Tafuta

Padre Leopoldo Ndakalako ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Menongue nchini Angola. Padre Leopoldo Ndakalako ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Menongue nchini Angola. 

Padre Leopoldo Ndakalo ateuliwa kuwa Askofu wa Menongue, Angola

Padre Leopoldo Ndakalako alizaliwa tarehe 13 Desemba 1968 kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Menongue nchini Angola. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kwenye Seminari ya Kristo Mfalme Huambo na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko Roma, alipewa Daraja ya Upadre hapo tarehe 14 Desemba 1997. Amewahi kuwa Gombera na Makamu Askofu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Leopoldo Ndakalako aliyezaliwa kunako tarehe 13 Desemba 1968 kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Menongue nchini Angola. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kwenye Seminari ya Kristo Mfalme Huambo na Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, kilichoko Roma, alipewa Daraja ya Upadre hapo tarehe 14 Desemba 1997. Katika maisha na utume wake kama Padre, amewahi kuwa: Makamu wa Gombera, Seminari na Paroko-usu wa Parokia ya “Nossa Senhora das Vitorias-Sé Catedral”.

Kati ya Mwaka 1999-2003 akatumwa na Jimbo kuendelea na masomo ya juu, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na hatimaye, kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Falsafa. Kati ya Mwaka 2003-20016 amekuwa ni Gombera wa Seminari kuu ya Moyo Safi wa Bikira Maria nchini Angola. Kati ya Mwaka 2012-2017 akateuliwa kuwa Makamu wa Askofu na kuanzia mwaka 2017 hadi kuteuliwa kwake, amekuwa ni Makamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Ondjiva na Msimamizi wa Parokia ndogo ya Sào Antònio Naipalal, Jimbo Katoliki la Ondjiva, nchini Angola.

Kanisa Angola

 

19 March 2019, 15:04