Askofu Mkuu Auza wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano wa ngazi za juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu Askofu Mkuu Auza wakati wa hotuba yake kwenye Mkutano wa ngazi za juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maendeleo endelevu 

Askofu Mkuu Auza katika mkutano juu ya mabadiliko ya tabianchi

Askofu Mkuu Bernardito Auza,Mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York,Marekani ametoa hotuba yake katika Mkutano wa ngazi za juu kuhusu tabianchi na maendeleo endelevu kwa wote

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Mkutano wa siku mbili tarehe 28-29 Machi 2019, wa ngazi za juu kuhusu tabianchi na maendeleo endelevu kwa wote, Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu Vatican katika makao ya Umoja wa Matafa mjini New York Marekani ametoa hotuba yake. Baada ya kutoa  salam zake anasema, Vatican inayo furaha ya kuudhuria mkutano wa ngazi za juu kuhusu  ulinzi tabianchi duniani katika kukubali kwa lengo lake juu ya kutafuta ufumbuzi wa vizazi vya sasa na vijavyo.  Hakika, kizazi cha mwanadamu lazima na daima kuhakikishwe usalama  katika mantiki za sasa za mabadiliko ya mazingira. Hata hivyo anasema Baba Mtakatifu Francisko, alikumbusha hayo miaka mitatu na nusu iliyopita katika mkutano  uliofanyika mjini Vatican ya kwamba tunapaswa kufahamu zaidi umuhimu wa kuharakisha na kurekebisha vitendo vyetu ili kuweza kujibu kwa kiasi kikubwa kilio cha masikini duniani. Kwa dhati, huduma ya kweli kwa ajili ya mazingira haihusishi kuwapatia umakini wa nyumba zetu, lakini ni kaka na dada zetu katika nyumba yetu ya oamoja tunayoishi. Kwa hivyo,inahitaji kuzingatia mfumo wa a maadili ya mazingira,wakati huo huo  kujikita kupambana na umasikini, ili kwa pamoja kuweza kuonja furaha za kawaida za kukuza ushirikiano kati ya jamii.

Lazima kuhamasisha njia ya maadili 

Askofu Mkuu Auza akiendelea na hotuba yake anasema, njia hii ya maadili dhidi ya migogoro ya sasa  inapaswa kuhamasisha mshikamano kwa vizazi vijavyo. Kama alivyokuwa amekumbusha Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake ya Laudato Si. “Mshikamano fungamani wa hiari ni jambo  msingi na haki tangu tulipo kabidhiwa na mabo tunatakiwa kuwakabidhi wale watakao fuata baada yetu. Kwa mtazamo huu, tuna jukumu kubwa la kuelekea kizazi cha baadaye, ambacho kinawakilishwa na vijana wa kizazi cha sasa. Katika  uelewa wao mkubwa wa mabadiliko ya hali ya hewa, vijana wanatuonyesha njia, anathibitisha Askofu Mkuu Auza. Vile vile anasema tunapaswa kuepusha kuzaa vizazi vijavyo na  matatizo ya sasa ambapo vizazi vilivyopita vimeundwa kutokana kwa sababu ya kuwa na majukumu ya kutafuta ufumbuzi, na ambao  Baba Mtakatifu Francisko,aliutoa na kuwaalika wasikilize kilio cha maskini katika dunia wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano kuhusu  Malengo ya Maendeleo Endelevu ( tarehe 8 Machi 2019). Baba Mtakatifu katika Wosia wake Laudato Si, akizungumzia juu ya matatizo ya mazingira ambayo pia tumesababisha, amesisitizia juu ya kuwa na jukumu na  kusema kwamba  ingawa kipindi cha kabla ya viwanda kinaweza kukumbushwa kama mojawapo ya wasio wajibika zaidi katika historia ,lakini  kuna haja ya kukumbuka sababu ya kuwa na matumaini ya ubinadamu wa karne ya ishirini  ambayo kwa dhati inakumbukwa kuwa na watu wakarimu na waliokuwa wanabeba majukumu katika mabega yao.

Jitihada za  makubaliano ya Paris na Katowice kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Baada ya hatua za mkutano kuhusu wa mkataba wa Paris na ule wa Katowice, kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Askofu Mkuu Auza anathibitisha kwamba, tuna ufahamu na ni kwa jinsi gani kizaza cha sasa kinaweza kufanya lolote kwa maana ya vitendo. Lakini hadi sasa hatujuhi ni shauku zipi za sera za kisiasa na  hisia za harakati  katika kutekeleza hatua za kupunguza na kukabiliana na suala la mazingiria. Wakati huo huo hata uwekezaji wa kifedha na teknolojia kwa  ajili ya sayari yenye kuwa na afya. Kwa maana nyingine Askofu Mkuu Auza anasema, maamuzi hayo  hayapaswi kuchukua  muda mrefu wakati yanatafuta hali hali za juu zaidi ya afya ya dunia. Lakini mwishoni wa siku, mazungumzo  kuhusu migogoro, lazima yafanyike kwa kwa haraka katuka kujibu hata utabiri wa wanasayansi, hofu ipo hata katika ongezeko la joto, na mambo hayo yawe ndiyo motisha kwa wadau wote ambao wanapambana kwa ajili ya kuokoa mazungira ambayo ni nyumba yetu ya pamoja.

30 March 2019, 12:05