Balozi wa Uturuki Bwana Lutfulla Goktas amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 22 Machi 2019. Balozi wa Uturuki Bwana Lutfulla Goktas amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko, tarehe 22 Machi 2019. 

Balozi wa Uturuki awasilisha hati za utambulisho mjini Vatican

Bwana Lűtfullah Goktas, Balozi mpya wa Uturuki mjini Vatican. Alizaliwa kunako tarehe 16 Desemba 1963 huko nchini Uturuki. Ameoa na ana watoto wawili. Katika maisha yake amewahi kuwa: Mwalimu, Msomaji wa Lugha y Kiarabu; Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea mjini Istanbul na Roma. Mwandishi wa Habari za Televisheni ya Uturuki, NTV na Wakala wa Shirika la Habari la Uturuki.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa, tarehe 22 Machi 2019 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Lűtfullah Goktas, Balozi mpya wa Uturuki mjini Vatican. Alizaliwa kunako tarehe 16 Desemba 1963 huko Balıklıçeşme/Biga nchini Uturuki. Ameoa na ana watoto wawili. Katika maisha yake amewahi kuwa: Mwalimu, Msomaji wa Lugha y Kiarabu; Mwandishi wa Habari wa Kujitegemea mjini Istanbul na Roma. Mwandishi wa Habari za Televisheni ya Uturuki, NTV na Wakala wa Shirika la Habari la Uturuki kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2011.

Bwana Lűtfullah Goktas, amewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Baraza la Mawaziri nchini Uturuji kati ya Mwaka 2011-2014. Kati ya Mwaka 2014 hadi kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Uturuki mjini Vatican alikuwa ni Mshauri na Mkuu wa Idara ya Kurugenzi ya Habari ya Rais wa Uturuki.

22 March 2019, 16:06