwa hakika ndiyo moyo wa Kipapa!

Kuhusiana na urafiki wa Papa na Imam Mkuu wa Al Azhar Ahmad Al-Tayyeb na ule wa Patriaki wa Costantinopli Bartholomew I katika mazungumzo yao, Dk Gisotti anabainisha kuwa, tangu mwanzo wa utume wake  Baba Mtakatifu Francisko amezungumzia juu ya utamaduni wa makutano ambapo anajaribu kuuweka katika matendo ya hdati akiwa mstari wa mbele na tema ya urafiki. Hiyo imepelekea Dk. Gisotti kukumbusha alivyoona shauku kubwa na urafiki wa Imam Al Tayyeb wakiwa pamoja huko Abu Dhabi jinsi gani aliwaona wote wawili wakiwa wanatafuta ule ukaribu na utambuzi, hata katika kutia sahini ya makubaliano ya pamoja ya udugu kibidamu. Hii  inaweza kuwa ni ishara ya kinabii na utajiri ambao kwa hakika unavuna matunda, hata utaweza kuvuna ya wakati ujao. Aidha kwa hakika tema ya mazungumzo ni jambo muhimu anathibitisha na kwamba  ni jambo ambalo lipo moyoni kwa Baba Mtakatifu na linaonekana wazi katika mazungmzo  yote mawili na urafiki. Ni urafiki ambao unazaliwa kwa njia ya kukutana na kwa njia hiyo urafiki  kama ilivyo kwa l-Tayyeb, ni pamoja na ule wa viongozi wengi wa kidini na wasiyo wa kidini.

Kuhusiana na suala la ulinzi wa watoto ambapo mkutano umemalizika hivi karibuni, Dk. Gisotti anasema mkutano huo ulikuwa wa lazima. Na wengi walikuwa na wasi wasi juu ya mkutano huokwamba haikuwa mwafaka kuufanya, lakini kwa upande wa Baba Mtakatifu ameonesha ujasiri, hata kwa upande wa Dk. Gisotti pia anathibitisha kwamba huo ni ujasiri wa kinabii kwani ni kwa mara ya kwanza  kukabiliana na kashifa hiyo isiyoelezeka ambayo inaweka hatari na si tu ukosefu wa uaminifu bali hata kw baadhi ya mantiki za utume wa Kanisa lenyewe.

Baba Mtakatifu alitaka kusema hawali ya yottatizo hili la kidunia lazima kutolewe jibu la pamoja duniani. Hata hivyo baadaye kuna tema nyingine ya kujikita katika matendo ya dhati na vipimo vyake. Kwa maana hiyo mwisho wa mkutano uliweza kuwa na azimia la kuanza kujikita katika matendo ya dhati, hivyo Motu proprio itakayotangazwa na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa, itakuwa na maelekezo zaidi ya sheria na hata kuanzishwa kwa nguvu ya kikundi cha  pamoja cha kufuatilia  kwa maana ya wataalam ambao wanaweza kusaidia mabaraza ya Maaskofu kujikita katika shughuli ya kulinda watoto.  Hata hivyo jambo jingine msingi  lazima lielezwe kuhusu Baba Mtakatifu  na ambalo limeonekana ni uongofu wa mioyo na ambao unaazliwa kutokana na kusikiliza waathirika.

 

 

12 March 2019, 12:17