Tafuta

Vatican News
Papa ataadhimisha misa na washiriki wa mkutano kuhusu hali halisi ya mapokezi ya wahamiaji huko Sacrofano Roma tarehe 15 Februari 2019 Papa ataadhimisha misa na washiriki wa mkutano kuhusu hali halisi ya mapokezi ya wahamiaji huko Sacrofano Roma tarehe 15 Februari 2019 

Tarehe 15 Februari Papa ataadhimisha Misa huko Sacrofano Roma

Bwana Alessandro Gisotti Msemaji Mkuu wa pito, vyombo vya habari Vatican amethibitisha kuwa Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Misa Takatifu tarehe 15 Februari 2019 saa 10.00 jioni masaa ya Ulaya kwenye Jumuiya ya Domus huko Sacrofano,Roma kama sehemu ya umakini wa mapokezi ya wahamiaji

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 12 Februari 2019, Bwana Alessandro Gisotti Msemaji Mkuu wa pito wa vyombo vya habari Vatican amethibitisha kwamba katika kusisitizia mara kwa mara juu ya umakini wa mapokezi ya wahamiaji, Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Misa Takatifu tarehe 15 Februari 2019 saa 10.00 jioni masaa ya Ulaya kwenye Jumuiya ya Domus huko Sacrofano Roma. Hiyo ni  misa ya  ufunguzi rasmi wa Mkutano unaojikita kutazama hali halisi ya sasa kwa kuongoza na madao ya  mapokezi huru dhidi ya hofu. Ni mkutano ulioandaliwa na Chama cha Migrantes, Caritas ya Italia na Kituo cha Astalli katika wa siku mbili tarehe 15 -17 Februari 2019. Ziara hii itakuwa na tabia ya kifaragha kwa uwepo wa waandishi na wahudumu wa mwasisliano japokuwa misa takatifu itahudumiwa na vyombo vya habari Vatican.

Taarifa kutoka chama cha Migrantes juu ya mkutano tarehe 15-17 Februari 2019

Naye mhusika wa maadalizi haya nathibitisha kwamba Mada inayoongoza mkutano huo huko Sacrofano ni mapokezi huru dhidi ya  hofu, mkutano wa familia na vyama vinavyojihusisha na mapokezi ya wahamiaji na wakimbizi. Ni Mkutano uliondaliwa na Caritas Italia, chama cha Migrantes na Kito cha Astalli. Naye mhusika wa maandalizi hayo anathibitisha kwamba ni kipindi ambacho wanataka kusema asante kusaidia na kuwatia moyo, kwa maana wengi wanaendelea mara nyingi kwa kujitoa bure hata kugusa mifukoni mwako ili wendelezea roho hiyo ya mapokezi na mshikamano.

Watu anajitolea na hata kuota sadaka zao

Ni katika familia, parokia, vyama  na hali halisi ambavyo wamechagua kukaribisha au kushirikisha wahamiaji walioko ndani ya nchi na ili kukutana kwa pamoja  ili  kishirikiana uzoefu na ushuhuda wao wanao uishi katika suala hili la mapokezi. Katika mkutano huo wanataka kutoa ujumbe wa matumaini katika nchi ya Italia. Kukutana kwa karibu na wahamiaji, kuwafahamu, kuwashika mkono, siyo hali halisi na mbaya au ya kupoteza wakati na ambayo mara nyingi walio wengi wanasukimiza pembeni. Kinyume chake  ni uzoefu wenye utajiri mkubwa na wenye uwezo wa kutoa chachu mpya ya nguvu ya maisha. Mkutano umefunguliwa kwa wote wanaojikita katika jitihada za mapokezi au ushirikishwaji kwa wahamiaji. Katika ratiba ya mkutano huo wanatazamiwa kuwa na vipindi vya sala, tafakari, tamasha ,shuhuda wasanii wa utamaduni, kazi ya makundi na michezo mbalimbali. Na mwisho watatoa ujumbe kwa nchi na kuwaaaga washiriki wa mkutano huo utakao fungwa  na Padre Camillo Ripamonto Rais wa Kituo cha Astalli.

12 February 2019, 15:33