Tafuta

Vatican News
Padre Joseph Eciru Oliach ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Soroti, nchini Uganda. Padre Joseph Eciru Oliach ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Soroti, nchini Uganda. 

Pd. Joseph Eciru Oliach, Askofu mpya wa Jimbo la Soroti, Uganda

Padre Joseph Eciru Oliach kutoka Jimbo Katoliki la Soroti, Uganda ameteuliwa kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Soroti, Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule alikuwa ni Jaalim na mlezi katika Seminari kuu ya Kitaifa ya Ggaba. Alizaliwa kunako mwaka 1970, huko Gweri, Madera, Jimbo la Soroti. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, akapewa Daraja ya Upadre tarehe 9 Agosti 2003.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Joseph Eciru Oliach kutoka Jimbo Katoliki la Soroti, Uganda, kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Soroti, Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule alikuwa ni Jaalim na mlezi katika Seminari kuu ya Kitaifa ya Ggaba. Alizaliwa kunako mwaka 1970, huko Gweri, Madre, Jimbo la Soroti. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, katika Seminari kuu ya Mtakatifu Thomas Aquinas, huko Katigondo na Taalimungu katika Seminari ya Mtakatifu Paulo, huko Kinyamasika, akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kunako mwaka 2003.

Katika maisha na utume wake kama Padre ametekeleza dhama na utume kama ifuatavyo: Paroko-usu, Mwalimu na mlezi wa seminari ya Mtakatifu Paulo. Kati ya Mwaka 2006-2009 akatumwa na Jimbo kujiendeleza katika Sayansi ya Maandiko Matakatifu katika Taasisi ya Biblia, maarufu kama “Biblicum”, iliyoko mjini Roma. Kati ya Mwaka 2009-2012 akahitimu masomo yake kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Maandiko Matakatifu. Baada ya kurejea nchini Uganda, akapewa dhamana ya kuwa mlezi pamoja na kufundisha Maandiko Matakatifu katika Seminari kuu ya St. Mary’s, iliyoko Ggaba, Jimbo kuu la Kampala, Uganda. Tangu mwaka 2006 hadi kuteuliwa kwake, alikuwa pia mkurugenzi wa Deski la Maandiko Matakatifu, Baraza la Maaskofu Katoliki Uganda.

Jimbo la Soroti
19 March 2019, 15:24