Baba Mtakatifu alitembelea Kambi ya mauaji ya kinyama huko Auschwitz - Birkenau Baba Mtakatifu alitembelea Kambi ya mauaji ya kinyama huko Auschwitz - Birkenau 

Mons.Urbanczyk:Siku ya kumbukumbu ya mauaji,Auschwitz

Kila mwaka Ulimwengu mzima unakumbuka Siku kukombolewa waathirika katika mauaji ya kinyama kwenye kambi ya Auschwitz ambapo iIlikuwa ni tarehe 27 Januari mwaka 1945.Hiyo ilikuwa ni kambi kubwa ya mateso na kuwaangamiza watua,iliyojengwa na Wanazi wakati wa Vita Vikuu ya Pili ya Dunia

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kila mwaka Ulimwengu mzima  unakumbuka Siku kukombolewa waathirika wa mauaji ya kinyama katika kambi ya Auschwitz ambapo ilikuwa ni tarehe 27 Januari mwaka 1945. Auschwitz ilikuwa kambi kubwa kabisa ya mateso na ya kuwaangamiza watu, tena ya kutisha kabisa, iliyojengwa na Wanazi wakati wa Vita Vikuu ya Pili ya Dunia. Katika kambi hiyo mauaji yalifanyika kwa ustadi wa kinyama. Vyumba vya gesi na matanuri makubwa ya kuchomea watu yalijengwa na kuwa viwanda vilivyo chukua si chini ya roho za watu milioni moja!

Tarehe 27 Januari 1945 ni ya kukumbuka sana

Kumbukumbu ya mauaji kiholela ndiyo ajenda ya kikao cha 1214 cha Baraza la Kudumu OSCE, ambapo  mwakilishi wa  Kudumu wa Vatican, katika Baraza hilo Monsinyo Janusz Urbanczyk  ametoa hotuba yake huko Vienna  tarehe 31 Januari 2019. Alianza kwa kumshukuru Mwenyekiti kutoka Italia wa Shirikisho la kimataifa la Kumbukumbu ya mauaji ya kikatili katika fursa ya kukombolewa kwa wafungwa na kukombolewa kambi ya mauaji AuschwitzBirkenau, kunako tarehe 27 Januari 1945, ambapo anathibitisha kwamba, siku hiyo inatazamwa kimataifa kama Siku ya kumbukumbu ya Yom Hashoah, yaani kukombolewa Kambi ya Mateso ya Auschwitz kutoka kwa majeshi ya SS ya Wanazi wa Kijerumani.

Katika Siku hizi ni kukumbuka siku za kutisha za mateso anaongeza Monsinyo Janusz Urbanczyk  na maangamizi dhidi ya wayahudi kabla na baada ya Vita Kuu ya wanazi. Ni kukumbuka maelfu na maelfu na waathirika wengi kutokana na unyama wa Wanazi. Roma na Sinti, watu wa mataifa madogo na wanaoamini katika imani yao. Na zaidi  hii Monsinyo Urbanczyk anasema ni kuwapongeza wale wote wanaohusika katika mchakato wa haki kati ya Mataifa na wote wanaondelea kuwalinda kutokana tishio la kuishi kwao. Leo hii hii kuna haja ya kuwakumbuka kwa dhati na kuwaheshimu waathirika, japokuwa  pia inapaswa kuwahudumia kwa makusudi thabiti.

Tukio hili linapaswa kuhakikisha kwamba siku za nyuma zinatoa fundisho ili kutorudia tena nyuma. Kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema miezi iliyopita kwamba, mauaji ya kinyama lazima yakumbukwe ili kufanya kumbukumbu ya maisha ya zamani. Bila kuishi na kumbukumbu, hakuna wakati endelevu iwapo kurasa nyeusi za historia hazitufundishi kuepuka makosa ya wakati uliopita, hadhi ya binadamu itabaki imekufa katika maandishi. Lengo kama hilo haliwezi kuwa la kawaida wala kuhalalishwa leo hii, kwa vile tunapaswa kutambua kwamba mateso ya chuki na unyanyasaji, bado yanaathiri familia ya wanadamu na kuendelea kuondoa nguvu zao katika jamii zetu na wakati huo huo ni kutoa wito wa dharura kwa kibinadamu haraka na muhimu.

Masikitiko ya Vatican kuhusiana na mabaki ya mbegu ya ukatili leo hii

Kadhalika Monsinyo Janusz Urbanczyk ameonesha masikitiko yake, kuona kwamba leo hii ukatili na mbegu zimezidi kuongezeka dhidi ya Shoa,na bado zipo katika jamii na hivyo ni  jukumu la kukumbuka na umuhimu wake  ili  kuongeza  jitihada za kila mmoja katika  kuepuka kurudia mateso ya kizamani. Akiendelea kusisitiza umuhimu wa siku hii ya Kumbukumbu ya mauaji ya kinyama, Monsinyo Urbanczky anasema, Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Salam zake kwa wawakilishi wa Kongmano  la Kimataifa la Mlima wa Wayahudi, tarehe 5 Novemba 2018, aliwakumbusha kuwa, kuhusisha vijana ni moja ya kipengele muhimu katika juhudi za kulinda na kuhifadhi wakati ujao katika kukumbuka ya zamani.

Kiukweli chombo cha kuleta ufanisi zaidi wa kupambana na ubaguzi wa kiyahudi na kutoheshimu utu wa binadamu unawezekana kupambana kwa njia ya elimu ambayo inapaswa kuwaongoza vijana ili kuwa na mahusiano na wengine,kusikiliza na kushirikisha,kuwa na subira na kuheshimu,kusaidiana na kuishi kwa pamoja. Mafundisho sahihi, makusudi na makini sana juu ya Uyahudi katika familia na katika ngazi zote za elimu, yanafanya kazi muhimu hasa katika kuondoa ujinga na kupambana dhidi ya ubaguzi mbaya, dharau, na mambo mengi yanayosababisha kwa urahisi chuki na kudhoofisha utu wa binadamu kwa ujumla.

Viongozi wa kisiasa na wa kidini,pamoja na sura nyingine za umma,pia wanapaswa kuwa na jukumu la kuendeleza ushirikiano wa pamoja,ambao ni pamoja na kuzungumza kwa nguvu zote mara moja wakati matukio ya kupambana na ubaguzi unapojitokeza. Kwa kuhitimishaMonsinyo anawahakikishia kwamba Vatican inashutumu vikali kila aina ya mtindo wa kizamani na wa leo wa ubaguzi dhidi ya wayahudi. Uwakilishi wake unaungana mkono kufanya kumbukumbu na kwamba yasisahauliwe kamwe mauwaji ya halaiki dhidi ya wayahudi (Holocaust) ambayo ni ya kinyama ili kuweza kutoa fundisho muhimu katika kukuza heshima ya hadhi ya kila binadamu.

/content/dam/vaticannews/pam/audio/agenzie/netia/2019/02/05/14/mons-urbanczky-134858076.mp3
04 February 2019, 16:14