Cerca

Vatican News
Dhana ya Ujumbe wa Kwaresima 2019 unajionesha juu ya wokovu wa binadamu na uhuru dhidi ya ubaya na dhambi  kutokana na laana anayoteseka nayo Dhana ya Ujumbe wa Kwaresima 2019 unajionesha juu ya wokovu wa binadamu na uhuru dhidi ya ubaya na dhambi kutokana na laana anayoteseka nayo 

Mkutano kwa vyombo vya habari kuhusu Ujumbe wa Papa wa Kwaresima

Tarehe 26 Februari 2019 umefanyika mkutano kwa waandishi wa habari kwa ajili ya uwakilishaji wa Ujumbe Kwaresima 2019 wa Baba Mtakatifu Francisko ambapo Kardinali Peter Turkson amethibitisha kwamba,matendo ya binadamu yanaleta matokeo ya hatima ya kazi ya uumbaji

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 26 Februari 2019, Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson Peter Rais wa Baraza la kipapa la Huduma ya  Maendeleo fungamani ya watu akiwa na Katibu msaidizi Monsinyo Segundo Tejado Muñoz, wamewakilisha kwa vyombo vya habari Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Kwaresima 2019. Kardinali Turkson anasema tendo la binadamu kuumbwa katika dhambi imeleta matokeo yake katika sayari hii, kwa maana hiyo inahitajika mabadiliko binafsi katika hatima ya kazi ya uumbaji.

Mantiki ya Ujumbe anasema Kardinali  

Viumbe vyote vinangojea kwa hamu Mungu awadhiihirishe watoto wake, ndiyo mada iliyochanguliwa na Baba Mtakatifu ambayo imetolewa katika Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Warumi. Kardinali Turkson anaeleza kuwa kazi ya uumbaji ina shauku ya kina na ambayo inaonesha kwa wana wa Mungu kwa sasabu  kama wamekuombolewa watafanya yaliyo mema hata viumbe. Dhana ya ujumbe wa mwaka 2019 wa Kwaresima inajionesha kuwa wokovu wa binadamu na uhuru dhidi ya ubaya na dhambi katika kujieleza kwa njia ya wokovu wa viumbe vyote kutokana na  laana mbaya  ambayo  anateseka kwa sababu ya dhambi ya binadamu.

Manyanyaso ya viumbe ni dhambi

Iwapo hatma ya matendo yetu yanatamani kazi ya uumbaji, maana yake ni kwamba wokovu una nguvu ya kuyabadili matokeo hayo. Kwa maana hiyo Kardinali anazungumza juu ya kizazi na wokovu dhidi ya dhambi, ikiwa na maana hata ya mazingira na wakati ujao kwa wale ambao watakuja baada yetu ili waweza kukuta hali  bora zaidi. Kardinali Turkson anasema, kukomaa na kukua kwa sura ya Kristo ambayo imo ndani mwetu inatuongoza katika kizazi cha utukufu wa wana wa Mungu anbao upo pamoja nasi, hata cha viumbe. Hayo ndiyo mazingira ambayo yanapaswa kuwekea jitihada zetu katika kipindi cha Kwaresima mwaka huu nathibitisha. Kwa kufanya uzoefu wa kila siku katika dhambi ya binadamu, sisi sote tumekuwa na uwezekano wa kuwa na  neema ya wokovu wa Kristo na zawadi ya Roho Mtakatifu ambaye anatoa taratibu  muundo wa maisha yetu na kutuongoa katika utukufu wa kuwa wana wa Mungu, kama Barua ya kwanza ya Mtakatifu Petro isemavyo  kuwa: “Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikiria upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa Neno la Mungu lenye uzima na lidumulo hata milele”. ( 1Pet 1,22-23)

Kaka yake yuko wapi? 

Naye Monsinyo Muñoz, Katibu wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungani ya watu amesema, tunapaswa kubadilika mara kwa mara, kubadilisha mwelekeo wa maisha yetu ili kufikia Pasaka hii. Kwa mujibu wake anaamini kwamba ni lazima kusisitizia  njia ya matendo makuu matatu ambayo Kanisa daima limekuwa likihubiri. Matendo hayo ni kufunga, kutoa sadaka na kwa sala. Kila mara tunapojikatilia sisi wenyewe, anasema tunaunda ule ubaguzi kama asemavyo Baba Mtakatifu Francisko ya  kwamba ni kuunda ubaguzi, wa kumweka mwingine pembezoni,iwe katika familia, katika kazi au katika jamii. Kwa maana hiyo uongofu  wa kweli ni ule wa kuanza kumtazama mwingine na kujiuliza kama Mungu alivyo muuliza Kaino  yuko wapi kaka yako? Ni swali pia ambalo Mungu alimuuliza hata Adamu huko wapi? Kwa maana hiyo ni kusema yuko wapi ndugu yako na sawa sawa na wewe huko wapi ?

Kufanya kazi kwa njia mpya

Wakati wa kuwakilisha ujumbe huu kwa kuongozwa na Baraza la Kipapa  la huduma ya maendeleo fungani ya binadamu  alikuwapo ha mwakilishi wa Kampuni ya Eni ambayo ina dhamana ya kuimarisha mazungumzo kati ya makampuni muhimu ya nishati,wawekezaji na wadau wenginemuhimu ambao wanasaidia kupambana na  umasikini mkubwa wa nishati inayo wakumba bilioni na milioni 1000 ya watu katika ongezeko kwa asilimia  (30%) ya mahitaji ya nishati kufikia 2030 na matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa. Bwana Alberto Piatti ambaye ni makamu rais wa kampuni ya Eni ametoa ushuhuda wake unaotazama ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko na kuthbitisha kuwa  wamekuwa na muda wa kukabiliana kwa pamoja mwezi Juni mwaka jana na kwamba  wanasubiri kikao kipya, mwezi Juni mwaka huu. Na kwa maana hiyo anasema hii ni fursa muhimu ya kufikiria kwa upya utamaduni wa kufanya kazi kwa kuzingatia kwamba sisi ni walinzi wa bustani hiyo na tunapaswa kuiacha ikiwezekana katika hali bora zaidi.

 

26 February 2019, 16:08