Tafuta

Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Diamantino Guapo Antunes, I.M.C. kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tete, Msumbiji. Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Diamantino Guapo Antunes, I.M.C. kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tete, Msumbiji. 

Padre Diamantino Antunes ateuliwa kuwa Askofu wa Tete, Msumbiji

Askofu mteule Diamantino Guapo Antunes, I.M.C alikuwa ni Mkuu wa Kanda ya Shirika la Waconsolata nchini Msumbiji na Angola. Alizaliwa tarehe 30 Novemba 1966 huko Ureno. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 19 Septemba 1993 akaweka nadhiri zake za daima, huko Maua, nchini Msumbiji. Tarehe 20 Julai 1994 akapewa Daraja ya Upadre huko Fatima, nchini Ureno.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Diamantino Guapo Antunes, I.M.C, wa Shirika la Waconsolata kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tete nchini Msumbiji. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Diamantino Guapo Antunes, I.M.C alikuwa ni Mkuu wa Kanda ya Shirika la Waconsolata nchini Msumbiji na Angola. Itakumbukwa kwamba, alizaliwa tarehe 30 Novemba 1966 huko Ureno. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikuhani, tarehe 19 Septemba 1993 akaweka nadhiri zake za daima, huko Maua, nchini Msumbiji.

Tarehe 20 Julai 1994 akapewa Daraja ya Upadre huko Fatima, nchini Ureno. Katika maisha na utume wake kama Padre na Mtawa amewahi kuwa mlezi, mkuu wa nyumba, Paroko na Mshauri wa Kanda ya Shirika la Waconsolata nchini Msumbiji. Kati ya Mwaka 2007 hadi mwaka 2014 alikuwa ni Makamu wa Askofu Jimbo Katoliki la Inhambane. Kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka 2017 amekuwa ni Mkuu wa Shirika la Wamisionari wa Consolata nchini Angola na mtoa hoja katika mchakato wa kuwatangaza Makatekista mashuhuda wa imani kutoka Guiùa.

22 March 2019, 16:16