Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sudan ya Kusini na ataendelea na utume wake nchini Kenya Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen ameteuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Sudan ya Kusini na ataendelea na utume wake nchini Kenya 

Askofu mkuu Van Megen ateuliwa kuwa Balozi wa Sudan ya Kusini

Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen alizaliwa kunako tarehe 4 Oktoba 1961 huko Eygelshoven, nchini Uholanzi. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 13 Juni 1987. Baba Mtakatifu Francisko, kunako tarehe 8 Machi 2014 akamteua kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 17 Mei 2014 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van MEGEN, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Sudan ya Kusini na ataendelea pia kuwa Balozi wa Vatican nchini Kenya! Hadi wakati wa uteuzi wake, Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria Van Megen alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Sudan na Eritrea. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria van Megen alizaliwa kunako tarehe 4 Oktoba 1961 huko Eygelshoven, nchini Uholanzi.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 13 Juni 1987. Baba Mtakatifu Francisko, kunako tarehe 8 Machi 2014 akamteua kuwa Askofu mkuu na kuwekwa wakfu tarehe 17 Mei 2014 na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican. Kumbe, amewahi kuwa Balozi wa Vatican nchini Sudan na Eritrea. Askofu mkuu ana shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa. Historia inaonesha kwamba, Askofu mkuu Hubertus Matheus Maria Van Megen alianza utume wake katika masuala ya kidiplomasia mjini Vatican kunako tarehe Mosi, Julai 1994. Amewahi kutekeleza utume wake nchini Sudan, Eritrea, Uruguay, Brazil, Yerusalemu, Slovachia; Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva huko Uswiss na hatimaye, nchini Malawi.

20 March 2019, 17:13