Tafuta

Vatican News
Kardinali George Pell amevuliwa nyadhifa zake zote na ameanza kutumikia adhabu yake jela, huku akisubiri rufaa yake itakayoanza kusikilizwa tarehe 13 Machi 2019. Kardinali George Pell amevuliwa nyadhifa zake zote na ameanza kutumikia adhabu yake jela, huku akisubiri rufaa yake itakayoanza kusikilizwa tarehe 13 Machi 2019. 

Kardinali Pell avuliwa nyadhifa zake, aanza kutumikia kifungo!

Baba Mtakatifu amemvua madaraka Kardinali George Pell, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uchumi kuanzia sasa! Zote hizi ni hatua madhubuti zinazoendelea kuchukuliwa na Kanisa ili kuhakikisha kwamba, kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo haijirudii tena katika maisha na utume wa Kanisa! Kanisa linajenga mazingira salama kwa malezi na makuzi ya watoto.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Mahakama nchini Australia baada ya kumtia hatiani Kardinali George Pell, mwenye umri wa miaka 77 kwa kupatikana na makosa matano ya kunyanyasa watoto wadogo, kwenye miaka 1990 wakati alipokuwa Askofu msaidizi wa Melbourne kati ya mwaka 1987-1998, amenyimwa dhamana na ameanza kutumia adhabu yake kwenye Jela ya Assessment iliyoko Mlebourne nchini Australia. Rufaa yake inatarajiwa kusikilizwa tarehe 13 machi 2019.

Kwa makosa ya Kardinali George Pell, kila kosa lililotendwa linastahili adhabu ya kifungo cha miaka 10 jela, lakini Kardinali Pell hadi wakati huu anaendelea kusema kwamba, hana hatia kutokana na shutuma zote zinazoelekezwa dhidi yake! Vatican inasubiri hukumu ya mwisho itakayotolewa na Jopo la Majaji watatu, baada ya Kardinali Pell kukata rufaa! Ili kuhakikisha kwamba, haki inatendeka, Baba Mtakatifu Francisko kwa kuchukua tahadhari, kuanzia sasa amemsimamisha Kardinali George Pell kufanya shughuli za kichungaji hadharani na wala haruhisiwi kukutana tena na watoto wadogo kadiri ya sheria, kanuni na taratibu zilizoko!

Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, Baba Mtakatifu amemvua madaraka Kardinali George Pell, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uchumi kuanzia sasa! Zote hizi ni hatua madhubuti zinazoendelea kuchukuliwa na Kanisa ili kuhakikisha kwamba, kashfa ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo haijirudii tena katika maisha na utume wa Kanisa! Huu ni wakati wa Kanisa kuendelea kujikita katika ukweli na uwazi, kwa kushirikiana na watu pamoja na taasisi mbali mbali ili kuhakikisha kwamba, Kanisa linajenga mazingira salama kwa malezi na makuzi ya watoto! Juhudi hizi pia zinapaswa kuungwa mkono na watu wote wenye mapenzi mema, ili hata jamii ziweze kujenga mazingira bora zaidi kwa ajili ya maisha ya watoto wadogo!

Kard. Pell
27 February 2019, 09:25