Askofu Mkuu Auza katika mkutano juu ya mabadiliko ya tabianchi
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Katika Mkutano wa siku mbili tarehe 28-29 Machi 2019, wa ngazi za juu kuhusu tabianchi na maendeleo endelevu kwa wote, Askofu Mkuu Bernardito Auza, Mwakilishi wa kudumu Vatican katika makao ya Umoja wa Matafa mjini New York Marekani ametoa hotuba yake. Baada ya kutoa salam zake anasema, Vatican inayo furaha ya kuudhuria mkutano wa ngazi za juu kuhusu ulinzi tabianchi duniani katika kukubali kwa lengo lake juu ya kutafuta ufumbuzi wa vizazi vya sasa na vijavyo. Hakika, kizazi cha mwanadamu lazima na daima kuhakikishwe usalama katika mantiki za sasa za mabadiliko ya mazingira. Hata hivyo anasema Baba Mtakatifu Francisko, alikumbusha hayo miaka mitatu na nusu iliyopita katika mkutano uliofanyika mjini Vatican ya kwamba tunapaswa kufahamu zaidi umuhimu wa kuharakisha na kurekebisha vitendo vyetu ili kuweza kujibu kwa kiasi kikubwa kilio cha masikini duniani. Kwa dhati, huduma ya kweli kwa ajili ya mazingira haihusishi kuwapatia umakini wa nyumba zetu, lakini ni kaka na dada zetu katika nyumba yetu ya oamoja tunayoishi. Kwa hivyo,inahitaji kuzingatia mfumo wa a maadili ya mazingira,wakati huo huo kujikita kupambana na umasikini, ili kwa pamoja kuweza kuonja furaha za kawaida za kukuza ushirikiano kati ya jamii.
Lazima kuhamasisha njia ya maadili
Askofu Mkuu Auza akiendelea na hotuba yake anasema, njia hii ya maadili dhidi ya migogoro ya sasa inapaswa kuhamasisha mshikamano kwa vizazi vijavyo. Kama alivyokuwa amekumbusha Baba Mtakatifu Francisko katika barua yake ya Laudato Si. “Mshikamano fungamani wa hiari ni jambo msingi na haki tangu tulipo kabidhiwa na mabo tunatakiwa kuwakabidhi wale watakao fuata baada yetu. Kwa mtazamo huu, tuna jukumu kubwa la kuelekea kizazi cha baadaye, ambacho kinawakilishwa na vijana wa kizazi cha sasa. Katika uelewa wao mkubwa wa mabadiliko ya hali ya hewa, vijana wanatuonyesha njia, anathibitisha Askofu Mkuu Auza. Vile vile anasema tunapaswa kuepusha kuzaa vizazi vijavyo na matatizo ya sasa ambapo vizazi vilivyopita vimeundwa kutokana kwa sababu ya kuwa na majukumu ya kutafuta ufumbuzi, na ambao Baba Mtakatifu Francisko,aliutoa na kuwaalika wasikilize kilio cha maskini katika dunia wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu ( tarehe 8 Machi 2019). Baba Mtakatifu katika Wosia wake Laudato Si, akizungumzia juu ya matatizo ya mazingira ambayo pia tumesababisha, amesisitizia juu ya kuwa na jukumu na kusema kwamba ingawa kipindi cha kabla ya viwanda kinaweza kukumbushwa kama mojawapo ya wasio wajibika zaidi katika historia ,lakini kuna haja ya kukumbuka sababu ya kuwa na matumaini ya ubinadamu wa karne ya ishirini ambayo kwa dhati inakumbukwa kuwa na watu wakarimu na waliokuwa wanabeba majukumu katika mabega yao.
Jitihada za makubaliano ya Paris na Katowice kuhusu mabadiliko ya tabianchi
Baada ya hatua za mkutano kuhusu wa mkataba wa Paris na ule wa Katowice, kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Askofu Mkuu Auza anathibitisha kwamba, tuna ufahamu na ni kwa jinsi gani kizaza cha sasa kinaweza kufanya lolote kwa maana ya vitendo. Lakini hadi sasa hatujuhi ni shauku zipi za sera za kisiasa na hisia za harakati katika kutekeleza hatua za kupunguza na kukabiliana na suala la mazingiria. Wakati huo huo hata uwekezaji wa kifedha na teknolojia kwa ajili ya sayari yenye kuwa na afya. Kwa maana nyingine Askofu Mkuu Auza anasema, maamuzi hayo hayapaswi kuchukua muda mrefu wakati yanatafuta hali hali za juu zaidi ya afya ya dunia. Lakini mwishoni wa siku, mazungumzo kuhusu migogoro, lazima yafanyike kwa kwa haraka katuka kujibu hata utabiri wa wanasayansi, hofu ipo hata katika ongezeko la joto, na mambo hayo yawe ndiyo motisha kwa wadau wote ambao wanapambana kwa ajili ya kuokoa mazungira ambayo ni nyumba yetu ya pamoja.