Tafuta

Wanaparokia wa  Mtakatifu Crispino wa Viterbo mjini Roma wanamsubiri kwa hamu sana Baba Mtakatifu tarehe 3 Machi 2019 Wanaparokia wa Mtakatifu Crispino wa Viterbo mjini Roma wanamsubiri kwa hamu sana Baba Mtakatifu tarehe 3 Machi 2019 

Ziara ya Papa Francisko katika Parokia ya Mt.Crispin wa Viterbo

Baba Mtakatifu atatembelea Parokia ya Mtakatifu Crispino wa Viterbo kwenye mtaa wa Offanengo,huko Labaro mjini Roma tarehe 3 Machi 2019. Wanaparokia wako tayari kumpokea kwa shangwe kuu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 3 Machi 2019 Baba Mtakatifu atakwenda katika Kanisa la Mtakatifu Crispino wa Viterbo kwenye mtaa wa Offanengo,n 6  huko  Labaro mjini Roma. Anatarajiwa kufika majira ya saa 10 jioni massa ya Ulaya na kupokelewa na Kardinali Angelo De Donatis Makamu wake Papa, Askofu Msaidizi Guerrino di Tore, Padre Luciano Cacciamani na mapadre wote wanaotoa huduma yao ya kichungaji katika parokia hiyo. Baba Mtakatifu anatarajia kuwa na mkutano na watoto na vijana, familia za watoto wadogo waliopata ubatizo, watu wasio kuwa na makazi, wagonjwa na walemavu.

Paroko anathibitisha kuwa kila kitu cha maandalizi ya kumpokea Baba Mtakatifu katika Parokia ya Mtakatifu Crispino wa  Viterbo ni tayati. Katika ratiba ya  parokia mkutano wa kwanza na Baba Mtakatifu utakuwa ni wa  sekta ya vijana. Hao ni watoto ambao wanaudhuria katekisimu ya maandalizi ya kupokea komunio ya kwanza na Kipaimara, vijana ambao wamekwisha pokea kipaimara na wanaudhuria katika mafunzo. Walio wadogo zaidi watampokea Baba Mtakatifu kwa wimbo na kusoma barua yao waliyoiandaa kwa ajili ya fursa hiyo.

Padre Cacciamani anasema wakati vijana wakubwa watauliza baadhi ya maswali ,wataomba ushauri na kujaribu kuondoa wasiwasi wao. Aidha Baba Mtakatifu atakutana na wazazi wa watoto waliopokea au wako katika maandilizi ya kupokea ubatizo. Baadaye ataondoka na kuingia katika chumba kingine mahali ambamo atakutana na watu karibia 30 wasiokuwa na makazi na ambao wanasaidiwa na Caritas ya Parokia na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio. Pamoja nao watakuwapo watu wa kujitolea. Pia atakutana na watu wagonjwa na walemavu wa Parokia ya Mtakatififu Crispino.  Hatimaye atasalimiana na mapadre wa jumuiya hiyo na kutoa nafasi ya maungamo kwa baadhi ya waamini. Mwisho wa ziara hiyo utahitimishwa na Misa Takatifu. Na ili kuwawezesha ushiriki wa mkubwa wa jumuiya mbele ya Parokia watawekwa luninga kubwa  kuwasadia wote washiriki mubashala kwa kile kitakachokuwa kinaendelea ndani ya Kanisa.

Kuna ushauku kubwa ya kutaka kukutana na Papa Francisko amethibitisha Paroko na  kwamba wote wako wanajitahidi kusafisha kila kona ili kufanya nyumba na jumuiya yao iwe ya makaribisho makubwa. Kwa upande wao anathibitisha, ni ishara ya kutiwa moyo kwa ajili ya kuendelea kutoa huduma yao vema na kutohisi upweke. Itakuwa ni fursa nzuri kwa ajili ya kukaribia imani katika baadhi ya watu ambao wamekwenda mbali na Kanisa.

26 February 2019, 12:36