Tafuta

Askofu Mkuu Jean Marie Speich ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Slovenia na mwakilishi wa kitume nchini Kosovo Askofu Mkuu Jean Marie Speich ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Slovenia na mwakilishi wa kitume nchini Kosovo 

Askofu mkuu Speich ateuliwa kuwa Balozi wa Slovenia na Kosovo

Askofu mkuu Jean Marie Speich alizaliwa tarehe 15 Juni 1955 huko Strasbourg, Ufaransa. Tarehe 9 Oktoba 1982 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Jimboni Strasbourg. Ilikuwa ni tarehe 17 Agosti 2013, alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ghana na kuwekwa wakfu tarehe 24 Oktoba 2013 na Baba Mtakatifu Francisko, Kanisa kuu la Mt. Petro, mjini Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Jean Marie Speich kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Slovenia pamoja na kuwa ni Mwakilishi wa Kitume nchini Kosovo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Jean Marie Speich alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Ghana. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Jean Marie Speich alizaliwa tarehe 15 Juni 1955 huko Strasbourg, Ufaransa.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 9 Oktoba 1982 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Jimboni Strasbourg. Ilikuwa ni tarehe 17 Agosti 2013, alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Ghana na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu na hatimaye, kuwekwa wakfu tarehe 24 Oktoba 2013 na Baba Mtakatifu Francisko kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Tarehe 19 Machi 2019, Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena akamteuwa kuwa ni Balozi mpya wa Vatican nchini Slovenia na Mwakilishi wa Kitume nchini Kosovo!

20 March 2019, 17:04