Kila tarehe 2 Februari ni siku ya watawa duniani ambao wanawakilisha na wito maalum wa kumfuasa Kristo Kila tarehe 2 Februari ni siku ya watawa duniani ambao wanawakilisha na wito maalum wa kumfuasa Kristo 

Siku ya watawa ni kama mwili ulivyo mmoja lakini viungo ni vingi

Maisha ya kitawa yameundwa na watawa wa kike na kiume,ambayo ni hali halisi kama mwili,maana viungo ni vingi lakini hufanya mwili mmoja.Ni maneno ya Askofu Mkuu Jose Rodriguez Carballo,Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume,katika fursa ya Siku ya Watawa tarehe 2 Februari 2019

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Hali halisi ya siku ya watawa ni kama mwili, kwa maana kama vile mwili ulivyo mmoja na wenye viungo vingi lakini hufanya mwili mmoja  (1 Kor 12,12-30). Utafouti hujionesha kwa haraka na kusifiwa katika maisha ya utawa. Maisha haya yameundwa na watawa wa kike na kiume: kuna maisha ya kimonasteri, wake na waume, mashirika ya kilei na vyama vya kitume, watawa wasiokuwa na wigo na waeremiti. Hata hivyo pia kuna changamoto nyingi zinazowakilishwa katika maisha ya kitawa na wingi wake unaweza kuhatarisha maisha yao. Kati ya changamoto hizo muhimu ni ile ya ukosefu wa muungano na udugu. Na mojawapo nyingine iliyo mbaya zaidi ni ile inayoibuka bila kuwa na mpangilio. Ndiyo mwanzo wa maelezo ya Askofu Mkuu Jose Rodriguez Carballo Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na vyama vya kitume wakati wa fursa ya Siku ya XXIII ya Watawa inayofanyika kila mwaka ifikapo tarehe 2 Februari, sambamba na Siku kuu ya Kutolewa Bwana Hekaluni.

Changamoto ya udugu

Katika Gazeti la Osservatore Romano linatoa taarifa yake kamili akifafanua juu ya changamoto zinazokabili maisha ya utawa, ambapo Askofu Mkuy Carballo anasema udugu unawakilishaw kama moja ya kiini msingi cha maisha ya kitawa. Maisha ya kidugu katika jumuiya ni unabii na ni mahali ambapo kuna utume. Yote hayo yanaanzia na zawadi ya kutambua kuwa kaka na dada. Kama asemavyo Mtakatifu Francisko wa Assisi kwamba:“Bwana alinipatia ndugu”. Na katika mtindo huo, undugu unatambua kujitoa bure kwa kaka na dada na siyo kuishi kama  kampuni,wala wazalishaji. Udugu kwa urahisi upo kwa ajili ya kuwa familia moja kati yao, kupendana,kumwilishwa kama mama anavyo mwilisha mwanae. Udugu una radha ya uhusiano binafsi. Hakuna maisha ya kidugu katika jumuiya bila kuwa na uhusiano binafsi wa dhati. Udugu unatambua kwa dhati usawa katika utofauti kama Yesu alivyosema, “ninyi nyote ni ndugu” ( Mt 23,8). Hata hivyo katika jumuiya mara nyingi inajitokeza changamoto kubwa katika hatua ya maisha ya pamoja hasa ya ukosefu wa hatua ya uhusiano wa dhati na ambao kuna ulazima wa kuongeza huduma inayotoa radha na chachu ya mawasiliano ya kina.

Na changamoto nyingine ya kidugu katika jumuiya ni ile ya kuweza kutafuta kuwa wajenzi kidugu na siyo kama sehemu ya kuwatumia na kunyonya, kwa maana hiyo inahitajika kukuza uhusiano chanya kati ya watu wa jumuiya na kuunda matumaini, kuvumilia uchungu, kukaribisha maisha, kuwa na wakati mwafaka na kusahihishana kindugu kwa dhati na upendo. Yote hayo ni kwa ajili ya kusaidia na kuwa na umakini kwa wengine kama vile wadhaifu, wazee, wagonjwa,masikini ambao ndiyo mwili wa Kristo. Katika dunia ambayo imegawanyika, maisha ya kitawa mbele yake yana wajibu muhimu na maalum, hasa katika kuunda na kutoa chachu, kuhamasisha jumuiya za kindugu ili ziweze kuchanua urafiki kwa kuwa na chachu chanya, kusaidaia mapatano bila kusahau maisha ya kindugu na kujenga na kuinua maisha yaliyo madhaifu ya kibinadamu. Katika dunia ya leo, na Kanisa linawataka watawa ambao ni wataalum wa umoja wawe ishara ya kuaminika na uwepo wa Roho, wawe wasanii wa mpango wa umoja na kuishi kwa kusali, kukutana na kuzungia barabara zote katika mtindo wa kutembea pamoja lakini kwa mujibu wa Mungu.

Kuenea kwa mtindo wa utamaduni wa dini mpya zenye misimamo mikali

Askofu Mkuu Carballo anaonesha pia wasiwasi mkubwa juu ya kuenea kwa utamaduni mpya wa dini zenye misimamo mikali  ambazo ni sawa na kutokuvumilia,itikadi kali,ubaguzi na kuongezeka zaidi kwa aina za ishara za aina hiyo. Kuenea kwa itakadi mpya za dini ni tukio la dharura katika jamii ya sasa ambazo, lakini si ngeni katika Kanisa na wala maisha katika utawa  wenyewe, anathibitisha Askofu. Katika  maisha ya kitawa mitindo mipya inaingia sana kwa upande wa kuamini wale ambao wana madaraka ambapo kwa taratibu wanachukua nafasi ya Mungu. Na kwa taratibu kutokana na sababu ya taalimungu wanaitumia kwa manufaa yao binafsi na ambayo hawezi kuwekwa katika ukatoliki, bali inajitambulisha kwa mwanzilishi au mkuu na karama yake. Waanzilishi hawa kwa kawaida wanadai ndiyo wenye kuwa  Roho Mtakatifu.

Hatari ni kubwa kwa maana ya kila neno au mwanzilishi linafikiriwa kama ni neno litokalo katika Roho Mtakatifu. Hii ni hatari kwa maana ni rahisi kubadilika kuwa udikteta, ni hatari sana katika msingi wa dini. Matokeo yake unaonekana haraka katika mfumo wa utawala wake kwa maana yote yanajikita katika nguvu ya utalawa na kila maamuzi yoyote yanatokana na mwanzilishi. Uwepo wa makundi kama haya katika maisha ya utawa, ni dhahili kuona kwamba yako mbali na harufu nzuri ya Injili. Madaraka hayaendani na mantiki ya Injili bali ni ya ulimwengu huu (Mt 20, 25-27). Huwezi kuishi utii kwa kusikiliza tu wasio kuwa na mantiki ya kiinjili bali ni lazima kusikiliza jumuiya binafsi,kuwa na  maamuzi mwafaka na katika kujishusha chini; kung’amua hakufanyiki katika tendo la kutafuta dhana ya kiinjili mazungumzo na  ishara za nyakati binafsi, bali ni kama zana ili kufanana na kile ambacho kinatoka juu; karama inatambuliwa katika mwenendo.

Maisha ya watawa wanafuata wakati endelevu na kufuata wito wa Yesu

Maisha ya kitawa ni wito wa msamaria, yana kiu ambapo hayawezi kwenda katika visima vyenye nyufa visivyoweza kuhifadhi maji (Yer 2,13). Kuna haja ya kwenda mara kwa mara katika kisima cha maji hai (Yh 4,14). Kwa kutazama wakati endelevu, maisha ya kitawa lazima yajifunze usanii wa ubunifu mwaminifu (Evangelii gaudium,33); lazima kujifunza kupendekeza kwa ujasiri na kuanza upya, kubuni na utakatifu mara nyingi vimekuwa ndiyo tabia; lazima kukwepa itakadi na kila aina ya ishara itokanayo na itikadi hizo na ambazo zinaumiza moyo wa Injili (Gaudete er exultate,100-103).

Karama ni kama maji. Maisha ya utawa lazima yafanye kumbukumbu lakini zaidi yazae matunda na kufanya kumbukumbu ya kutoka ( Kumb 26) ambayo inaruhusu kwenda katika mzizi kwa namna ya kuruhusu kuishi utawa wa upendo ambao unatazama  kwa dhati wakati ujao kwa matumaini. Wakati ujao wa maisha wa kutazama mambo mengi na kufanya mang’amuzi. Ni kwa njia ya mang’amuzi yanaweza kuhakikisha ukovamavu wa kuweka wakfu. Bila mang’amuzi mtawa ana mapungufu makubwa mno, kwani anakosa ukomavu katika utawa. Iwapo watawa wanataka kujibu utume wa kuangaza dunia hawawezi kuanguka na kufanana na jumba la makumbusho, bali lazima waache washangazwe daima na mapya ya Roho, ambaye anaruhusu kufanya mambo yote kuwa mapya ( Mdo 21,5).

Maisha ya utawa kwa upande wa wote na wakati endelevu unataka kuhakikisha matunda ya kiinjili ambapo lazima kutoa kipaumbele cha makutano na Yesu kwa kutambua kuwa nguvu ya wito ni Kristo na kisima cha furaha ya kweli. Ni lazima kutoa kipaumbele cha umoja na watu wa Mungu na kuepuka vishawishi vya kutaka ukuhani, ili kuweka karama kwa pamoja, utume na unabii; kutafuta kila wakati mtindo wa mang’amuzi na kupendelea zaidi nafasi ya masikini. Maisha ya kitawa leo hii lazima yachukue wajibu  ambao ni kipindi cha kutembea na kusikiliza wito wa Yesu, akitamka: “simama na tembea"(Lk 5,25).

/content/dam/vaticannews/pam/audio/agenzie/netia/2019/02/05/13/ask-carballo-utawa-134858030.mp3
04 February 2019, 14:12