Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ameteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa Balozi wa Vatican huko New Zealand. Wakati wa uteuzi wake alikuwa Balozi wa Honduras Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ameteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa Balozi wa Vatican huko New Zealand. Wakati wa uteuzi wake alikuwa Balozi wa Honduras 

Ask.Mkuu Novatus Rugambwa Balozi mpya wa New Zealand!

Tarehe 29 Machi 2019 Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi mpya wa Vatican nchini New Zealand Mheshimiwa sana Askofu Mkuu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Balozi wa Vatican nchini New Zealand na mwakilishi wa Kitume wa Bahari ya Pwani, Mheshimiwa sana Askofu Mkuu  Rugambwa. Kabla ya uteuzi wake alikuwa ni Balozi wa Vatican huko Honduras.

Askofu mkuu Novatus Rugambwa alizaliwa tarehe 8 Oktoba 1957, Katika Jimbo Katoliki Bukoba, Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya kikasisi, alipewa daraja Takatifu ya Upadre kunako tarehe 6 Julai 1986. Baada ya kufanya kazi mbali mbali katika Balozi za Vatican, kunako tarehe 6 Februari, 2010, Baba Mtakatifu mstaafu  Benedikto XVI, alimteua kuwa  Askofu mkuu na Balozi wa Vatican nchini Angola, Sao Tome na Principe. Na tarehe 5 Machi 2015 aliteuliwa kuwa balozi wa Vatican huko Honduras, ambapo sasa  tarehe 29 Machi  2019, ameteuliwa kuwa  Balozi wa Vatican huko  New Zealand na mwakilishi wa Kitume wa Bahari ya Ocean.

29 March 2019, 13:47